Kagame is ruthless lakini siamini kwamba amekuwa mjinga kiasi cha kufanya kosa la lutaka kumuua Msevenni mchana kweupe huku akijua dhahiri kwamba mambo mabaya yanaweza kutokea baada ya hilo jaribio. Kama kujifunza tu, RPF walijifunza somo gumu sana kwenye lile tukio la mwaka 1994 (Hyabarimana na Cyprian) na sidhani kama wanaweza kurudia kirahisi hasa kipindi hichi ambacho macho mengi yanamwangalia.
Maswali ya kujiuliza hapa kwa mtazamo wangu ni haya:
1. Je, kama Kagame angetungua hiyo ndege ya Musseveni, Je ni kwa faida ya nani ???
2. Jarida linatuambia kwamba kwasababu ya kisasi dhidi ya Musseveni baada ya kumgeuka, lakini hili lina ukweli wowote ule ??? Maana kama ni kisasi basi angeanza na Raisi Jakaya Kikwete na Tanzania ambao waliingia moja kwa moja Congo DRC kuwapiga M23 na pia wao ndiyo walimrudisha Pierre Nkhurunzinza madarakani kwa mabavu. Kama kisasi basi angeanza na Tanzania na siyo Uganda (Hili linatia sana ukakasi)
NB: Rwanda hawezi kufanya kitu chochote cha kijinga bila kupewa ruhusa na wafadhili wake, maana wao utulivu wa Rwanda ni faida kubwa sana kiuchumi kwao. Hivyo wataleta mbwembwe zote lakini vita siyo rahisi kabisa (Too much is at stake), Rwanda atafanya vurugu kubwa pale tu ambapo maslahi ya wakubwa yataguswa (Kumbuka yaliyomkuta Raisi Laurent Kabila baada ya kutaka reforms za kuwagusa wakubwa nchini Congo) : Nchi kama Tanzania, Burundi na Uganda zinaweza kuwepo nchini Congo lakini huwa zinajua dhahiri mipaka yao linapokuja swala la maslahi ya wakubwa.