A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?

Jifunze kwanza lugha sahihi:

A Kangaroo Court Moja = One Kangaroo Court​

Je, nacho ni A Kangaroo? = Je, nacho ni Kangaroo Court?​


Halafu Mkuu, unaboa sana baada ya kuteremsha blah blah blah zako, kila mara unapenda ku-refer orodha za nyuzi zako za nyuma kama vile unataka kutudhihirisha wewe ni mtabiri mbobevu na mjuvi sana wa mambo yote chini ya jua. Huu ni usanii.
 
Kama mwendazake hakukuona huyu hangaya utahangaika sana.
 
Mnapompiga mawe paskali mnapaswa kutambua kuwa ni mwanahabari, so ana haki ya kuchambua, kuandika any article anayoweza kuchambua.

Tatizo la baadhi yetu ni kumuangalia mtu jinsi haiba yake na kusahau taranta yake.
Habari za uchochezi ni habari??
 
Baada ya watu kuhumiwa na a kangaroo court na hukumu ya kikangaroo wakaamua kwenda kwenye a proper court, huko nako wanapokutana na Ukangaroo wa legal technicalities, watu kama hawa, haki yao waipate wapi?.
Sisi watu wa kushauri, tulishauri.
Ila nime realize Tanzania hatuna kabisa mawakili makini!.
Ila mahakama zetu nazo...!. Lengo iwe ni kutoa haki, hizo legal technicalities za nini?.
P
 
Kama Mahakama zikitekeleza maamuzi haramu ya ccm kwa Watanzania unaona zimetenda haki ila zikisimamia sheria kwa mujibu wa sheria(Katiba na sheria nyinginezo za nchi na Kimataifa) unaona hazifai,kweli tuna safari ndefu.
 
Kwanini hutaki akina Halima waje CCM?
 
Technicality kwenye sheria si tatizo mkuu zipo enzi na enzi kwa kuzingatia pleadings zilivyo
Mahakama haiwez kuvumilia defective ambazo ni fatal kwa vyovyote vile.
Lakini technicality zisiwe chanzo cha kufanya haki isitendeke
 
Nadhani unahitaji likizo. "You look confused".
 
Technicality kwenye sheria si tatizo mkuu zipo enzi na enzi kwa kuzingatia pleadings zilivyo
Mahakama haiwez kuvumilia defective ambazo ni fatal kwa vyovyote vile.
Lakini technicality zisiwe chanzo cha kufanya haki isitendeke
Mkuu mgunga pori, kwanza asante, kwa kuelewa kitu kinachoitwa legal technicalities kwenye sheria ambacho ni kikwazo kikuu kwenye utoaji haki ndani Mhimili wa mahakama.

Mwaka jana nimeendesha mfululuzo wa makala za "Kilio cha Haki" kwenye TV Programs na Magazeti,
Baadhi ni hizi
Hii Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Na Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?

Na Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Na Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Kusema la ukweli, makala hizi, zilisaidia Sana.

Sasa nimeanza mfululizo mwingine wa makala za "Haki za Kikatiba Zilizoporwa" ambapo mimi navaa viatu vya mtunga katiba na kueleza dhamira ya mtunga katiba wakati akitunga kipengele fulani ambacho baadae kimekuja kufanyiwa marekebisho ambayo yamekwenda kinyume cha dhamira ya mtunga katiba.

Nimeanza na Ibara ya 5 na ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

P
 
Nadhani unahitaji likizo. "You look confused".
Mkuu Stan Mashamba, asante sana kwa ushauri, nitauzingatia, ila namna bora ya kumsaidia mtu ambaye yuko confused, ni kwa kumuonyesha the right thing ili aone tofauti na anachofanya. Hoja iliyopo mezani kwenye bandiko hili ni kuhusu a kangaroo court fulani kutoa maamuzi ya kikangaroo na mamlaka ya rufaa ambayo yenyewe sio a kangaroo, ila inapoyabariki maamuzi batili ya Kikangroo, nayo inageuka a kangaroo court?. Kama aliyeuliza swali hili ni mtu aliye changanyikiwa, nitakushukuru sana kama utaainisha ni maeneo gani au ni hoja gani ni za a confused man?.
P
 
Zee nafiki wewe, kaa lea wajukuu
 

This is well below your God-given ability to put forward a learned arguement. Umeanza kwa kulaumu mawakili wabovu, kisha ukaja kulaumu mahakama kwa legal technicalities.
Bila hizo technicalities justiice haiwezi kuwa served, hujui hilo au unalipuuza mara hii TU kwa kuwa maamuzi ya mahakama sio uliyotarajia??

Akina Mdee walete madai yasiyo na technical issues, ili tuone hizo mahakama unazolaumu zinaamuaje!!
 
Mkuu NewOrder , kiukweli kabisa mimi kuna vitu sielewi kabisa tena vingine ni vya kawaida sana, mfano Siwa, watu kuvaa majoho, misafara, hata Mwenge wa Uhuru niliwahi uulizia Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Mahakamani panategemewa kuwa ni mahali pa haki bin haki, hizo legal technicalities za nini?!.
P
 
Ili ufanye marekebisho kama na kufile upya ili umshitaki mhusika.Sio kushitaki ambao hawapo. Soma kesi ya Lujuna Balonzi vs Board of Trustees of Ccm
Kusema ukweli uzungu, umeiharibu sana fani ya sheria, kuna tatizo gani baraza la udhamini kuitwaa bodi ya udhamini?.
P
 
KANGAROO COURT

Ni kauli ya kisheria na jina lililopewa kwa taasisi yoyote inayofanya kazi ya kusikiliza shauri lolote iwe mahakama ( JUDICIAL) au chombo cha kiutawala kinachosikiliza shauri la mtumishi au mwanachama ( QUASI JUDICIAL) ambayo imesikiliza kienyeji kutoa maamuziki kienyeji bila kufuata misingi ya HAKI MSINGI ( NATURAL JUSTICE)

Chombo chochote kinachosikiliza shauri kinatakiwa kisifanye ile mahakama ya hadharani ambapo kuna washabiki na kutoa hukumu hapo hapo bila kufuata NATURAL JUSTICE maana maamuzi hayo yanaathiri moja kwa moja mtu huyu na hata kama baadaye itakuja kugundulika hakuwa na hatia ile stigima aliyoipata itamsababishia POST TRAUMATIC SRESS DISORDER (PTSD)

Hivyo usiwe una maslahi na shauri unalolisikiliza na kulitolea hukumu, mtuhumiwa asiwe rafiki yako au adui yako, asiwe mwanao au ndugu yako au msiwe na maslahi ya kibiashara ikiwa ni kmpuni moja au mnadaiana ( NEMO JUDEX IN CAUSA SUA) Hayo mambo yanaweza kuathiri maaumuzi yako yasiwe ya haki

Mtuhumiwa anatakiwa kwanza asishtukizwe shutuma dhidi yake, mfano kwenye mkutano wa hadhara unasimamishwa unasomewa tuhuma zako na hukumu kutolewa hapo hapo. Mtuhumiwa anatakiwa apewe notice ya shutuma dhidi yake, apewe muda mzuri wa kuandaa ushahidi na utetezi wake pamoja na vielelezo na ikiwezekana na mashahidi, awe na nafasi ya kuhojiana moja kwa moja na anayemtuhumu kwa kross examination (AUDI ALTERUM PATERM)

Mtuhumiwa baada ya kusikilizwa kwa shauri lake na hukumu ikatolewa dhidi yake ni haki yake ya msingi ya kuelezwa sababu za kufikiwa uamuzi iule dhidi yake ili kuonyesha kuwa haki ilifuatwa na mtoa maamuzi aliongozwa na misingi ya haki bila shinikizo la aina yoyote (NULLUM ALBITRIUM SINE RATIONIBUS)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…