Abbas Max (1918 - 1993): Kumbukumbu za Uhuru 1961

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU ZA UHURU: ABBAS MAX WA IRINGA (1918 - 1993)

Abbas Max ana historia ya kusisimua sana kama ilivyo kwa wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini kwa bahati mbaya historia imewasahau.

John Iliffe mwanahistoria nguli aliyeiokoa historia ya Tanganyika amepata kusema kuwa historia nyingi ya TANU ipo katika mikono ya watu binafsi.

Iliffe alisema maneno haya katika miaka ya 1960 lakini kwa sasa ni wazi kuwa historia nyingi ya TANU si tu iko katika mikono ya watu binafsi bali iko pia katika masanduku na makabati yaliyoachwa na wazalendo wale waliopigania uhuru ambao takriban wote wameshatangulia mbele ya haki.

Historia hii ndani ya makabati na masanduku ya hawa wazalendo ni picha za "black and white" na nyaraka zilizoandikwa kwa mkono na type writer.

Siku chache zilizopita katika kutayarisha vipindi kwa ajili ya Nyerere Day nilitembelewa na waandishi na katika kuhitimisha mazungumzo yetu wakawa wanataka kujua majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini wamesahaulika.

Ndipo nilipolitaja jina la Abbax Max katika video ambayo tulikuwa tunarekodi.
Hii video fupi ipo hapo FB.

Mtoto wa Abbas Max, Ally Abbas Max baada ya kuiona hii video siku ya pili tu akanitumia picha ya baba yake na ''cuttings'' za gazeti kuhusu historia ya marehemu baba yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ally Abbas Max kwa miaka mingi alikuwa Marekani na sikutegemea kama atakuwa na kumbukumbu za baba yake huko alikokwenda ughaibuni.

Ally amenitia moyo sana aliponiambia kuwa baba yake ameacha nyaraka na zimehifadhiwa hadi leo zaidi ya miaka 30 toka kufariki kwake, ni kiasi cha kuzifungua tu na bila shaka mengi yatajulikana jinsi yeye na wenzake walivyofungua tawi la kwanza la TANU Iringa mwaka wa 1955.

Naeleza hapa yale niliyoweza kupata kutoka kwa Ally Abbas Max nikichanganya kidogo na yangu.

Inawezekana watu wengi wasijue kuwa Chief Adam Sapi Mkwawa ni mtu wa kwanza kuingia TANU Iringa.

Chief Mkwawa aliwaalika Abdul Sykes na Dossa Aziz Kalenga katika sherehe ya kupokea fuvu la babu yake Chief Mkwawa kutoka Ujerumani.

Hili fuvu liliwasili Dar es Salaam tarehe 9 Julai 1954 na kupelekwa iringa siku mbili tu baada ya TANU kuasisiwa.

Katika mazungumzo ya faragha baina ya Chief Adam Sapi Mkwawa, Dossa Aziz na Abdul Sykes, Chief Adam Sapi akakata kadi ya TANU kwa siri.

Abbas Max amewaeleza watoto wake kuwa Abdul Sykes alikuja Iringa wakati tayari TANU ishapamba moto Dar es Salaam na alifikia nyumbani kwake.

Abdul Sykes alikuwa anaelekea Njombe kumtembelea mume mwenzie.
Abbas Max akaamua kumpeleka Njombe na gari yake Peugeot Pickup 203.

Mazungumzo baina yao yalikuwa kuhusu TANU, Nyerere na juhudi za kudai uhuru.

Abbas Max akamwambia Abdul Sykes amwambie Nyerere aje Iringa ili wafungue tawi la TANU na wao wawemo ndani ya juhudi hizi za kupigania uhuru.

Hakupita muda Abdul Sykes akamtumia Abbas Max taarifa kuwa Nyerere atafika Iringa akitokea Lindi, Songea na Njombe.

Abbas Max alitoka na wazalendo wenzake kwenda kumpokea Julius Nyerere njiani nje ya mji wa Iringa.

Nyerere alikuwa ameongozana na Ally Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani na dereva wa TANU Omari Simba.

Nyerere alimfahamisha Abbas Max kuwa ili kufungua tawi la TANU kwanza lazima awe na wanachama 12 wanye kadi za TANU.

Watu walikuwa wanaogopa kuingia chama na hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Abbas Max.
Nyerere aifanya mkutano wa hadhara Iringa lakini ulihudhuriwa na watu wachache.

Juu ya haya yote Abbas Max aliweza kupata watu waliokuwa tayari kujiunga na TANU na hawa walikuwa: Saleh Masasi ambae Nyerere alilala nyumbani kwake, Hussein Issa, Hussein Kandoro, Yasin Hamid, Ahmed Mahmoud, Abdulrahman Mwangili, Juma Lipinjime na Khalfani Ally, Abbas Max akiwa Mwenyekiti.

Katika mkutano wa Kura Tatu Tabora mwaka wa 1958 Abbas Max akachaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauru Kuu ya TANU hivyo ikabidi ajiuzulu uenyekiti.

Nafasi yake ikachukuliwa na Chogga.

Chogga ameacha historia ya pekee katika wanasiasa ndani ya TANU waliokuwa mwiba wa koo kwa Julius Nyerere.

Itapendeza sana kama wanahistoria wataandika historia hii yake kwani mwaka wa 1968 Chogga na wenzake walifukuzwa TANU.

Ikutoshe tu kuwa Abbas Max anasema kuwa Chogga alisababisha TANU ifungiwe iringa.

Hii ikapelekea Abbas Max na wenzake waendeshe harakati zao chinichini kupitia Jambo Club waliyoianzisha baada ya TANU kupigwa marufuku.

Safari ya pili Nyerere alipokwenda Iringa alifikia nyumbani kwa Abbas Max.

Abbas Max alitembea kote na Nyerere Nyanda za Kati Kusini katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Charles Mzena ambae wakati wa kupigania uhuru alikuwa Special Branch alipata kumwambia Salum Khamis wakati huo uhuru ushapatikana kuwa, ''Chief Adam Sapi Mkwawa alikuwa ndiyo chief wa Wahehe lakini Abbas Max wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika alikuwa na nafasi yake juu ya Chief Adam Sapi.''

Abbas Max alikuwa na kawaida katika misafara ile na Nyerere kuwa wakati wa kula yeye alikuwa akisubiri hadi dakika ya mwisho wakati chakula kimetengwa na wanaanza kula yeye atampora Nyerere sahani yake na kumpa ya kwake.

Nyakati zile zilikuwa nyakati ngumu na Nyerere alikuwa akiwindwa.
Abbas Max alikuwa akisema, ''Hakuna huku wa kunidhuru mimi.''

Historia ya Abbas Max katika kupigania uhuru wa Tanganyika ina mengi sana.

Mimi Inshaa Allah nasubiri siku wanae watakapofungua Nyaraka za baba yao Abbas Max na kuziweka hadharani zisomwe na wanahistoria.

Tunamuomba Allah awarehemu wazee wetu hawa waliopigania uhuru wa nchi yetu kwa hali na mali zao.

Amin.

Picha ya kwanza ni Abbas Max.
Picha ya pili kulia ni Abbas Max, Julius Nyerere na Chande Ali.

Picha ya tatu kushoto ni Abbas Max ameegemea gari akiwa na Julius Nyerere na msafara wake.

Picha ya nne Mzee Abbas Max na mjukuu wake.

Screenshot_20211104-063117_Facebook.jpg
 
Mzee wangu mada zako huwa nzuri lakini zina mashaka mengi.

Kwa hiyo Abas Max huko Iringa alikofungua hilo tawi lilikuwa na wanachama Waislamu tupu?
 
Jer...
Hivi ndivyo ilivyokuwa ndugu yangu kuanzia kuasisiwa kwa African Association mwaka wa 1929 hadi TANU 1954.

Wala isikupitikie kuwa mimi naandika uongo.

Najua unataabika lakini hatuwezi kubadilisha historia.
 
Mzee wangu mada zako huwa nzuri lakini zina mashaka mengi..

Kwa hiyo Abas Max huko Iringa alikofungua hilo tawi lilikuwa na wanachama waislamu tupu?
Badala ya kutilia mashaka, kwangu naona hii ni researchable subject.

Dar es salaam, majina ya MWANZO yakijaa watu wenye majina ya Kiislamu, at least inaweza ku-make sense hususani kwa wakati huo ambao mwingiliano na watu wa bara haukuwa mkubwa sana!

Hawa watu wa bara ni wale ambao wengi walikuwa/wana majina ya Kikristo au ya kiasili!!!

Iringa nako, ambako na-assume watu wenye majina ya Kikristo ni wengi zaidi kuliko wale wenye majina ya Kiislamu, of course, siwezi ku-doubt kilichoandikwa lakini it surprises me!!

Hilo linanifanya nijiulize maswali kadhaa, assuming anayoeleza Mohamed Said ni SAHIHI... yaani hapa nampa the benefit of the doubts hadi pale mtu mwingine anatakapokuja na maelezo tofauti!

Maswali ninayojiuliza ni haya:-

1. Je, inawezekana Watanganyika, kwa namna fulani waligawanyika kwa mitazamo ya kidini?

Kwamba, Waislamu walimuona Mkoloni Mwingereza kama kafiri anayetakiwa kuondoka kwenye ardhi yao na kwahiyo kwao ilikuwa rahisi kuunga kwa wepesi zaidi juhudi za kumuondoa Mkoloni Mkristo?.

2. Je, inawezekana Wakristo walipata hamasa taratibu kwa kuona anayepingwa ni Mkrisro mwenzao aliyaweletea Neno la Mungu?

3. Je, inawezekana kwavile wanaharakati wa mwanzo na wenye majina walikuwa ni Waislamu, kwahiyo hawa walitumia Misikiti kutafuta uungwaji mkono, na ndo maana mahali kama Iringa waliojitokeza mapema zaidi ni Waislamu kwavile walifikiwa kirahisi misikitini?

4. Je, inawezekana lau kama harakati za kupigania uhuru zingekuwa ni dhidi ya Mwarabu, hivi sasa historia ya watu kama akina Mohamed Said ingekuwa tofauti...

...kwamba, watu wa mwanzo kwenye harakati hizo kwenye kila mkoa wangekuwa Wakristo wanaotaka kumuondoa Kafiri la Kiislamu lililopo kwenye ardhi yao, huku Waislamu wakijiweka nyuma kwenye harakati hizo?

5. Je, inawezekana kwa kuwa watumishi wa Mkoloni wengi wao walikuwa ni Wakristo waliopewa elimu na mkoloni, hawa kwa makusudi, na sana sana wakiongozwa na ubinafsi, baadhi yao hawakuwa tayari kumpinga mkoloni kwa sababu ya kutetea kitumbua chao, wakati wao ndo walitarajiwa kuwa wa mwanzo zaidi?
 
Mzee wangu, vipi hizi nondo natamani ziingie wikipedia maana kule zitatambaa sana na kuinfluence zaidi. Naweza kuzipeleka?
 
Andoza,
Zipeleke hakuna kizuizi.

Nitashukuru ukinipatia link ukishakamilisha.
 
Mzee MS akikujibu nitag
 
Mijini kipindi hicho wenye dini ni waislam,wengine wengi wapagani,hapo kanisa Lina miaka Kama 90 hivi tanganyika
 
Back
Top Bottom