Young Kibaka
JF-Expert Member
- Oct 6, 2012
- 319
- 46
Duu zipo nyingi ila ukienda kwenye menu ya JF kuna option ya SEARCH, hapo bofya ID yangu utazipata
Unamaanisha meditation? Maisha yetu chuoni yalijaa meditation lakini ile ya kukaa kimya kwenye lotus posture (yenye maumivu mengi sana) ilikuwa ni dk 50 kila siku lakini pia tulikuwa na meditation retreats za siku 3,5 na 7
Kwa kiasi fulani nimeongelea ishu za ajabu ajabu lakini ndani ya Buddhism kuna mengi mazuri na yenye faida nyingi, namaanisha Buddhism kama philosophy na sio kama dini
1: CHAKULA
hiki ni kitu kinachoheshimiwa mno ndani ya Buddhism, sio kila mtu ana Neema ya kuenjoy utamu wa chakula, ale ashibe
Ndani ya Buddhism chakula ni ibada, na mikalangizo yote ya chakula ni kwasababu ya kiungo kidogo sana ULIMI, lakini ndani ya Buddhism chakula ni dawa chakula ni ibada kwahiyo hatupaswi kuchagua chakula
Huwa kuna kitu cha ajabu sana na cha kijinga nakiona sehemu nyingi...!!!! Watu kubakisha chakula.. Ndani ya buddhist college ilikuwa ni mwiko mkubwa kubakisha chakula... Pakua unachomaliza, usile ukabakisha hakuna aliye tayari kula makombo, lakini vilevile ni kwamba wakati wewe unabakisha kuna mtu anahitaji japo robo ya hicho ulichobakisha...TAFAKARI
2:MAJI
Hapa Africa tuna matumizi mabaya sana ya maji, hatujali serikali haijali viongozi hawajali...tunapoteza maji mengi mno kwa upuuzi tu...Maji ni uhai Maji ni kila kitu, kila tone la maji lina thamani na maana kubwa mno....yaheshimu Maji yatunze
Ok tajaribu kufanya hivyo japo nyingine zipo jukwaa la dini ambapo ni wachache wana access ya kufika huko
Levitating??
Ulieza ku-levitate mkuu???
3: KANUNI YA IMPERMANENCE
Kwamba hakuna kidumucho milele, lakini kwenye hili tuna shida moja kubwa sana, tunavyovipenda tunatamani viwepo milele, tusivyovipenda tunatamani vituondoke mara...! Hii kanuni inayomtesa sana mwanadamu.. Laiti tungekuwa na ufahamu wa kutomiliki milele matatizo mengi sana Africa yasingekuwepo hasa kwenye siasa
4:COMPASSION AND LOVING KINDNESS(HURUMA NA UPENDO)
hili wengi tunalikosea tangu ngazi ya familia mpaka kwenye Jamii, unaonyesha UPENDO kwa mtoto kwa kumpa pesa nyingi za matumizi bila kutafakari atazitumiaje
Unampa teja pesa bila kujua kuwa unaelea tatizo
Unashindwa kukemea uovu kisa tu unaogopa kuonekana mbaya kwenye familia au Jamii au kwakuwa una maslahi na huo uovu
Buddhism inafafanua vifungu vingi kwenye misahafu yetu ambavyo havikufafanuliwa
Infopaedia nipende tu kusema kuwa nashukuru mno uwepo wa JF , sehemu ambapo tunaweza kuongea kwa uhuru na uwazi... Imenichukua zaidi ya miaka mitatu na kujishauri kwingi sana mpaka kuleta hii habari lakini vilevile nikiwa makini kusimulia bila kuharibuIla mwenzangu we una moyo. Mi kuelezea mambo ya kule kwa watanzania nahisi ni mpaka ipite miaka kama 150 hivi ndiyo watanzania wa kizazi hicho wataweza kunielewa kidooogo!. Ila hongera sana.
Dah!! Umenikumbusha mbali sana. Mambo ya Tripitaka: Vinaya, Sutra, na Abhidharma.
Shelizi, se bu yi kong, kong bu yi se,
kong ji shi se, se ji shi kong. Kitu cha 'shin jing' hicho (heart sutra). Hapo unagonga 'muyu' kama huna akili nzuri vile.
Kwenye hiyo picha kama sikosei yule kule mbele ni "mzungu f@la".
Ila wacongo waliharibu sana, mpaka waafrica wote tukaonekana siyo.
Mkuu ulimaliza nyundo tatu???
Pouwa witnessj nimekupenda bure mdada
Hii ishu ya levitation kuna mdau humu aliniita muongo na kwamba chuo chetu ni feki...lakini bado naomba niseme tena sisi hatukujifunza levitation... Buddhism ina sects nyingi kama Mahayana, Vajrayana na Theravada lakini vilevile hata Taoism na Conficious zote zinahusishwa na Buddhism bila kusahau Krishna/kshna consciousness
Naona hapo ume-confuse them (changanya) kila kitu kupata dini yako mwenyewe. Hii dini yako yakuamini kila kitu inaitwaje?