Abbas sykes (1929 - ) Sehemu ya pili: Mjumbe wa kamati ya Saadan Abdu Kandoro na Japhet Kirilo kuchangisha fedha kupeleka mjumbe UNO 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ABBAS SYKES (1929 - ) SEHEMU YA PILI:
MJUMBE WA KAMATI YA SAADAN ABDU KANDORO NA JAPHET KIRILO KUCHANGISHA FEDHA KUPELEKA MJUMBE UNO 1953

Mwaka wa 1952 Japhet Kirilo akiongozana na Earle Seaton alikwenda UNO kuwasilisha malalamiko ya dhulma ya Wameru walioporwa ardhi yao na Wazungu Meru.

Kirilo alirudi Tanganyika mikono mitupu.

Uongozi wa TAA Makao Makuu Abdul Sykes akiwa mstari wa mbele ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Ilikuwa Abdul ndiye aliyemtaka Seaton aisaidie Meru Citizens Union kutayarisha petition yao na kuiwakilisha UNO.

Itakumbukwa kuwa ilikuwa huyu huyu Seaton ndiye aliyeisaidia TAA Political Commitee kuandika memorandum yao kwa Constitutional Develompent Commitee ya Gavana Edward Twining.

Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa ipite katika mikoa iliyochaguliwa kuchangisha fedha na kuwaeleza wananchi kuwa wakati umefika wa kudai uhuru.

Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA chini ya Mzee John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.

Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.
Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.

Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.

Abbas Sykes ana historia nzuri sana kuhusu picha ya Waasisi wa TANU, New Street 1954
Kuna picha mashuhuri sana ya wanachama waasisi wa TANU.

Picha hiyo ilipigwa na Gomes mpiga picha maarufu sana wa Ki-Goa katika siku zile.
Abdul Sykes alikuwa amepatana na Gomes aje makao makuu ya TAA kupiga picha hiyo ya kihistoria.
Kwa bahati mbaya Gomes alichelewa kufika ofisi ya TAA.

Abdulwahid alikosa subira kwa hiyo, alimwomba Abbas aende kumchukua Gomes kutoka kwenye studio yake Acacia Avenue (siku hizi Samora Avenue) katikati ya mji.

Chombo pekee cha usafiri walichokuwa nacho TAA ilikuwa baiskeli moja iliyochakaa.

Wakati Abbas ananyonga baiskeli kuelekea mjini kumchukua Gomes, Gomes alikuwa keshaondoka anakuja makao makuu ya TAA; kwa hiyo wakaipishana njiani.

Hivi ndivyo Abbas Sykes alivyokosa kuwepo ndani ya picha hiyo mashuhuri.

Katika picha hiyo wanachama watatu hawaonekani, Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu.

Hawa walikuwa watumishi wa serikali na kwa kanuni za utumishi katika serikali ya Kiingereza, watumishi wa serikali walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa.

Mwafrika yoyote aliyevunja amri hiyo kuu adhabu yake ilikuwa kufukuzwa kazi mara moja.
Kwa hiyo picha hiyo ilipopigwa Ally, Tewa na Kasella Bantu walijiondoa.

Kiasi cha kama juma moja baada ya kuundwa kwa TANU Zuberi Mtemvu akamwambia Nyerere waende Morogoro wakakitangaze chama:

Mtemvu alimuelezea Ally kwa ufupi juu ya mkutano wao na Nyerere Morogoro mjini na aliomba apewe mara moja kadi 200 za TANU na akamfahamisha kuwa ameongea na Ali Mwinyi Tambwe kuhusu TANU na amekubali kujiunga na chama.

Ally aliwaandikia na kuwapa kadi za uanachama wa TANU, Mtemvu na Tambwe na akamwambia mdogo wake Abbas, awaalike wote wawili kwenye mkutano wa uzinduzi wa tawi la TANU la Dar es Salaam ambao ulikuwa ufanyike Jumamosi iliyofuata.

Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Abbas Sykes alinihadithia anasema Nyerere alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Pugu kuja kuonana na kaka yake alikuwa anapanda basi moja la Muhindi likiitwa ''Majigo.''

Kituo cha basi hili kilikuwa Mtaa wa Msimbazi na Aggrey.

Ukiingia na mzigo ndani ya basi basi yule Muhindi utamsikia akipiga kelele, ''Majigo juu, majigo juu.''
Maana ya maneno haya ilikuwa, ''Mzigo juu.''

Yaani mizigo ipandishwe juu ya basi kwenye ''carrier.''

Hivi ndivyo basi lile lilivyopata umaarufu wake na kuishia kuitwa ''Majigo.''
Hiki kilikuwa kipindi kabla ya Nyerere hajajiuzulu ualimu.

Nyerere alikkuwa akishashuka pale kwa Majigo atashika njia kuelekea Kariakoo Market ofisini kwa Market Master Abdul Sykes.

Abbas Sykes kashuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe akiwa kijana mdogo wa miaka 20 hivi.
Huwa sichoki kumsikiliza Balozi Abbas Sykes.

Picha ya kwanza ni Waasisi wa TANU, picha ya pili ni Kariako Market 1950s na picha ya tatu wa kwanza kushoto ni Japhet Kirilo.

Itaendelea...
 
Attachments

  • 1567911586573.png
    1567911586573.png
    18.1 KB · Views: 16
Mzee uko vizuri endelea kutupa nondo tuijue historia yetu.....
 
Nimependa huo ufafanuzi wa watu waliokosekana kwenye picha ya waasisi wa TANU. Hapa umetusaidia kuelewa kwa Kasela Bantu ni mmoja wa wasisi wa TANU. Ningeomba baadae utupe kwa kina kisa cha Kasela Bantu na Nyerere. Pia itapendeza sana kama ukiendelea na udadavuzi wa kina wa kisa cha Zuberi Mtemvu na TANU. Ingawa tumesoma japo kiduuuchu kwenye historia lakini itafaa sana kama tukapata habari zenye kina kuhusu hao watu niliowataja.
 
ABBAS SYKES (1929 - ) SEHEMU YA PILI:
MJUMBE WA KAMATI YA SAADAN ABDU KANDORO NA JAPHET KIRILO KUCHANGISHA FEDHA KUPELEKA MJUMBE UNO 1953

Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.
Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.

Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.
Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.

Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.

Abbas Sykes ana historia nzuri sana kuhusu picha ya Waasisi wa TANU, New Street 1954
Kuna picha mashuhuri sana ya wanachama waasisi wa TANU.

Picha hiyo ilipigwa na Gomes mpiga picha maarufu sana wa Ki-Goa katika siku zile.
Abdul Sykes alikuwa amepatana na Gomes aje makao makuu ya TAA kupiga picha hiyo ya kihistoria.
Kwa bahati mbaya Gomes alichelewa kufika ofisi ya TAA.

Abdulwahid alikosa subira kwa hiyo, alimwomba Abbas aende kumchukua Gomes kutoka kwenye studio yake Acacia Avenue (siku hizi Samora Avenue) katikati ya mji.

Chombo pekee cha usafiri walichokuwa nacho TAA ilikuwa baiskeli moja iliyochakaa.

Wakati Abbas ananyonga baiskeli kuelekea mjini kumchukua Gomes, Gomes alikuwa keshaondoka anakuja makao makuu ya TAA; kwa hiyo wakaipishana njiani.

Hivi ndivyo Abbas Sykes alivyokosa kuwepo ndani ya picha hiyo mashuhuri.

Katika picha hiyo wanachama watatu hawaonekani, Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu.

Hawa walikuwa watumishi wa serikali na kwa kanuni za utumishi katika serikali ya Kiingereza, watumishi wa serikali walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa.

Mwafrika yoyote aliyevunja amri hiyo kuu adhabu yake ilikuwa kufukuzwa kazi mara moja.
Kwa hiyo picha hiyo ilipopigwa Ally, Tewa na Kasella Bantu walijondoa.

Kiasi cha kama juma moja baada ya kuundwa kwa TANU Zuberi Mtemvu akamwambia Nyerere waende Morogoro wakakitangaze chama:

Mtemvu alimuelezea Ally kwa ufupi juu ya mkutano wao na Nyerere Morogoro mjini na aliomba apewe mara moja kadi 200 za TANU na akamfahamisha kuwa ameongea na Ali Mwinyi Tambwe kuhusu TANU na amekubali kujiunga na chama.

Ally aliwaandikia na kuwapa kadi za uanachama wa TANU, Mtemvu na Tambwe na akamwambia mdogo wake Abbas, awaalike wote wawili kwenye mkutano wa uzinduzi wa tawi la TANU la Dar es Salaam ambao ulikuwa ufanyike Jumamosi iliyofuata.

Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Abbas Sykes alinihadithia anasema Nyerere alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Pugu kuja kuonana na kaka yake alikuwa anapanda basi moja la Muhindi likiitwa ''Majigo.''

Kituo cha basi hili kilikuwa Mtaa wa Msimbazi na Aggrey.

Ukiingia na mzigo ndani ya basi basi yule Muhindi utamsikia akipiga kelele, ''Majigo juu, majigo juu.''
Maana ya maneno haya ilikuwa, ''Mzigo juu.''

Yaani mizigo ipandishwe juu ya basi kwenye ''carrier.''

Hivi ndivyo basi lile lilivyopata umaarufu wake na kuishia kuitwa ''Majigo.''
Hiki kilikuwa kipindi kabla ya Nyerere hajajiuzulu ualimu.

Nyerere alikkuwa akishashuka pale kwa Majigo atashika njia kuelekea Kariakoo Market ofisini kwa Market Master Abdul Sykes.

Picha ya kwanza ni Waasisi wa TANU, picha ya pili ni Kariako Market 1950s na picha ya tatu wa kwanza kushoto ni Japhet Kirilo.

Itaendelea...
https://www.facebook.com/photo.php?...4BbLDr59AMBYryTHWfpjvItYAB4j3SW_Sh05gXreECfbW

Safi sana mkuu.
 
mi ninachojua safari ya Nyerere UNO ilifadhiliwa na baba yake Freeman Mbowe wa CHADEMA
 
Wakiochangia huo mfuko Ni wengi tu akiwemo na akina Bomani wa mwanza, mzee Kagasheki wa bukoba, na akina masasi wa iringa na wengineo. Hawa Ni watu waliokuwa vizuri kifedha kabla ya Uhuru enzi hizo
 
Back
Top Bottom