Abdi Banda ashikiliwa na polisi akituhumiwa kwa wizi wa gari

Abdi Banda ashikiliwa na polisi akituhumiwa kwa wizi wa gari

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
6,941
Reaction score
7,808
Beki wa Simba, Abdi Banda anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tanzania kwa tuhuma za kushiriki upotevu wa gari lililoibiwa.

Habari za uhakika zilizoifikia SALEHJEMBE zimeeleza kuwa Banda anashikiliwa pamoja na mdogo wake kwa tuhuma za wizi wa gari linalomilikiwa na mwanamke mmoja aliyeelezwa kuwa ni mpenziwe.

Ingawa viongozi wa Simba wamekuwa wagumu kupatikana na kuzungumzia suala hilo, lakini SALEHJEMBE imethibitisha Banda ameshikiliwa kituoni hapo tokea jana usiku.

Mmoja wa askari wa kituo cha Magomeni amethibitishwa kushikiliwa kwa beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo na uchunguzi unaendelea.

“Kweli yuko kituoni anashikiliwa, anashikiliwa yeye na mdogo wake kuhusiana na kuibiwa kwa gari la dada mmoja anayeelezwa ni mpenzi wa mchezaji huyo,” alisema.

Taarifa zinaeleza Banda amekuwa akilianzima gari hilo na kulitumia kila mara.

“Kweli amekuwa akilitumia gari hilo lakini yeye hajui kuendesha. Mdogo wake amekuwa akiendesha gari hilo na kuna mkanganyiko wa taarifa.

“Inaelezwa wakati linapotea yeye alikuwa jijini Mbeya Simba ilipokwenda kuivaa Mbeya City. Lakini mmiliki wa gari anasisitiza Banda ndiye alilianzima kupitia mdogo wake. Hivyo tumewaachia polisi wafanye kazi yao,” alieleza ndugu wa Banda.

Viongozi wa Simba walikuwa hawapokei simu zao lakini ilielezwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Stephen Ally alikuwa katika kituo hicho cha Magomeni akilishughulikia suala hilo.

Source:http://salehjembe.blogspot.in/2015/04/exclusive-abdi-banda-ashikiliwa-na.html
 
Kuna uhusiano Kati ya mikia na wizi!Toka zaman ukianzia kwa Mambosasa,Michael Paul,Christopher Alex na Leo Banda wote wameshalala Central kwa tuhuma za ukibaka
 
Mchezaji wa simba hawezi kuendesha gari?????? Banda ni mariooo na wafungwe tu usikute gari yenyewe ni gx90 au collora ya 80.
 
Huu uandishi uchwara. Mwandishi smeshindwa kutaja hata aina ya gari!!!??

Tiba
 
Huu uandishi uchwara. Mwandishi smeshindwa kutaja hata aina ya gari!!!??

Tiba
Hatuna haja ya kufahamu aina ya gari, hata kama angeiba mkokoteni. Point hapa ni kwamba mchezaji wa simba Abdi Banda ameiba gari.........
 
Aliyeibiwa gari ni nani (huyo mdada)
 
Hatuna haja ya kufahamu aina ya gari, hata kama angeiba mkokoteni. Point hapa ni kwamba mchezaji wa simba Abdi Banda ameiba gari.........

Kwani wewe unamsemea nani unaposema "hatuna" haja. Wewe nani mwingine? Kama wewe huna haja, mimi nina haja ya kujua ni gari aina gani lililoibiwa.

Tiba
 
Kwani wewe unamsemea nani unaposema "hatuna" haja. Wewe nani mwingine? Kama wewe huna haja, mimi nina haja ya kujua ni gari aina gani lililoibiwa.

Tiba

Umeshaambiwa Passo used mkuu...!!!.
 
Kuna uhusiano Kati ya mikia na wizi!Toka zaman ukianzia kwa Mambosasa,Michael Paul,Christopher Alex na Leo Banda wote wameshalala Central kwa tuhuma za ukibaka
Hahahaha umewaza mbali
 
Hatuna haja ya kufahamu aina ya gari, hata kama angeiba mkokoteni. Point hapa ni kwamba mchezaji wa simba Abdi Banda ameiba gari.........

Ni kweli sie tunaanzia hapo
 
Kuna uhusiano Kati ya mikia na wizi!Toka zaman ukianzia kwa Mambosasa,Michael Paul,Christopher Alex na Leo Banda wote wameshalala Central kwa tuhuma za ukibaka

Umemsahau yule manara aliekuwa pia mwenezi wa chama tawala
 
Mimi nafikiria kivingine,huenda Banda alimnunulia gari huyo mwanamke na ameamua kumpora na bint kaamua kwenda kushtak polisi kivingine.HUENDA!!!!!!!!!
 
Mimi nafikiria kivingine,huenda Banda alimnunulia gari huyo mwanamke na ameamua kumpora na bint kaamua kwenda kushtak polisi kivingine.HUENDA!!!!!!!!!

Yeah huenda...na kama kweli banda alimnunulia halafu kadi ya gari akaanduka jina la mwanamke alikosea...
 
Back
Top Bottom