Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 55
Katika pita pita ya kanzi mitaa ya uarabuni kalikutana na mazungumzo yafuatayo kwenye Benki moja yenye makao makuu Canada.
Mfanyakazi:"Habari za leo kanzi?"
Ka-nzi: "Nzuri tu habari za hapa Dubai"
Mfanyakazi: "kwema tu, naona mambo ya tanzania siyo mabaya bwana"
Ka-nzi: "Kwanini tena, wenzio tunabangaiza tu"
Mfanyakazi: "Hivi wenzetu mnabiashara gani siku hizi Tanzania?"
Ka-nzi: "Una maana gani?"
Mfanyakazi: "Naona hela nyingi kweli inatoka huko kwenu bwana" akajibu huku anamtazama nzi anavyosafisha mikono yake kwenye mbawa zake kujihakikisha kuwa yeye ni msafi.
Ka-Nzi: "Una maana gani hela nyingi"? kakauliza kwa udadisi.
Mfanyakazi: "Wiki hizi mbili zimepitia hapa fedha karibu dola miliioni 30 hivi kutoka Tanzania"
Ka-nzi: "Zimepita kama maji yanavyopita mtoni yakaenda zake au zimepita zikatuwama?" kakagangamala kuuliza.
Mfanyakazi: "Zimepita kama maji mtoni, zimeingie na baada ya muda zikatoweka kwenda akaunti mbalimbali na hii si mara ya kwanza"
Ka-nzi: "Wanajulikana waliopitisha au ni mizimu ya watu wa kale?"
Mfanyakazi: "Wanajulikana sana tu, wanakuja hapa mara kwa mara na kutumia watu wao hapa"
Ka-Nzi: "Ni kina nani hao?" Ka nzi kakauliza. Jamaa hakutoa jibu. Akanyanyuka kupekua kabati lake la kisasa lililoupande wa kushoto wa kiti chake. Dirisha la ofisi yake liliangalia upande wa barabara maarufu ya Sheikh Zayed. Alirudi na makaratasi kadhaa hivi ambayo yamshikanishwa pamoja kwa pini. Akayaweka mezani.
Ka-nzi: "ni watu ambao naweza kuwajua ukiwataja?" aliuliza.
Mfanyakazi:"theluthi mbili unawajua kwani mnao huko huko" alikuwa anaangalia yale makaratasi huku akitingisha kichwa. Alipomaliza akarudia tena "ndiyo karibu asilimia 75 ni watu wenu huko huko". Aliyaweka mezani. Akamuangalia nzi machoni. Kwa haya nzi akapepesa macho yake kwingine.
Mfanyakazi akachukua simu yake na kubonyeza namba fulani na mara baada ya upande wa pili kujibu akazungumza maneno kadhaa kwa lugha ya Kiarabu, na baada ya kumaliza akamgeukia kanzi.
Mfanyakazi: "natoka mara moja nisubiri hapa, nitarudi kama dakika kumi hivi". Akanyanyuka kwa ghafla akiyaacha yale makaratasi mezani. Akafunga mlango nyuma yake na kumuacha kanzi mle ndani. Kuna dirisha kubwa la kioo kwenye ofisi ya "mfanyakazi" lakini likiwa limewekwa vioo vyeusi vinavyozuia walio nje kuona waliyomo ndani, lakini wa ndani kuweza kuona kinachoaendelea.
Ka nzi kakaa pale. Kakabakia kujiuliza swali. "Ni kina nani hao".
* * *
Baada ya dakika kumi, mfanyakazi alirudi.
"Samahani, kulikuwa na jambo nashughulikia." Alisema na kuyaangalia makaratasii yake aliyokuwa ameyaacha mezani.
"hamna neno, miye ni mtu wa subira" alisema ka nzi.
"Aisee natumaini hukuchungulia haya makaratasi maana wakijue nimefungwa." aliyakusanya haraka na kuyarudisha kwenye kabati lake na kutia "komeo".
Ka nzi: "usiwe na wasiwasi mkuu". Hakukanusha.
"Kama nilivyokuambia, kuna mzungunguko wa ajabu sana wa fedha za kigeni kutoka Tanzania, ni mamilioni ya dola na watu ni karibu wale wale tu". alisema mfanyakazi.
"Sidhani kama watu wengi wanajua hilo" kanzi kalikiri.
"Wengi wanafikiri ni biashara tu, Dubai hapa ndiyo Uswisi, watu wanahamisha na kufunga maakaunti yao Geneva wanakuja hapa, ndiyo kitovu siiku hizi cha offshore banking na wanauhusiano wa karibu sana na Costa Rica, Cayman Islands n.k" alisema mfanyakazi na kama aliyebadili mawazo akakoma hapo hapo.
"Well, tuyaache hayo, habari za familia lakini" aliuliza.
Ka nzi: "Ni nzuri tu, ila magonjwa magonjwa tu kila kukicha"
Wakaendelea kuzungumza mambo ya familia zao huku wakikumbushana maisha yao ya ujana kabla "mfanyakazi" hajapata nafasi ya kwenda Dubai kikazi akitokea Canada. Urafiki wao umekuwa wa muda mrefu na wa pekee, mmoja akiwa ni Mtanzania mwenye asili ya Uhindi na mwingine ana asili ya Uarabuni. Walisoma pamoja shule ya Popatlal Tanga. Walisoma miaka ile ya sabini chini ya mwalimu mkuu mashuhuri Chaudry.
Walipomaliza kukumbushana walikubaliana kuonana nyumbani kwa "mfanyakazi" kwa maakuli ya jioni kwani ka"nzi" alikuwa aendelee na msafara wake maeneo ya Oman katika biashgara zake za "njugu na korosho".
Kanzi aliondoka akisindikizwa hadi kwenye lift na 'mfanyakazi'. Waliachana kwa kutakiana heri.
Alipoingia kwenye lift, ka nzi alishika mfuko wake wa nyuma. Alikuwa amekunja nakala za "makaratasi". Alijisemea moyoni "namna hii tumekwisha!". Kichwa kilikuwa kinamzunguka. Alipofika hotelini tu, hakuchelewa alichukua simu yake na kubonyeza makao makuu ya ANTI-UFISADISM INTERNATIONAL HQ".
Sauti iliyopokea upande wa pili ilikuwa ni ya kike, nyororo na yenye mvuto wote wa haiba na yenye kuweza kufamfanya simba acheze sindimba na nyoka acheze "mugongo mugoongo".
Kanzi: "Mwanakijiji please!"....
The END...
Hadithi yako nzuri!