Hapa sina uhakika, kwa kweli nakubali ustaraabu mnatuweza tena wa asilimia kubwa. Lakini inafaa ifahamike kuwa kenya ilitawaliwa na mkoloni aliyekua mkorofi na aliwapiga sana babu zetu huku akiwaamrisha wa kila kitu.
Ndo maanake kiswahili chetu huwa kimejaa amri na vitisho. Mateso hayo yalichangia sana. Fanya utafiti sana Waafrika waliocharazwa na mzungu jinsi walivyo hata Marekani wale weusi huko.
Ila Wabongo pamoja na ustarabu huo wenyu wapo walio na roho mbovu na wamejificha humo ndani ya ustaraabu huo. Kiasi kwamba huwezi jua mtu hisia zake kamili ndio zipi.
Nikiwa Bongo muda fulani niliwaona wanachimbana kikazi na kibiashara na unyangau hata kuliko wa kikenya lakini walifanyiana hayo yote huku wakitabasamiana na kuongea kwa ustaarabu. Halafu matapeli wapo unakuta jamaa Mtz anakutapeli akitumia ustaraabu yaani unaposhtuka huamini kwamba mtu aliyekua anaongea kwa heshima na ustaraabu hivyo anaweza kuwa tapeli.
Kuna mmoja kanitapeli na hadi sasa huwa naomba sana nikutane naye sio kwa ajili anirejeshee alichonitapeli lakini nimuangalie kwa macho na kuamini kweli jamaa kanitapeli na jinsi alvyokua anaongea kwa heshima na tena sana.