A Boiling Conflict Between Rwanda, Uganda, and Burundi.

I know what we are missing. Good leadership or just leadership at that.
 
Marekebisho kidogo kabla ya kujibu hoja zako.
Vita ya Vietnam iliisha mwaka 1975 siyo 1972
Afghanistan Urusi ilitoka mwak 1989 na siyo 1989
Vita vya Mogadishu ni vya mwaka 1993.

Kuhusu hoja yako sasa:
Jeshi bora ni lile ambalo linakuwa na wanajeshi walifundishwa vizuri na kuwa vifaa vya kisasa kabisa. Huku wakiwa na Reserve ya kutosha katika ngazi ya kijeshi na kiraia ili kuweza kufanya mambo yawe marahisi wakati wa vita. Lakini bahati mbaya sana jeshi linaweza kuwa ni la kisasa lakini likashindwa kupigana vita na maadui.

Kazi ya jeshi siyo kujisifia tu kwamba lina vifaa bali ni kupigana vita na kulinda mipaka.
Hivyo leo hii tukisema Tanzania ana jeshi lenye nguvu halafu tukapigwa na Al-Shabaab tunaweza kujisifu kwamba tuna jeshi Imara hata kama tuna vifaa vya kisasa kabisa ??? Sasa hapo Ubora wetu utakuwepo wapi ??? Au mwenzangu ubora wa jeshi unapima kwa kuwa na bajeti na vifaa vya kisasa tu ??? Maana wewe umeangalia silaha na vifaa (The Ballistic Side) vipi kuhusu (Mission) ambako kuna vitu vingi zaidi ya silaha na uchumi ???
 

Pale Congo DRC walioruhusu Tanzania waende walikuwa ni Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) ambapo ndani yake kuna Marekani, Uingereza na Ufaransa. Tanzania waliongoza vikosi lakini walienda kama majeshi ya Umoja wa Mataifa chini ya MUNISCO INTERVENTION BRIGADE. Kazi yao ilikuwa ni kuwapiga M23 na kuhakikisha kwamba hali ya amani inarudi kwenye ule ukanda ambapo walikuwepo waasi na siyo zaidi ya hapo. Hivyo kitaalamu Tanzania ilikuwa ni Troop Contributing Country (TCC) ambapo wanajeshi wake walifuata maagizo ya Umoja wa Mataifa japo waliruhusiwa kupiga waasi.

Kuna mengi sana hapa yamefichika, ngoja nikae vizuri ntakuja kuchangia.....
 
Karibu uzidi kumwaga nondo mkuu maana wengi hapa jf tulikua tunajua baada ya M23 kupigwa basi maslahi ya Rwanda yaliguswa directly.

By the way M23 nimeona majuzi wamelalamikiwa na Machali yule Muasi wa kule Sudan kwamba Salva kiir anawatumia kwny vita.
 
Maj Gen Godefroid Niyombare
===
Nani hasa alimtuma kufanya mapinduzi ya kijeshi!?
Na mimi unajiuliza hili swali hata sipati , kwamba niyombare alisimama Kwa ajiri tuu ya kutokubaliana na regime ya Nkurunzinza?
 
You are contradicting your self brother .......but thanx for the correction g9te byee
 
Niliwahi kusema huyo Slim anafanya kila namna ili atawale Afrika Mashariki na baadae Afrika!
Sasa kamkalia kooni mchunga ng'ombe wa Geita ila avune Mererani
Mambo ni Moto,na tatizo kubwa ni Mr Slim.
 
.."(Kikwete) clearly stated that such a military move would not be tolerated by Tanzania"...

Mhh!
So, if the attempted coup in Burundi had succeeded, JWTZ would've gone into a second "Kagera War"
JWTZ iende mara ngapi?
Bila JWTZ Nkurunzinza ingekuwa story!
 
Kuna rafiki yangu alikuwa anaishi karibu na Ubalozi wa USA Dsm, aliwahi kupigiwa simu na walinzi wa ubalozi (akiwa amesafiri nje ya dsm bila kuwaaga maana hakuwa na mazoea nao) kuwa kuna majambazi walitaka kuvamia nyumbani kwake lakini walinzi hao wa US Embassy wamewadhibiti. Huwa wako siriazi na kazi, they spy everywhere all the time for their nation's welfare
DGSE, FRENCH External Intelligence Agency.
How come wanaonekana kujishughulisha na Internal Affairs za baadhi ya nchi za Great Lakes Region?!, halafu sio kujisghulisha tu, mpaka ku spill the beans, i.e the allegedly assassination plot ya Museveni?
 
Mimi haya mambo siyafahamu lakini ninachoweza kusema ni kwamba kweli maslahi ya Rwanda yaliguswa baada ya kupigwa kwa M23 kwasababu umoja wa mataifa ulisema kwamba kile kikundi kilikuwa kinaongozwa na Rwanda. Japo kukipiga kile kikosi hakukugusa maslahi ya mataifa makubwa yanayonufaika na rasilimali za Congo: Makampuni makubwa kutoka Ulaya na Marekani yanavuna madini Congo bila hata kutumia M23 na yalianza tokea miaka ya 1960's.

Katika picha kubwa:
Chanzo cha matatizo na migogoro mikubwa kwenye ukanda wa maziwa makuu siyo Raisi Paul Kagame na Raisi Musevenni, haya matatizo yalikuwepo kabla yao na yataendelea kuwepo hata siku ambayo Raisi Paul Kagame na Raisi Musseveni wanaondoka madarakani. Tatizo kubwa kwenye huu ukanda ni MASLAHI YA MATAIFA YA KIBEPARI: Maslahi ya kiuchumi, Kimkakati na Kiushawishi, hivyo binafsi nadhani tutakuwa tunakosea kudhani kwamba Raisi Kagame ndiyo chanzo cha haya matatizo.

Lazima tusome historia na tufahamu kwamba Raisi Kagame na Raisi Musseveni ni Pawns in a greater chess game. Waziri wa Ufaransa Benard Debre alishawahi kusema haya kuhusu mgogoro wa Rwanda "What one forgets to say is that, if France was on one side, the Americans were on the other, arming the Ugandans, who armed the Tutsis. I don’t want to portray a showdown between the French and the Anglo-Saxons, but the truth must be told"

NB: Hivyo tukumbuke kwamba hata uvamizi wa RPF nchini Rwanda miaka ya 1990's uliratibiwa na British MI6. Kutungua kwa ndege ya Hyabarimana mwaka 1994 mpango ni CIA kwasababu kuna nyaraka zinasema RPF waligoma kufanya hivyo lakini ilibidi watii wakubwa zao. Kumfukuza Mobutu Sese Seko mwaka 1997 iliratibiwa na CIA. Kumshughulikia mzee Kabila mwaka 2001 ushahidi mkubwa unasema ni CIA, hivyo hawa wakina Raisi Paul na Raisi Joel ni vikaragosi tu vya mataifa makubwa.

Hata kupeleka vikosi nchini Congo ilikuwa ni ubishi wa Benard Membe tu, lakini TISS wakishajua hii historia vizuri walishauri vikosi vya Tanzania visipelekwe hata kutuliza hiyo amani. Tuangalie maslahi yetu ya ulinzi tu na hayo mengine tuwaachie wao wenyewe na tamaa zao, lakini kama ilivyo kawaida ya Tanzania yetu (Siasa na maslahi binafsi yaliwekwa mbele ya utaalamu)
 
They could not say it all the way it was. Umewahi kujua kwanini haswa Nguza Vick na vijana wake walihukumiwa that way?
 
Exactly!
 
Bina unitafsirieee
 

Niko vizuri ndugu Nalendwa.
Huku utashangaa sana lakini mbali na DGSE kuna CIA, MOSSAD, BND, BOSS (Apartheid Intelligence) na Chinese Intelligence.
Kuna miaka ya nyuma MOSSAD walishawahi kuzinguana na Shirika la Kijasusi la Uchina nchini Congo: Kuna kipindi hadi majasusi ya MOSSAD walikamatwa na majasusi ya Uchina, yakafungwa na kutupwa kwenye mto wenye mamba na ujumbe ukapelekwa Tel Aviv (Just crazy)

Ukisoma kwenye The Encyclopedia of Politics by Rodney P Carlise, Johh P Murphy kutoka American Military University anasema haya kwenye ukurasa wa 594 "The war saw the introduction of unique surrogates on both sides , as Cuban mercenaries supported the Communist liberation forces in the fighting in Angola and the Israel MOSSAD carried on a bitter struggle against the Chinese in Congo" Israel na Uchina walipigana vibaya sana nchini Congo kisa maslahi sema kuna mambo huya hayasemwi tu. Miminilikuja kuambiwa haya mambo mwaka 2010 ndiyo nkajua kumbe kuna mchezo mchafu sana unaendelea hapa Afrika.

Nadhani kuna andiko la zamani sana lilizungumzia hiyo Spy Affair baina ya Uchina na Israel walivyokuwa wanaviziana kimafia. Nikilipata ntaliscan na ntakuwekea hapa uone jinsi ambavyo haya matatizo yana mzizi mrefu.

CC: zitto junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…