Niko vizuri ndugu Nalendwa.
Huku utashangaa sana lakini mbali na DGSE kuna CIA, MOSSAD, BND, BOSS (Apartheid Intelligence) na Chinese Intelligence.
Kuna miaka ya nyuma MOSSAD walishawahi kuzinguana na Shirika la Kijasusi la Uchina nchini Congo: Kuna kipindi hadi majasusi ya MOSSAD walikamatwa na majasusi ya Uchina, yakafungwa na kutupwa kwenye mto wenye mamba na ujumbe ukapelekwa Tel Aviv (Just crazy)
Ukisoma kwenye The Encyclopedia of Politics by Rodney P Carlise, Johh P Murphy kutoka American Military University anasema haya kwenye ukurasa wa 594 "The war saw the introduction of unique surrogates on both sides , as Cuban mercenaries supported the Communist liberation forces in the fighting in Angola and the Israel MOSSAD carried on a bitter struggle against the Chinese in Congo" Israel na Uchina walipigana vibaya sana nchini Congo kisa maslahi sema kuna mambo huya hayasemwi tu. Miminilikuja kuambiwa haya mambo mwaka 2010 ndiyo nkajua kumbe kuna mchezo mchafu sana unaendelea hapa Afrika.
Nadhani kuna andiko la zamani sana lilizungumzia hiyo Spy Affair baina ya Uchina na Israel walivyokuwa wanaviziana kimafia. Nikilipata ntaliscan na ntakuwekea hapa uone jinsi ambavyo haya matatizo yana mzizi mrefu.