Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ILIPOKUWA NYUMBA YA ABBAS MAX MUASISI WA TANU IRINGA
Hapa ni Iringa sehemu nayojulikana kama Makorongoni.
Mtaa huu ni Mtaa wa Pangani.
Hapa ndipo ilipokuwa nyumba ya Abbas Max (1918 - 1993) muasisi wa TANU.
Nimepata kuandika historia ya Abbas Max na niliandika maneno haya, ''Abbas Max ameacha nyaraka na zimehifadhiwa hadi leo zaidi ya miaka 30 toka kufariki kwake, ni kiasi cha kuzifungua tu na bila shaka mengi yatajulikana jinsi yeye na wenzake walivyofungua tawi la kwanza la TANU Iringa mwaka wa 1955.''
Hizi nyaraka bado hazijafunguliwa lakini nimebahatika leo kufika ilipokuwa nyumba yake Iringa, Makorongoni, Mtaa wa Pangani.
Mtaa wa Pangani ni Mtaa mrefu.
Miaka ya 1950 Abbas Max alipokuwa kijana barabara hii iliyokuwa inapita mbele ya nyumba za huo mtaa ilikuwa barabara ya vumbi.
Leo mtaa huu barabara yake ni ya lami na pembezoni make kuna majumba mazuri yenye maduka ya biashara za kila aina kuanzia saluni hadi show room za samani za kuvutia.
Nyumba ya Abbas Max haipo iliuzwa na badala yake iipokuwa nyumba yake au tuseme nyumba zake kwa kuwa hapo kulikuwa na nyumba mbili, moja ya mama yake pamejengwa godown kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
Mama yake Abbas Max Bi. Seluwanga Sekinyaga alikuwa na nyumba Miyomboni ambayo Abbas Max ndipo alipokulia.
Huyu mama alikuwa mfanya biashara na nyumba yake ingawa imejengwa miaka mingi labda zaidi ya miaka 80 iliyopita inajieleza yenyewe kwa aina ya mjengo wake kuwa hii ilikuwa familia ya watu waliofanikiwa kimaisha.
Picha ya nyumba hii ingawa haiba yake yote haionekani kwa kuwa mbele zimejengwa fremu za biashara lakini ukiiangalia kwa juu utaona kuwa mjengo wake ulikuwa mjengo wa kupendeza.
Abbas Max alijenga nyumba hapo Miyomboni pembeni ya nyumba ya mama yake na hii nyumba iliyokuwapo hapo ina historia ya pekee katika mji wa Iringa.
Hapo kwenye nyumba hiyo ndipo zilipokuwa zikifanyika harakati zote za kupigania uhuru wa Tanganyika na Mwalimu Nyerere hapa ndipo yalipokuwa makazi yake nyumbani mbali na nyumbani kwake kila alipofika Iringa.
Historia hii imepotea kwa kule kuvunjwa nyumba hiyo lau kama kumbukumbu ya nyumba hiyo bado inaishi katika vichwa vya watoto wake.
Itaendelea Insha Allah...
Ikiwa mtafiti atatafiti historia ya TANU Iringa atakuta kuwa kama muasisi wa TANU Abbas Max ndiye mwanachama no. 1 Iringa na sababu ni kuwa yeye ndiye aliyetafuta wanachama wa mwanzo na ndiye aliyekisajili chama.
Ilikuwa kazi ngumu sana na sababu ni kuwa watu walikuwa wanaogopa serikali na wengine walikuwa hawana hata fedha za kununua kadi.
Abbas Max yeye alibeba jukumu lote hilo hadi kuwalipia wanachama kadi zao.
Lakini ukweli ni kuwa Abbas Max hakuwa mwanachama wa TANU wa kwanza Iringa.
Mwanachama wa kwanza wa TANU Iringa alikuwa Chief Adam Sapi Mkwawa.
Hili litawashangaza wengi kwa kuwa machifu wote walijiweka mbali sana na siasa za kupigania uhuru.
Ikiwa hivi ndivyo sasa ilikuwaje Chief Adam Sapi akawa na kadi ya TANU?
Wakati Abdul Sykes alipokuwa kiongozi wa TAA kwanza kama Secretary 1950 kisha Act. President 1951 hadi 1953, alijenga uhusiano mzuri sana na machifu wote wa Tanganyika.
Machifu wote walikuw akila wakija Dar es Salaam lazima watafikanumbani kwake kumsalimia.
Chief Adam Sapi Mkwawa alikuwa mmoja wa machifu hawa.
Mwaka wa 1954 fuvu la Mtwa Mkwawa liliporejeshwa Tanganyika kutoka Ujerumani Chief Mkwawa aliwaalika Abdul Sykes na Dossa Aziz Kalenga katika sherehe ya kupokea fuvu la babu yake.
Hilii fuvu lilipokelewa Dar es Salaam tarehe 9 Julai 1954 na TANU tayari ilikuwa imeshaasisiwa.
Katika mazungumzo ya faragha baina ya Chief Adam Sapi Mkwawa na hawa wageni wake walimweleza kuhusu TANU na maazimio yake ya kudai uhuru.
Chief Adam Sapi Mkwawa hakusita hapo hapo kwa siri kubwa aliingia TANU.
Ilikuwa Abdul Sykes ndiye aliyemfikishia Abbas Max TANU.
Abbas Max na Abdul Sykes walijuana vipi?
Abbas Max ana historia ndefu na ya kusisimua lakini hapa hatuwezi kuihadithia yoote kwa ukamilifu wake.
Kwa nini Abbas Max alicha shule Tabora School na kuja Dar es Salaam kuanza kazi Tanganyika Railways na vipi kuacha kwake shule kukamuingiza katika siasa nk. nk.
Abbas Max aliingia Tanganyika Railways akamkuta Kleist Sykes pale akawa mmoja wa wazee wake na hivi ndivyo alivyokuja kujuana na Abdul Sykes na nduguze.
Urafiki wao hapa ndipo ulipoanzia katika Dar es Salaam ya miaka ya mwishoni 1930 mwishoni kabisa kuingia 1940s.
Hapa kuna jambo lazima nilieleze.
Abbas Max na Adam Sapi Mkwawa walikuwa marafiki wakubwa sana toka udogoni na uhusiano huu ulivuka mipaka yote ya urafiki kufikia rafiki ndugu.
Abdul Sykes na yeye alikuja kuelewana vyema sana na Chief Adam Sapi Mkwawa ujanani wakati huo tayari Adam Sapi kakalia kiti cha uchifu wa Wahehe.
Mwaka wa 1955 Abdul Sykes alikuwa akienda Njombe akapita Iringa na kufikia nyumbani kwa Abdul Sykes Makorongoni.
Abbas Max alisoma Malangali Secondary School pamoja na Adam Sapi Mkwawa na baada ya hapo akaenda Tabora School ambako alikuwa na wanafuzi wenzake kama kwa kuwataja wachache walikuwa Charles Mtawali na Hans Poppe.
Hans Poppe na Abbas Max mama zao walikuwa marafiki wakubwa na waliwalea watoto wao pamoja kama ndugu wa kuzaliwa tumbo moja.
Hiki ni kisa kingine kabisa lakini ikutoshe tu kuelewa kuwa Abbas Max na Hans Poppe walinyonya ziwa moja.
Kwa sheria ya Kiislam hawa ni ndugu na watoto wao hawawezi kuoana mradi wamenyonya ziwa moja.
Wanasayansi pekee ndiyo wanaweza kueleza kwanini Allah kapitisha hukumu hii.
Shule ya Malangali ilikuwa kati ya shule bora wakati wa ukoloni na ilitoa viongozi wengi katika harakati ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Abbas Max akaamua kumpeleka Abdul Sykes Njombe na gari yake Peugeot 203.
Ilikuwa wakati wako dani ya gari hii wakielekea Njombe ndipo Abdul Sykes akamweleza Abbas Max kuhusu TANU.
Abbas Max akamwambia Abdul Sykes afanye mipango Nyerere afike Iringa ili wafungue tawi la TANU ili sehemu hii ya Tanganyika ishiriki katika kupigania uhuru.
Haukupita muda mrefu Abbas Max akapokea telegram kutoka kwa Abdul Sykes kuwa Nyerere anakuja Iringa na wajiandae kumpokea.
Nyerere alifika Iringa akitokea Lindi na akapokelewa na Abbas Max.
Nyerere alihutuia mkutano wa hadhara lakini wananchi wa Iringa walikuwa bado wanasita kuipokea TANU.
Mkutano haukupata mahudhurio makubwa.
Itaendelea In Shaa...