A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Nadhani uko sahihi, lkn kabla hatujalinganisha afrika na mzungu, hebu fikiria maisha ya kijijini kwenu na mjini kwanin watu wanaishi nyumba za udongo miaka nenda miaka rudi, hivi kutengeneza tofari lile la udongo na kulichoma kunahitaji teknolojia kubwa, je fundi ujenzi anahitaji malipo makubwa kweli? ukitafakari hilo kwa kina utagundua wa afrika ni wavivu sana wa kufikiri.Fikiria kwann tununue nguzo za umeme south Africa, kwann tununue njiti za meno china, kwanin tununue chanuo/kitana china, kwanin tununue kijiko, mwiko kutoka china?
 

Huko ndio kubweteka kwenyewe sasa. Watu wetu wameridhika kuishi maisha ya shida, maisha ya kutokuthubutu, hatutaki kutoka nje ya box tunataka kubaki humo hadi 'mwisho wa dunia'. Wazungu walithubutu. Na huwezi kuzungumzia maendeleo bila kulinganisha.
 
Hoja ya mleta mada ni ya msingi sana. Na inafikirisha.

Tangu tupo shule tumekuwa tukiambiwa sababu za waafika kutokuendelea kuwa ni Wakoloni ndio walisababisha. Na ukihoji mbona wao walishaendelea kabla ya kuja Africa ndio majibu haya kuwa mazingira yao hasa hali ya hewa ndiyo yalichangia.

Haya, tukiangalia sasa baada ya hao wakoloni kuondoka je lipi jipya tumefanya au kugundua na ni kwanini hakuna jipya, SASA HIVI LAWAMA ZINAELEKEZWA KWA SERIKALI .

Binafsi naamini utofauti uliopo sio ktk rangi tu bali hata KIAKILI, TUKUBALI TU.
Najua wapo watakaosema mbona tukiwa darasani na hao wazungu huwa tunawaburuza. Akili ninayoiongelea ni ya kugundua kitu kipya na sio yakufundishwa kilichopo.


Chunguza Tabia na Akili ya mtu Mweusi yeyote duniani hapa utakuta zinafanana tu.Si Wamarekani weusi waliozaliwa karne nyingi huko wala Mzigua au Mjaluo wa Kenya
 
saafii kabisa mkuu@
 
rafiki umeandila kwa ustadi wa hali ya juu
 
Nawaza tu vitu Kama vile meli ndege na vinginevyo vilivumbuliw miaka ya 1807 huko wakati sisi tuna ambiwa miaka ya 1880 tulikuwa tunavaa magome ya miti sasa tungemtawala vp mwenye akili kutuzidi
 
Na vyeti walikuwa navyo hapo darajani?
 
Wee vp unaongelea Nyerere wa juzi, ubatakiwa kuvuta hisia kuanzia miaka ya 500 kurudi nyuma (500-0) hapo katikati Elimu, Dini, masoko, fedha tulikuwaje ukilinganisha mzungu.
 
maisha ya Afrika hayakuwa ya taabu; kwa hiyo walikuwa wanajitosheleza kivyaovyao na hawakutaka kutafuta namna nyingine ya maisha. Taabu za maisha ya Ulaya ziliwafnaya wazungu wawe wanapigana wao kwa wao kunyangnyana raslimali na kutumikishana wao kwa wao kama mafungwa hadi wakafikia kugundua sila za moto na usafri wa majini wa harak kwende kushambuklia wenzao. Walipogundua kuwa Afrika kuna watu wengi sana ambao hawana silaha za aina hiyo ndipo wakatumia mwanya huo.. Ukisoma historia ya Ulaya utagundua kuwa hawakuwa na amani kwa muda mrefu sana kabla ya kuanza kuiteka Afrika. Na hata yale makubalinao yao ya Berlin ilikuwa ni mwendelezo huo huo wa kujaribu kuzuia wasije wakatwangana tena.
 
Hili ndio jibu sahihi
 
Bravo! Umewaza sana kwa sauti mkuu.. Hii ndo sababu pekee ya wao kutuzidi kimaendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…