Hapana mzee; uwezo wa kijeshi siyo directly proportional na uchumi, na wala katika maelezo yangu hayo sikutumia kigezo cha mwaka 1970 bali nimekupa mfano wa kuonyesha kuwa wingi wa silaha na ukubwa wa jeshi (manpower) havina uhusiano na uwezo wa kupigana vita. Unaposoma takwimu za wingi wa silaha na manpower zisikudanganye kuwa huo ndio uwezo wa jeshi; hapana. Uwezo wa jeshi umo katika utaalamu wa kupanga na kuendesha mapigano ambao unatokana na training ya makamanda wake. Makamanda wa jeshi la JWTZ wana training kali sana kuliko jeshi lolote ukanda wetu huu. Pitia safu za uongozi kwa maafisa wote kuanzia Brigedia Jenerali na kuendelea ndipo utagundua kuwa training zao siyo mchezo mchezo. Marekani na israel unazosema, zina training kali sana kwa makamanda wao, siyo silaha na uchumi tu kama unavyodhani. Kama unajua mambo ya kijeshi sawasawa, utakubali kuwa ushindi wa israeli dhidi ya majirani zake miaka ile ulitokana na jinsi makamanda wa israeli walivyopanga vita hizo siyo ukubwa wa jeshi wala ukubwa wa uchumi, in fact Israel ilikuwa maskini sana wakati huo wala haikuwa hata na TV yake yenyewe kulinganisha na majirani zake wote.