kisa kilianza zaidi ya miaka 10 iliyopita, wawili hawa walikuwa wapenzi wakazaa mtoto lakini kutokana na 'external forces' hawakuoana. maisha yakaendelea kila mmoja akashika njia yake na sasa kila mmmoja ameoa/kuolewa na ana watoto wawili katika ndoa yake . lakini hawa watu wana kitu kimoja kinachofanana katika ndoa zao 'matatizo'. katika birthday party ya mtoto wao walijikuta wanakaa pamoja na kila mmoja akagundua kuwa mwenzie ana kitu kinamsumbua walipoamua kuambiana ukweli wakagundua wote wana matatizo makubwa katika ndoa zao.. mambo hayaendi sawa magomvi yasiyoisha, kutokuaminiana, kununiana na hata kufukuzana, kusuluishwa kila mara na hivyo ndoa zao hazina ladha. hapo ndipo mwanamume kwa ujasiri akatoa kauli " look baby.. am here... am a shoulder you can cry on... if you you need someone to talk to I will always be there for you!' maneno hayo yameibua hisia kali za mapenzi kati yao na wameanza kuwasiliana kwa kasi ya ajabu. huyu dada anasema amefika mahali anahisi uzalendo utamshinda na anaweza kujikuta wanarudiana na mpenzi wa zamani na mzazi mwenzie. ananiomba ushauri aamue vipi? mimi kabla ya kumpa jibu nimeona nililete hapa ili mnipe ushauri ili kupitia michango yenu niweze kumshauri vema.