A lister anaweza kufikiria mtu aliyekwisha kula na kusaza, sasa ana muda wa kuangalia cable na kununua magazeti ya udaku, katika nchi yenye watu wa aina hiyo wa kutosha kufanya kuwepo a sustainable economy ya hawa manyigu malkia.
Huko kwetu watu mvua hazijanya wanafikiri mihogo itapatikanaje wapate kuchemsha japo na chumvi tu we unataka kuleta habari za A list.
Ndiyo maana watu wanakwambia anaweza kuja Beckham watu wasimjue wala nini, akaonekana mzungu tu sanasana ombaomba watamzonga tu bila kumjua.
Na hata hao watoto wa IST na Masaki wawili watatu watakaomuomba autograph watafanya hivyo kizushi tu, nani ana keep autograph bongo?
Wewe umeona AY watu wametaka kumtwanga huko, naye star waliyelipa hela kumuona.
Watu wana njaa na hasira.