figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
A.C KATIKA GARI IMEUNDWA NA VIFAA KADHAA AMBAVYO VYOTE KWA PAMOJA UFANYA KAZI YA UZALISHAJI WA BARIDI KATIKA GARI
1.A.C COMPRESSOR
Kifaa hiki kinatumika katika ufuaji wa ubaridi katika A.C.
2.A.C CONDENSER
Kifaa hiki hutumika katika upoozaji wa gesi katika AC
3.A.C EVAPORATOR
Kifaa hiki hutumika katika kugandisha ubaridi kwenye mfumo wa upoozaji.
4.EXPANSION VALVE
Kifaa hiki hutumika katika kulinganisha gesi ya kiasi kikubwa na kiasi kidogo.
5.RECEIVER DRIER
Kifaa hiki hutumika katika uchujaji wa gesi katika A.C
6.HIGH PIPE
Kifaa hiki hutumika katika kupitgisha gesi kwenye mfumo wa A.C ikiwa ya moto.
7.LOW PIPE
Kifaa hiki hutumika katika kupitisha gesi kwenye mfumo wa A.C ikiwa ya baridi
8.THERMOSTART
kifaa hiki hutumika katika kupumzisha compressor pindi hewa inapokuwa kali(baridi sana au joto sana).
9.AC FILTER
Kifaa hiki hutumika katika kuchuja vumbi lisiingie ndani ya gari na kuchafua mfumo wa hewa.
10.BLOWER FAN
Kifaa hiki hutumika katika kutengeneza hewa na kupeleka katika overporator.
11.SPEED CONTROL
Kifaa hiki hutumika katika kuongeza na kupunguza kasi ya blower fan.
12.CONDENSOR FAN
Kifaa hiki hutumika katika kusaidia kupooza condensor ili ipishe gas kwa wepesi
14.COMPRESOR A.C OIL
Ni mafuta yanayosaidia katika ulainishaji wa ndani ya piston.
15.VACUUM SILENCE
Kifaa hiki hutumika katika kupandisha na kushusha ukimya (silence) na sauti ya injini pindi uwashapo A.C.
16.PRESSURE SWITCH
Kifaa hiki hutumika katika kuwasha compressor na feni ya condenser pindi uwashapo A.C.
"Elimu kuhusu usalama barabarani ni jukumu letu sote"