Abahaya n'Empaya

Abahaya n'Empaya

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,174
Reaction score
16,794
TUJIFUNZE KIHAYA SANIFU KATIKA MUKTADHA WA WAZIBA:

1. USISEME: Mjwahuzi yagya aruwanja rwe ndege.
SEMA: Mjwahuzi yagya aituriro lye ebiarazi.

2. USISEME: Ompe omwanvuli.
SEMA: Ompe ekiziba izoba.

3. Husiseme: Ntugya akikao
Sema: Ntugya alukiko.

4. USISEME: Ntulya omuchele
SEMA: Ntulya ekibuzamagezi.

5. Usiseme: Ompe amabati.
SEMA: Ompe ekishwekanju.

6. USISEME: Ningya akanisa
SEMA: Ningya anteko.

7. USISEME: Tukutane mjini.
Sema: Tushangane akatare.

8. USISEME: Yesu akatufela amushalaba
Sema: Yesu akatufela antelano.

9. USISEME: Ompe ekyoo.
SEMA: Ompe ekilebano.

10. USISEME: Olimpumbavu
Sema: Olimlolwa.

11. USISEME: Olimjinga.
SEMA: Olimfela.

12. USISEME: Ayombekile egorofa
Sema: Ayombekile enjwetwekana.

13 USISEME: Yagya sokoni.
SEMA: Yagya amujajalo.

14. Usiseme: Ninyanga shetani.
Sema: Ninyanga omubisha.

15. USISEME: Aina obukoma.
Sema: Aina ebibembe.

16. Usiseme: Aina Korona.
Sema: Aina endwaramuyaga.

17. USISEME: Ompe ekibiriti.
Sema: Ompe ekiletamuriro.

18. USISEME: Ningonza obushauri
Sema:Ningoza kukwejunizao.

19. Usiseme: Yagura emotoka.
SEMA: Yagura ekigendeza gana.

20. HUSISEME: Yagula ebaiskeli.
SEMA: Yagura ekiselela.
21. Usiseme: Karibu tulye omuchele.
SEMA: Onyegere tulye ekibuzamagezi.

22. USISEME: ondetele ekibatari.
Sema: Ondetele akatadoba.

23. USISEME: omusehemu ze siri.
SEMA: omunzalabantu.

24. USISEME: Ompe olukaratasi.
SEMA: Ompe olupapuro.

25. USISEME agizile engoma.
Sema: Aguzile enyetabantu.

26. Usiseme: Aguzike ekijiko.
SEMA: Aguzile ekiliso.
27. USISEME : Anyiamile akitanda.
SEMA: Anyiamile amushago.

21. USISEME: Ataileo obumeme.
Sema: Ataileo omwako.

22. USISEME: Aguzile ekalukuleta.
SEMA: Aguzile ekyanguyamashabu.

24. USISEME: Ompe erimoti.
Sema: Ompe ekilaguzi.

25. Usiseme: Aguzile eshera
Sema: Aguzile elavari.

26. USISEME: Azaile zeruzeru.
SEMA: Azaire ekinyamagoye.

27. USISEME: Ntukukaribisha muno.
SEMA: Nitukunyegeza na kanyeto.

28. USISEME: Aguzile ebilatwa.
Sema: Aguzile enkaito.

29. USISEME: Aguzile emiwani.
SEMA: Aguzile ekilebero.

30. USISEME: Ompe esanturi.
SEMA: Ompe esahani ze ekyegunde.

31. USISEME: Yesu akakuba empunda.
SEMA: Yesu akakuba endogoobe.

32. USISEME: Otamsiga buchafu.
SEMA: Otamsiga nziro.

33. Kama ni rafiki wa kawaida, sema NINKWENDA lakini kama ni urafiki inaohusisha mapenzi sema NINKUGONZA.

34. Kama unamtaja Mungu kama muumba sema, KATONDA(ELOHIM) lakini kama utamtaja Mungu kama kiongozi sema MKAMA(YEHOVAH).

35. Yesu kwa Kihaya ni MULOKOZI/MUJINI. Nasema hivyo kwasababu Yesu ni neno linalotokana na YOSHUA ikimaanisha MWOKOZI.

36. USISEME: Ninduga kuhemea
SEMA: Ninduga kushaka.

37. USISEME : Ningya abaa
SEMA: Ningyo omunju akigata.

38. USISEME: Ningya a choo.
SEMA: Ningya amushalani.

39. Neno MUKAZI WANGE linatumika kwa mke yeyote yule aliyeolewa lakini unapotaka kumaanisha mke kwa ukaribu zaidi umpendaye unasema MUKYARA.

TUJIFUNZE JUU YA MANENO YA KIHAYA AMBAYO TUMEKOPA KUTOKA KATIKA LUGHA ZA KIGENI.

Kabla hatujaangalia kwa upana juu ya hili eneo ambalo ni nyeti, ningependa kuwakumbusha kuwa WAHAYA wako katika kundi la WABANTU. Kati ya Lugha zinazonishangza kutokana na muundo wake ni LUGHA YA KIHAYA. Sidhani kama kuna LUGHA ya KIENYEJI katika nchi ya Tanzania na barani Afrika kwa ujumla yenye mchanganyiko wa maneno ya lugha za Kizungu kama Kihaya.

A. MANENO YA KIHAYA YALIYOTOKANA NA KIFARANSA.

1. DEMANCHE (Matamshi yake ni
"DIMASHI," ambapo katika lugha ya Kihaya neno hili utamkwa kama "EILIMANSI." Maana ya neno hili katika muktadha wa lugha ya kifaransa ni " SIKU YA BWANA au JUMAPILI kwa kufuata Kalenda ya Papa Gregory 111 ambayo tunatumia mpaka leo.

B. MANENO YA KIHAYA YALIYOTOKANA NA LUGHA YA KILATINI.

Wakati nikiwa mdogo katika maisha yangu ya kawaida huko Bukoba, Ruzinga.Nilikuwa nikisia matamshi/ tungo katika lugha ya Kihaya kama,

"MATHONE YAGYA AKELEZIA," (MATHONE ni kijina, YAGYA ni kitendo na "AKELEZIA" ni kijina ambacho kimetoka katika lugha ya KIRUMI. Neno linatokana na neno la Kigiriki, " ἐκκλησία (ECCLESIA/ ikimaanisha" KUSANYIKO au KANISA. Neno hili lilikuwa likitumika sana kwa watu wa Ruzinga ambao uabudu hapo KYAIBONA (Abaroma) ingawa neno hili pia linapaswa kutumiwa na makanisa yote kutokana na umaana wake.

C. LUGHA YA KIHAYA YANAYOTOKANA NA LUGHA YA KIINGEREZA.

Mifano:
1. Neno " ESOSAITI limetokana na neno la Kiingereza , " SOCIETY" na kwa Kiingereza utamkwa kama, "SOSAYATI."
Neno hili linamaanisha "JUMUIA" au "Vyama vya ushirika." Kimatuzi, neno hili lilimaanisha maeneo ambayo wahaya waliuzia kahawa zao baada ya mavuno. Kwakuwa lilikuwa neno geni uhayani wao walitamka neno hili kama "ESOSAITI."

2. Kuna neno ambalo nililisikia kwa babu yangu mara nyingi akitamka kila mara baada ya kuuza kahawa. Neno hilo ni"KUKWATA ELIASI." Neno,"KUKWATA ELIASI" nimekuwa nikilisikia kwa miaka mingi katika utoto wangu. Sasa baada ya kuwa mtu mzima na kusoma miaka ya hivi karibuni ndipo neno " KUKWATA ELIASI" lilianza kuzunguka kichwani mwangu.

Nilianza kutafakari upya juu ya hili neno na kuanza kujiuliza kama ni la Kihaya au ni neno la lugha nyingine. Nimekuwa nikifanya sana utafiti kwa muda mrefu bila majibu. Kusema ukweli sikuweza kujua hata linaandikwa je. Nilitambua neno hili kwa sauti tu.

Namshukuru sana Mungu siku ya leo asubuhi nikiwa naangalia TV nilisikia hili neno katika hotuba ya Raisi wa Kenya alipokuwa akiongelea juu ya malimbikizo ya malipo ya pesa ya wakulima. Nilisikia akitumia neno " ARREARS(Matamshi yake ni ELIAZI)."

Alipotamka hili neno, sauti yake ilifanana neno, "ELIASI." Mara moja nilienda kwenye kamusi ya kiingereza na nikakuta likimaanisha, " MALIMBIKIZO." Hapo ndipo niliweza kujua maana ya neno,"KUKWATA ELIASI." Kumbe neno "ELIASI" ni neno la kizungu kutoka katika neno "ARREARS"
(Malimbikizo).

Kwa maana hiyo Wahaya walitumia neno hilo kuonyesha malimbikizo ya pesa ya kahawa ambayo yalikuwa hayajalipwa kwao na vyama vya wakulima.

3. Angalia neno, "EMOTOKA" ni neno linalotokana na neno la kizungu, "MOTOR CAR" ila kwa kuwa motor-car siyo asili yetu, wahaya wa kwanza walipoona gari wakaliita, " EMOTOKA.

NB: Haya ni maoni yangu tu. je wewe una maoni gani juu ya muundo wa lugha ya Kihaya inayoongewa katika eneo la Kizinba?
Katika somo lijalo tutaangazia juu ya maneno ya lugha ya Kihaya ambayo yanaundwa kwa kutumia VOKALI mwanzoni na mwishoni mwa maneno yaliyokosa maana katika lugha ya Kihaya.
Waitu Mukama abalinde!


By Askofu Edwin Rweyemamu Mihigo.

NB: nimekopi na kupost, tittle nimeandika mwenyewe
 
Ehhh kina bhashaija muko wapi nimeshafika nilikuja Kwa usafiri wa kandege.....na kubebwa na range sport hata hivyo wameniudhi hii ni gari ya kijana wangu wa mwisho Dk.Mugabuso.....infact .................,
 
Back
Top Bottom