A true sad story: Taarifa fupi ya Wastara na mumewe SAJUKI

Leornado

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
1,529
Reaction score
198
A George Iron mini documentary, 2012

TRUE SAD STORY

ILIKUWA siku ya furaha…kwanza kukutana na familia yako maeneo ya Tabata…pili kuisikiliza historia yako na mke wako Wastara ilivyokuwa ya kustaajabisha.
Katika mahojiano Wastara alijizuia asitokwe machozi lakini ilishindikana alilia sana na hadi wakati huo hakuamini kama umemuoa akiwa hana mguu mmoja. Ni maajabu sana.
ILIKUWA HIVI. Wastara aligoma katakata kuwa hapandi pikipiki kamwe, ukamlazimisha alipogoma ukamuuliza.
“Unanipenda” akajibu ndio.
“Unaniamini” akajibu ndio.
“Basi utapanda pikipiki kama unaniamini”
Wastara akapanda…..kilichotokea mbele ni ajali mbaya, wewe haukuumia lakini Wastara akaupoteza mguu wake baada ya hospitali kushauri kuwa ukatwe maana hauwezi kuunganika.

Wakati Wastara anakatwa mguu, kidume ukaamua kutafuta mahari, ukamtolea….hata akiwa hajapona vizuri UKATANGAZA ndoa, na mwanamke asiyekuwa na mguu..tena akiwa bado ana kidonda kikubwa. WEWE NI WA AJABU SANA.
Ilifikia kipindi cha kucheka hasahasa ulipokuwa unacheza na Wastara….mchezo wa kumnyang’anya mguu wake wa bandia na kukimbia nao naye anakukimbiza. Ilikuwa inashangaza.
Baada ya mastori mengi ya kusisimua, Wastara akatukaribisha pilau la nguvu……amakweli anajua kukarimu wageni.
Baada ya kushiba sasa tukaungana kupiga picha hii ya ukumbusho,
Waliosimama nyuma: Wastara, Yvonne cherry Monalisa, George Iron mosenya.
Mbele: Sonia, Hayati SAJUKI, na Suzan Lewis NatashA

​
773_534844959868358_1196606602_n.jpg

**Sipendi kukusifia sana angali u marehemu sasa…lakini ulikuwa mchangamfu na upendo wako wa ajabu kwa Wastara….wanao wanaume wachache sana duniani..kumuoa mtu aliyekuwa mzima kabisa kisha akakatika mguu???? Ni ngumu sana.​
umeondoka na PENZI la maajabu, PENZI la kusadikika

**MUNGU akulaze mahali unapostahili JUMA KILOWOKO...SAJUKI…Amen.

SHARE kwa marafiki zako kama imekugusa

Kwa kweli chunguzeni lugha zenu msije kufuru au kunyanyapaa watu wengine.Kuoa aliyekatika mguu nayo ni sifa jamani?Je walemavu ambao nao ni wana-jf wanajisikiaje kwa kauli hizi?.Walemavu hawapendeki au?
 
chunguzeni lugha zenu msije kufuru au kunyanyapaa watu wengine.Kuoa aliyekatika mguu nayo ni sifa jamani?Je walemavu ambao nao ni wana-jf wanajisikiaje?

Stori inagusa sana. Mtoa mada alikuwa na lengo zuri lakini akajisahau kidogo tu kuwa ulemavu si kosa kiasi kwamba mtu akiolewa na ulemavu basi inakuwa "bahati".

Yawezekana marehemu alimuoa kama "fadhila" kwa kuwa alimsabibishia ulemavu au kwa mapenzi ya kweli hatuezi jua

Mungu amrehemu na ampe ujasiri mkewe..
 
Kwani nini mna-doubt penzi la marehemu kwa Wastara kuwa huenda alimuonea huruma?Hakuwahi kusema hivyo kabla hajafa.Mbona hamzungumziii Wastara alichofanya wakati Sajuki akiwa mgonjwa ambapo wapo wanawake wengi wangeweza kumtelekeza.
 
Huyo Sajuki namsikia tu ni yupi hapo pichani maana Nimemuona Natsha na Monalisa ndio ninaowafahamu kwa pichani...
 
Ndio tuseme hujui kusoma ulikuwa unasubiri picha tu?hatukuambii soma tena thread!
 
Mungu ailaze mahali pema peponi roho yamarehemu. Pia awape nguvu nafaraja wafiwa wote.
 
Ndio tuseme hujui kusoma ulikuwa unasubiri picha tu?hatukuambii soma tena thread!

Ah Mwanzoni nilitizama picha tu kwani huyu jamaa nimekuwa nikimsikia tu tokea pale alipokuwa anaumwa akavuma sana na sikufuatilia hata kidogo. Sasa baada ya kutuma huu uzi nikaupitia tena ndio nikaona maelezo ya Picha sikuona haja ya ku edit Mkuu nimeipotezea tu... Sawa!
 
Eti jamaa alipigwa juju baada ya kupora kifaa(wastara) cha mdau watanga ndo mabalaa yote hayo yakaanza.
 
kweli sie viumbe tuliumbwa na Mwenyezi Mungu hatukosagi ya kusema.? kha!
 
Stori inagusa sana. Mtoa mada alikuwa na lengo zuri lakini akajisahau kidogo tu kuwa ulemavu si kosa kiasi kwamba mtu akiolewa na ulemavu basi inakuwa "bahati".

Yawezekana marehemu alimuoa kama "fadhila" kwa kuwa alimsabibishia ulemavu au kwa mapenzi ya kweli hatuezi jua

Mungu amrehemu na ampe ujasiri mkewe..
Sometimes una point sana Asprin actually nakuunga mkono umeongea kweli,mwandishi hakuwa na maana mbaya alitaka tu ujumbe ufike,ila nina amini kabisa 100% Sajuki hakumwoa Wastara kama fadhila ila ni kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Wastara.
 
A George Iron mini documentary, 2012

TRUE SAD STORY

ILIKUWA siku ya furaha…kwanza kukutana na familia yako maeneo ya Tabata…pili kuisikiliza historia yako na mke wako Wastara ilivyokuwa ya kustaajabisha.
Katika mahojiano Wastara alijizuia asitokwe machozi lakini ilishindikana alilia sana na hadi wakati huo hakuamini kama umemuoa akiwa hana mguu mmoja. Ni maajabu sana.
ILIKUWA HIVI. Wastara aligoma katakata kuwa hapandi pikipiki kamwe, ukamlazimisha alipogoma ukamuuliza.
"Unanipenda" akajibu ndio.
"Unaniamini" akajibu ndio.
"Basi utapanda pikipiki kama unaniamini"
Wastara akapanda…..kilichotokea mbele ni ajali mbaya, wewe haukuumia lakini Wastara akaupoteza mguu wake baada ya hospitali kushauri kuwa ukatwe maana hauwezi kuunganika.

Wakati Wastara anakatwa mguu, kidume ukaamua kutafuta mahari, ukamtolea….hata akiwa hajapona vizuri UKATANGAZA ndoa, na mwanamke asiyekuwa na mguu..tena akiwa bado ana kidonda kikubwa. WEWE NI WA AJABU SANA.
Ilifikia kipindi cha kucheka hasahasa ulipokuwa unacheza na Wastara….mchezo wa kumnyang'anya mguu wake wa bandia na kukimbia nao naye anakukimbiza. Ilikuwa inashangaza.
Baada ya mastori mengi ya kusisimua, Wastara akatukaribisha pilau la nguvu……amakweli anajua kukarimu wageni.
Baada ya kushiba sasa tukaungana kupiga picha hii ya ukumbusho,
Waliosimama nyuma: Wastara, Yvonne cherry Monalisa, George Iron mosenya.
Mbele: Sonia, Hayati SAJUKI, na Suzan Lewis NatashA

​
773_534844959868358_1196606602_n.jpg

**Sipendi kukusifia sana angali u marehemu sasa…lakini ulikuwa mchangamfu na upendo wako wa ajabu kwa Wastara….wanao wanaume wachache sana duniani..kumuoa mtu aliyekuwa mzima kabisa kisha akakatika mguu???? Ni ngumu sana.​
umeondoka na PENZI la maajabu, PENZI la kusadikika

**MUNGU akulaze mahali unapostahili JUMA KILOWOKO...SAJUKI…Amen.

SHARE kwa marafiki zako kama imekugusa

Actuaaly imenigusa sana na kamwe sintoacha kustaajabu kwa aina ya mapenzi waliyooonyeshana watu hawa hasa kwa ulimwengu wetu wa sasa na umaarufu waliokuwa nao na uzuri aliokuwa nao Sajuki na uzuri alionao Wastara mpaka sasa.Hivyo havikurudisha nyuma mapenzi yao walipendana mpaka basi, nilidhani mapenzi hayo yalikuwepo zamani tu lakini watu hawa wamenionyesha kuwa bado wapo watu wanaoweza kupendana sana na kiukweli ktk ulimwengu wetu wa sasa.Naumia sana kila nifikiriapo Wastara ana hali gani kwa sasa,kutoka moyoni mwangu nampenda sana huyu dada na namuombea Mungu amzidishie na kumpa nguvu za kuvumilia kumkosa mpenzi wake wa maisha Sajuki.
 
Sometimes una point sana Asprin actually nakuunga mkono umeongea kweli,mwandishi hakuwa na maana mbaya alitaka tu ujumbe ufike,ila nina amini kabisa 100% Sajuki hakumwoa Wastara kama fadhila ila ni kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Wastara.
Afu we mtoto uwe na adabu kwa wazee, ina maana kuna wakati huwa namwaga mapumba badala ya mapwenti?:becky::becky:
 
Hasira hasara jamani cheki sasa mpaka unakosea badala ya mapoint unasema mapwenti au ndo inavyotakiwa siku hizi?.Nisamehe mwayego.
 
Hapo unaona umemwaga mapweeeenti. Nyie vizazi vya ving'amuzi mna taabu kweykwey....
 
Back
Top Bottom