Aache kazi aliyonayo ili akafungue duka la rejareja kwa Tsh. milioni 5...

Aache kazi aliyonayo ili akafungue duka la rejareja kwa Tsh. milioni 5...

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
712
Reaction score
1,748
Habari za muda huu, kuna jamaa yangu ni masonry yaani fundi uashi. Amejikusanya kwa muda mrefu amefanikiwa kukusanya kiasi cha pesa shilingi 5m, amepanga kufungua biashara ya duka la rejareja ili aachane na hii kazi ya masonry uashi ili aweze kuisimamia biashara yake mwenyewe.

Je, hii biashara ya duka kwa makisio kwa siku inaweza ikamuingizia faida ya Tsh. 30k au zaidi kama anavyosema? Ambayo ndicho kiasi anachokiingiza kwa siku kwenye hii kazi yake ya uashi au zaidi kutokana na mapatano ya kazi sababu ya yeye kuachana na hii kazi anasema ni kazi ngumu yaani mpaka utoke jasho na kuchafuka na cement ndio uingize kipato.

Anasema ni kazi ngumu

1622536371826.png

Asiache kazi ya ufundi ni bora akafanya zote, si kila siku ataenda kujenga siku asizoenda kujenga asimamie duka, labda aseme kuwa nguvu za kubeba tofari zimeisha.
 
Amefanya reaearch juu ya biashara ya duka?

Ana uzoefu wa biashara?

Tunasubiri mrejesho wa kilio cha kusaga meno
 
Ushauri kwenye biashara, unapo fungua biashara inayohitaji mtaji 5m, atleast uwe na hela mara mbili ya hio 5m,

Biashara zina mambo mengi sana na huwezi piga mahesabu yakaja hivyo hivyo hasa kwa yeye ambaye ni mgeni,
 
Kupigia mahesabu ya faida kwa siku wakati hata biashara yenyewe hujaanza ni ngumu sana, Biashara ina mambo mengi mzunguko wa biashara kwa siku ndio utakaokupa kiasi cha faida.
 
Ushauri kwenye biashara, unapo fungua biashara inayohitaji mtaji 5m, atleast uwe na hela mara mbili ya hio 5m,

Biashara zina mambo mengi sana na huwezi piga mahesabu yakaja hivyo hivyo hasa kwa yeye ambaye ni mgeni,
Ushauri nzuri ila kwa hali zetu hizi hapo unaona hiyo 5M kamenyeka mtu anajipinda kutafuta 1M aanzishe Biashara ya 1M
 
Ushauri nzuri ila kwa hali zetu hizi hapo unaona hiyo 5M kamenyeka mtu anajipinda kutafuta 1M aanzishe Biashara ya 1M
Unless wewe tayari Una uzoefu na biashara husika, otherwise kama unaanza Una asilimia chache sana za kutoboa.
 
Back
Top Bottom