A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?

Wanabodi,
Kunapotokea jambo kubwa kama hili, usually huwa it's not over until it's over, kwa hapa hili lilipofikia, kwa ndani ya Chadema, it's over!.

Paskali.
Hili jambo sasa it's over yake ni keshokutwa siku ya Jumatano
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Nimeisoma hukumu, 1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CCM ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…