Aachiwe Mbowe peke yake?

Inapendeza Sana mtu mwenye akili akisimamia uhalisia
 
Siyo kwa Mahakama hii ambayo Jaji mchongo anahalalisha hukumu ambayo tayari imeshaandikwa na mawakili wa Serikali.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 

..hivi kutokuonekana kwa Lijenje huwezi kukulinganisha na kutokuonekana kwa Lugakingira ktk kesi ya uhaini ya miaka ya 80?

..Na Murtaza Lakha si alikuwa wakili wa utetezi ktk kesi hiyo?

..Sasa kwanini hakuwasilisha hiyo habeas corpus ktk kesi ile? Kwanini alishindwa kuibananisha jamhuri mpaka kesi uondolewe?

..Hatuwezi kuhukumu umahiri wa mawakili wa utetezi au hata wa jamhuri wakati kesi bado inaendelea.

..Hata kesi ya uhaini ya miaka ya 80 tungetoa maksi wakati kesi inaendelea badala ya kusubiri mpaka mwisho wa kesi huenda tungewapa maksi ndogo sana mawakili wa jamhuri / waendesha mashtaka.

..umahiri wa upande wa jamhuri ktk kesi ya uhaini ya 1980s ulionekana wakati wa majumuisho / closing argument. Kwa maoni yangu walishinda kesi ile dakika za mwisho kwenye majumuisho.

Cc Nguruvi3
 
Hivi kuna mahali Jamhuri imekiri kumshikilia Lijenje? Kama haijakiri, utetezi watathibitisha vipi kuwa alikamatwa ikiwa juhudi zao za kuonyesha kuwa wakina Adamoo waliteswa ( mpaka kuonyesha makovu), kuwa hawakuwahi kuwa central zote zimetupiliwa mbali na Mheshimiwa Jaji? Kwa namna hiyo watailazimishaje jamhuri kutoa mtu ambae wanasema walimtafuta na hawakumpata?
Mawakili wa utetezi wanajitahidi katika mazingira magumu ambapo kuna shaka kuhusu neutrality ya refa. Wakina Lakha walitetea wateja yao mbele ya Mahakama ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa inalinda uhuru wake kwa wivu mkubwa. Hapa ni kungoja tu watu wafungwe.

Amandla..
cc. JokaKuu
 
Pascal Mayalla anasahau mambo mengi katika kesi hii ya Mbowe tofauti na ya uhaini
Kwa waliofuatilia kesi ya uhani 80's Majaji walikuwa 'wima' katika kufuata sheria

Hii ya sasa Jaji anautaka upande wa mashtaka ukafanyie marekebisho baadhi ya vifungu
Jaji anakataa ushahidi na kutoa ''maoni yake' badala ya sheria

Katika mazingira ya kawaida huenda hata mawakili wa utetezi wangejitoa . Kuwalumu????
 
Umeandika ukweli,pale Kuna vimbwanga, meza inapinduliwa waziwazi ,watu wanahapia vitabu vitakatifu wakijua wakifanyacho sio kweli, Binadam tunampa KAZI ngum Sana Mungu,japo tunasema ni mwingi wa rehema ,ila achezewi hovyohovyo, binadam wote ni sawa Mbele zake, machozi ya mateso KWa watu wake wasiokua na hatia ,hayatawaacha salama,ndivyo ilivyo na ilishakua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…