Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
Nakumbuka;
Nikiwa mdogo mdogo hivi kuna "BIBI" mmoja alifariki pale kijijini, yule bibi alikuwa anasadikika ni mshirikina "mchawi".
Wakati ulipowadia wa kukaribia kufariki, yaani anakaribia kukata roho, alikuwa akiweweseka sana, wale ndugu zake waliokuwa wakimuuguza walimsikia akiongea maneno kwa lugha ambayo hawakuijua. Siku tatu alikuwa akiongea lugha ya ajabu ajabu, baada ya hapo akaanza kuwataja watu mbalimbali ambao walishafariki.
Huku akitokwa jasho jingi sana, alilia kwa maumivu makali sana akidai watu hao ambao walishafariki wanamuandama, wanamchoma moto. Alikuwa akilia kwa uchungu sana, aliomba asamehewe na kwa madai kwamba hakufanya yeye, hakuwaua yeye.
Kilio na malalamiko yale yale yaliwatokea na wazee wengine ambao walikuwa ni wachawi, kabla ya kukata roho walilia sana na kulalamika sana na muda mwingine kukana kuwaua watu.
Nimekulia unyaturuni, hii hali kwa kinyaturu sijajua huwa inaitwaje lakini naamini wapo wanayoijua vizuri, lakini kuwataja watu wanasema "ODONA" .
Sijui nilitaka kusema nini asubuhi yote hii.
Abdoulquarim Malisa