Abbas Kleist Sykes (1929 -) na Bilal Rehani Waikela wanasiasa waliobakia walioshuhudia kuasisiwa kwa tanu 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1567884197488.png

Balozi Abbas Kleist Sykes juma hili tarehe 4 September amefikisha umri wa miaka 90.

Kwa kipimo chochote kile ni kuwa Allah kamjaalia umri mrefu na tunamuombea maisha marefu na afya njema.

Katika kujua kwangu naamini kuna watu wawili tu ambao kwa sasa ndiyo waliobakia katika waasisi wa TANU ambao waliona yote katika historia ya TANU kuanzia mwanzo wake hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961 na wakamjua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa karibu sana katika miaka ile ya kupigania uhuru.

Watu hawa ni Bilali Rehani Waikela na Abbas Kleist Sykes na wote hawa waliwajua vizuri sana wazee wangu. Abbas Sykes na kaka zake Abdulwahid na Ally na baba yangu Said Salum walikulia mtaa mmoja Kipata Street nyumba zao zikiangaliana.

Mtaa huu sasa unajulikana kama Kleist Sykes Street.

Mzee Waikela alifungwa pamoja na babu yangu Salum Abdallah Iyui Prison, Tabora kufuatia maasi ya wanajeshi mwaka wa 1964.

Baada ya majeshi ya Waingereza kumaliza maasi yale viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi walikamatwa na kuwekwa ndani pamoja na wale wote waliodhaniwa ni wapinzani wa serikali.

Babu yangu alikuwa Rais wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) chama aliachoasisi mwaka wa 1955 mwaka mmoja baada ya yeye kuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tabora.

TRAU ilitokea kuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru ikipambana na serikali ya kikoloni bega kwa bega na TANU.

Mwaka wa 1960 TRAU chini ya uongozi wa babu yangu na Kassanga Tumbo iliendesha mgomo uliodumu siku 82 ukivunja rekodi ya mgomo wa Kenya wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh.

Babu yangu alipingana na Mwalimu Nyerere kwenye suala la kuvunja vyama vya wafanyakazi huru na kuwa na chama kimoja cha wafanyakazi nchi nzima chini ya TANU.

Babu yangu alimpinga Nyerere katika hili na kwa nia njema katika mkutano ulifanyika Moshi, kwa kumwambia yeye aendeshe serikali aviache vyama vya wafanyakazi vibaki huru kumrekebisha pale atakapokosea.

Mwalimu inaelekea hakupendezewa na maneno yale.

Hilo ndilo kilikuwa kosa la babu yangu ingawa propaganda zilizoenezwa wakati yeye akiwa jela ni kuwa alikuwa kwenye njama pamoja na wanajeshi walioasi ya kupindua serikali.

Katika vitu vilivyomuumiza nafsi yake ni pale yeye na wafungwa wenzie walipoambiwa waombe radhi kama sharti la kutolewa gerezani.

Babu yangu aliumia kwa sababu walikuwa wamesingiziwa uongo mkubwa sana.

Aliyekwenda jela kuwapa taarifa hii alikuwa Regional Commissioner wa Tabora Rashid Kheri Baghdelleh, rafiki ya baba yangu akimjua sana babu yangu.

Msomaji ingiza mwenyewe akilini mwako Baghdelleh alimwangaliaje baba ya rafiki yake ndani ya ile selo pembeni yuko Bwana Jela Munthali, kutoka Nyasaland.

Munthali akifahamiana vizuri sana na babu yangu kwani shamba la babu yangu lilipakana na jela.

Siku zote hujiuliza ingekuwaje kama Abdul Sykes angebakia Uyui Prison na jukumu la kukabiliana na babu yangu lingemwangukia yeye?

Abdul Sykes muda mfupi kabla ya uhuru alijiunga na Idara ya Magereza na akawa Bwana Jela Gereza la Uyui lakini hakukaa sana pale.

Babu yangu akimjua Abdul toka utoto wake pale Kipata Street na kwa hakika ingemtaabisha sana kuwa babu yangu awe mfungwa wake pale Uyui Prison.

Hakika uhuru ulikuja na changamoto nyingi zilizosababisha fitna kubwa katika jamii yetu.

Mzee Waikela anasema Baghdelleh alikuwa kila akizungumza na Waikela akimkazia macho na kuuma meno kujaribu kumtisha.

Waikela Mmanyema alimtazama Mnubi, Rashid Kheri Baghdelleh kwa kile Wamanyema wanaita, ''Kinyangarakata,'' yaani kijitu kisichokuwa na maana kibaraka tu na tarishi wa Nyerere.

Babu yangu alikuwa na orodha ya viongozi aliowaita ''vibaraka,'' waliowasaliti wafanyakazi na wakulima wa Tanzania na siku akifurahi anawataja kwa majina yao.

Lakini nikimuona Baghdelleh akija nyumbani kwetu kumtembelea baba yangu.

Baghdelleh alipatapo kumueleza baba yangu kuwa hapakuwa na njama ya kupindua serikali lakini kilichokuwa kinatafutwa ni kuwaweka ndani viongozi wote wa wafanyakazi ili ipatikane nafasi ya kuunda NUTA na kuviua vyama huru vya wafanyakazi.

Katika miaka niliyokuwa na wazee hawa wao wamekuwa walimu wangu wa si wa historia ya TANU, Mwalimu Nyerere na harakati za kuikomboa Tanganyika bali hata historia ya wazee wangu katika siku za ujana wao.

Nilipokuwa natafakari kuhusu miaka 90 ya maisha ya Balozi Abbas Sykes nikakumbuka mengi aliyonihadithia katika historia ya TANU.

1574519298886.png

Bilal Rehani Waikela na Mwandishi​

Itaendelea...
 
Kaka ninaposoma maandiko yako nakuwa kama naangalia sinema vile,unatia hamu ya kukusoma.
 
Huyu ni nani.nilishawahi kukutana nae
 
Attachments

  • Screenshot_20191124-173954_Google.jpg
    Screenshot_20191124-173954_Google.jpg
    65.3 KB · Views: 3
Nyerere kuvunja vyama vya wafanyakazi lilikuwa jambo la kidikteta.
 
Mohamed Saidi, nimeshajua tatizo lako, unaeleza historia ya Nyerere wakati una chuki nae kwa kumfunga jela baba yako ndio maana mara zote humuelezi kwa mema, una conflict of interest na Nyerere, Siku ukifuta chuki yako kwa Nyerere utakuwa mwandishi mzuri sana wa historia
 
Laki...
Hapana sina chuki na Nyerere wala sijapatapo kumsema kwa ubaya.
Tafuta mahali nilipomsema kwa ubaya lete ushahidi sote tuuone.
 
Balozi Abbas Kleist Sykes juma hili tarehe 4 September amefikisha umri wa miaka 90.

Kwa kipimo chochote kile ni kuwa Allah kamjaalia umri mrefu na tunamuombea maisha marefu na afya njema.

Katika kujua kwangu naamini kuna watu wawili tu ambao kwa sasa ndiyo waliobakia katika waasisi wa TANU ambao waliona yote katika historia ya TANU kuanzia mwanzo wake hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961 na wakamjua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa karibu sana katika miaka ile ya kupigania uhuru.

Watu hawa ni Bilali Rehani Waikela na Abbas Kleist Sykes na wote hawa waliwajua vizuri sana wazee wangu. Abbas Sykes na kaka zake Abdulwahid na Ally na baba yangu Said Salum walikulia mtaa mmoja Kipata Street nyumba zao zikiangaliana.

Mtaa huu sasa unajulikana kama Kleist Sykes Street.

Mzee Waikela alifungwa pamoja na babu yangu Salum Abdallah Iyui Prison, Tabora kufuatia maasi ya wanajeshi mwaka wa 1964.

Baada ya majeshi ya Waingereza kumaliza maasi yale viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi walikamatwa na kuwekwa ndani pamoja na wale wote waliodhaniwa ni wapinzani wa serikali.

Babu yangu alikuwa Rais wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) chama aliachoasisi mwaka wa 1955 mwaka mmoja baada ya yeye kuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tabora.

TRAU ilitokea kuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru ikipambana na serikali ya kikoloni bega kwa bega na TANU.

Mwaka wa 1960 TRAU chini ya uongozi wa babu yangu na Kassanga Tumbo iliendesha mgomo uliodumu siku 82 ukivunja rekodi ya mgomo wa Kenya wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh.

Babu yangu alipingana na Mwalimu Nyerere kwenye suala la kuvunja vyama vya wafanyakazi huru na kuwa na chama kimoja cha wafanyakazi nchi nzima chini ya TANU.

Babu yangu alimpinga Nyerere katika hili na kwa nia njema katika mkutano ulifanyika Moshi, kwa kumwambia yeye aendeshe serikali aviache vyama vya wafanyakazi vibaki huru kumrekebisha pale atakapokosea.

Mwalimu inaelekea hakupendezewa na maneno yale.

Hilo ndilo kilikuwa kosa la babu yangu ingawa propaganda zilizoenezwa wakati yeye akiwa jela ni kuwa alikuwa kwenye njama pamoja na wanajeshi walioasi ya kupindua serikali.

Katika vitu vilivyomuumiza nafsi yake ni pale yeye na wafungwa wenzie walipoambiwa waombe radhi kama sharti la kutolewa gerezani.

Babu yangu aliumia kwa sababu walikuwa wamesingiziwa uongo mkubwa sana.

Aliyekwenda jela kuwapa taarifa hii alikuwa Regional Commissioner wa Tabora Rashid Kheri Baghdelleh, rafiki ya baba yangu akimjua sana babu yangu.

Msomaji ingiza mwenyewe akilini mwako Baghdelleh alimwangaliaje baba ya rafiki yake ndani ya ile selo pembeni yuko Bwana Jela Munthali, kutoka Nyasaland.

Munthali akifahamiana vizuri sana na babu yangu kwani shamba la babu yangu lilipakana na jela.

Siku zote hujiuliza ingekuwaje kama Abdul Sykes angebakia Uyui Prison na jukumu la kukabiliana na babu yangu lingemwangukia yeye?

Abdul Sykes muda mfupi kabla ya uhuru alijiunga na Idara ya Magereza na akawa Bwana Jela Gereza la Uyui lakini hakukaa sana pale.

Babu yangu akimjua Abdul toka utoto wake pale Kipata Street na kwa hakika ingemtaabisha sana kuwa babu yangu awe mfungwa wake pale Uyui Prison.

Hakika uhuru ulikuja na changamoto nyingi zilizosababisha fitna kubwa katika jamii yetu.

Mzee Waikela anasema Baghdelleh alikuwa kila akizungumza na Waikela akimkazia macho na kuuma meno kujaribu kumtisha.

Waikela Mmanyema alimtazama Mnubi, Rashid Kheri Baghdelleh kwa kile Wamanyema wanaita, ''Kinyangarakata,'' yaani kijitu kisichokuwa na maana kibaraka tu na tarishi wa Nyerere.

Babu yangu alikuwa na orodha ya viongozi aliowaita ''vibaraka,'' waliowasaliti wafanyakazi na wakulima wa Tanzania na siku akifurahi anawataja kwa majina yao.

Lakini nikimuona Baghdelleh akija nyumbani kwetu kumtembelea baba yangu.

Baghdelleh alipatapo kumueleza baba yangu kuwa hapakuwa na njama ya kupindua serikali lakini kilichokuwa kinatafutwa ni kuwaweka ndani viongozi wote wa wafanyakazi ili ipatikane nafasi ya kuunda NUTA na kuviua vyama huru vya wafanyakazi.

Katika miaka niliyokuwa na wazee hawa wao wamekuwa walimu wangu wa si wa historia ya TANU, Mwalimu Nyerere na harakati za kuikomboa Tanganyika bali hata historia ya wazee wangu katika siku za ujana wao.

Nilipokuwa natafakari kuhusu miaka 90 ya maisha ya Balozi Abbas Sykes nikakumbuka mengi aliyonihadithia katika historia ya TANU.

View attachment 1270364
Bilal Rehani Waikela na Mwandishi​

Itaendelea...

14 October 2020​

Tabora, Tanzania

MZEE ASIMULIA YALIYOJIFICHA ENZI ZA NYERERE "NILIMPOKEA, AKANIWEKA 'KIZUIZINI', ALILALA KWANGU"

Mzee Bilali Rehani Waikela umri miaka 97 afanyiwa mazungumzo exclusive na Millard Ayo TV na pamoja na mahojiano aonesha kumbukumbu za picha kibao za wanasiasa mashuhuri wapigania uhuru ambazo amezihifadhi kwa zaidi ya miaka 60.

Hakika nyumba zake mbili za mjini Tabora ni makumbusho ya aina yake kukiwemo nyaraka, barua, kadi, beji na picha kibao zilizo katika hali njema kabisa.

Mzee Bilali Rehani Waikela enzi za ujana wake alikuwa fundi saa maarufu na mfanyabishara pia akijishughulisha na masuala ya kisiasa kupitia TANU na kijamii kama ya Muslim Welfare society kanda ya Tabora.
 
Mwaka 2016 mahojiano na Mzee Bilali Rehani Waikela

Historia Ya Tanganyika Kabla Ya Uhuru Na Matukio Yalio Jiri Wakati Wa Mwalimu Jk. Nyerere

Source : Hussein Waziry
 
Balozi Abbas Kleist Sykes juma hili tarehe 4 September amefikisha umri wa miaka 90.

Kwa kipimo chochote kile ni kuwa Allah kamjaalia umri mrefu na tunamuombea maisha marefu na afya njema.

Katika kujua kwangu naamini kuna watu wawili tu ambao kwa sasa ndiyo waliobakia katika waasisi wa TANU ambao waliona yote katika historia ya TANU kuanzia mwanzo wake hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961 na wakamjua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa karibu sana katika miaka ile ya kupigania uhuru.

Watu hawa ni Bilali Rehani Waikela na Abbas Kleist Sykes na wote hawa waliwajua vizuri sana wazee wangu. Abbas Sykes na kaka zake Abdulwahid na Ally na baba yangu Said Salum walikulia mtaa mmoja Kipata Street nyumba zao zikiangaliana.

Mtaa huu sasa unajulikana kama Kleist Sykes Street.

Mzee Waikela alifungwa pamoja na babu yangu Salum Abdallah Iyui Prison, Tabora kufuatia maasi ya wanajeshi mwaka wa 1964.

Baada ya majeshi ya Waingereza kumaliza maasi yale viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi walikamatwa na kuwekwa ndani pamoja na wale wote waliodhaniwa ni wapinzani wa serikali.

Babu yangu alikuwa Rais wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) chama aliachoasisi mwaka wa 1955 mwaka mmoja baada ya yeye kuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tabora.

TRAU ilitokea kuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru ikipambana na serikali ya kikoloni bega kwa bega na TANU.

Mwaka wa 1960 TRAU chini ya uongozi wa babu yangu na Kassanga Tumbo iliendesha mgomo uliodumu siku 82 ukivunja rekodi ya mgomo wa Kenya wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh.

Babu yangu alipingana na Mwalimu Nyerere kwenye suala la kuvunja vyama vya wafanyakazi huru na kuwa na chama kimoja cha wafanyakazi nchi nzima chini ya TANU.

Babu yangu alimpinga Nyerere katika hili na kwa nia njema katika mkutano ulifanyika Moshi, kwa kumwambia yeye aendeshe serikali aviache vyama vya wafanyakazi vibaki huru kumrekebisha pale atakapokosea.

Mwalimu inaelekea hakupendezewa na maneno yale.

Hilo ndilo kilikuwa kosa la babu yangu ingawa propaganda zilizoenezwa wakati yeye akiwa jela ni kuwa alikuwa kwenye njama pamoja na wanajeshi walioasi ya kupindua serikali.

Katika vitu vilivyomuumiza nafsi yake ni pale yeye na wafungwa wenzie walipoambiwa waombe radhi kama sharti la kutolewa gerezani.

Babu yangu aliumia kwa sababu walikuwa wamesingiziwa uongo mkubwa sana.

Aliyekwenda jela kuwapa taarifa hii alikuwa Regional Commissioner wa Tabora Rashid Kheri Baghdelleh, rafiki ya baba yangu akimjua sana babu yangu.

Msomaji ingiza mwenyewe akilini mwako Baghdelleh alimwangaliaje baba ya rafiki yake ndani ya ile selo pembeni yuko Bwana Jela Munthali, kutoka Nyasaland.

Munthali akifahamiana vizuri sana na babu yangu kwani shamba la babu yangu lilipakana na jela.

Siku zote hujiuliza ingekuwaje kama Abdul Sykes angebakia Uyui Prison na jukumu la kukabiliana na babu yangu lingemwangukia yeye?

Abdul Sykes muda mfupi kabla ya uhuru alijiunga na Idara ya Magereza na akawa Bwana Jela Gereza la Uyui lakini hakukaa sana pale.

Babu yangu akimjua Abdul toka utoto wake pale Kipata Street na kwa hakika ingemtaabisha sana kuwa babu yangu awe mfungwa wake pale Uyui Prison.

Hakika uhuru ulikuja na changamoto nyingi zilizosababisha fitna kubwa katika jamii yetu.

Mzee Waikela anasema Baghdelleh alikuwa kila akizungumza na Waikela akimkazia macho na kuuma meno kujaribu kumtisha.

Waikela Mmanyema alimtazama Mnubi, Rashid Kheri Baghdelleh kwa kile Wamanyema wanaita, ''Kinyangarakata,'' yaani kijitu kisichokuwa na maana kibaraka tu na tarishi wa Nyerere.

Babu yangu alikuwa na orodha ya viongozi aliowaita ''vibaraka,'' waliowasaliti wafanyakazi na wakulima wa Tanzania na siku akifurahi anawataja kwa majina yao.

Lakini nikimuona Baghdelleh akija nyumbani kwetu kumtembelea baba yangu.

Baghdelleh alipatapo kumueleza baba yangu kuwa hapakuwa na njama ya kupindua serikali lakini kilichokuwa kinatafutwa ni kuwaweka ndani viongozi wote wa wafanyakazi ili ipatikane nafasi ya kuunda NUTA na kuviua vyama huru vya wafanyakazi.

Katika miaka niliyokuwa na wazee hawa wao wamekuwa walimu wangu wa si wa historia ya TANU, Mwalimu Nyerere na harakati za kuikomboa Tanganyika bali hata historia ya wazee wangu katika siku za ujana wao.

Nilipokuwa natafakari kuhusu miaka 90 ya maisha ya Balozi Abbas Sykes nikakumbuka mengi aliyonihadithia katika historia ya TANU.

View attachment 1270364
Bilal Rehani Waikela na Mwandishi​

Itaendelea...
Andiko limenfinya macho.Hawa wazee bado wapo?Mungu aendelee kuwasimamia.natumaini umechota maarifa ya kutosha kutoka kwao.
 
Da! Kuna mambo mengi kumbe yamejificha sana nyuma ya uhuru wetu. Naipenda sana JF kwa kuwa mwalimu mzuri na taa katika msitu mnene wa fikra na ufahamu wa mambo. Abarikiwe sana mbeba maono na mwanzilishi wa jamvi hili.
 
Back
Top Bottom