Abdu Fatah Mussa Mtangazaji wa Radio Tehran Iran

Abdu Fatah Mussa Mtangazaji wa Radio Tehran Iran

ABDU FATAH MUSSA MTANGAZAJI WA RADIO TEHRAN IRAN

Ulikuwa mwaka wa 2000 Uchaguzi Mkuu wa Pili baada ya uchaguzi wa kwanza 1995.

Niko Tanga.

Sikumbuki vipi tulifahamiana lakini ninachokumbuka ni kuwa siku moja wakati wa kampeni za uchaguzi zikiendelea alinipigia simu akaitambulisha Sauti ya Iran na yeye mwenyewe kuniomba anihoji kuhusu siasa za Tanzania.

Huu ukawa ndiyo mwanzo wa usuhuba wetu.

Ikawa mara kwa mara ananipigia simu tunafanya mahojiano na mazungumzo yetu yanarushwa na Radio Tehran Iran.

Mimi sikujua.

Nilikuja kujua baadae sana kuwa namna yangu ya kueleza matokeo ya siasa na historia ya Tanzania ilikuwa tofauti sana na namna wengine walivyokuwa wanaeleza.

Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili inasikilizwa Arabuni ambako kuna wasemaji Kiswahili wengi.

Sasa baada ya mimi kuwa mmoja wa wachambuzi wa siasa kutoka Tanzania vipindi hivi nilivyokuwa nikifanya na Abdul Fatah vikavutia wasikilizaji wengi.

Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili ikapanda chati ikawa iko juu.

Radio nyingine mashuhuri wasikilizaji watasikiliza lakini mwisho watafungua Radio Tehran kusikiliza na wao wana lipi kuhusu taarifa hiyo.

Abdul Fatah ni mtangazaji hodari Mashaallah anayejua kuhoji yale ambayo wewe muhojiwa hukutegemea.

Atakuchukua ngazi baada ya ngazi mnapanda na kila kidato kinazua kisa kipya.

Abdu Fatah anakuwa mwanamasumbwi anaemperemba mpinzani wake amtwange sumbwi litakalomwangusha chini na kumaliza pambano.

Wako wanaoghadhibishwa na maswali chokonozi kipindi kikawaka moto muhojiwa akamaliza hasira zake kwa mtangazaji wakaagana.

Hicho ndicho mtangazaji alichokuwa akikitafuta na kakipata bure kabisa.

Akizima digital yake na kuvua headphones anaangua kicheko cha furaha.

Kapata kipindi burudani kwa wasikilizaji wake.

Milton Obote alimfokea mtangazaji wa BBC na akawakomesha wasimpigie simu tena kumletea upuuzi wao.

Siku hizo mwisho wa uhai wake yuko Zimbabwe.
Abdu Fatah akiniwekea staha lakini akiniangushia makombora mazito.

Miaka ya mwanzo ya vyama vingi toka kurejeshwa siasa za vyama vingi zilikuwa moto hasa Zanzibar.

Uchaguzi wa 1995 CCM Zanzibar ilikuwa imeshindwa uchaguzi na waandishi wengi wakihofu kulieleza hili.

Abdu Fatah ataniperemba kwa upole kabisa kunilainisha tuangalie hali ya baadae ya visiwani.

"Sikiliza Abdu mimi panya sifunzwi kula sufi..."

Atacheka.
Nazungumza na Mswahili tena Mzanzibari.

Keshanifahamu.
Ikawa Radio Tehran inapendeza.

Nilipata mshtuko nilipokutana na Abdu Fatah Tehran akaniambia kuwa yeye shahada yake ni ya Uhandisi.

Huyu ndiye Injinia Abdu Fatah Mussa wa Idhaa ya Kiswahili Radio Iran Tehran.

View attachment 3008452
Abdu Fatah Mussa​
View attachment 3008451
Mzee unetembea Sana aiseeeeee....majiji mengi sana umefika...

Hongera kwa hilo
 
MashAllah!! Siku ukifika Lushoto unishtue ili nikufungashie matunda ya kula na wajukuu zako.
 
Mzee said angekuwa sio mdini angekuwa mtu wa kuigwa na jamii,lakini udini umemwelemea mzee wa watu mpaka hata maandiko yake ni udini mtupu.
Katika maandiko yake msukumo wa kuyaandika huwa ni uislamu kwanza hivyo habari nzima itapindishwa kuelekea kwenye uislamu 😀 😀😀😀 anyway namwelewa mzee anamtetea allah na heri afanye kwa njia hii kuliko zile njia zao nyingine.......
 
Mada zako zote zinashabihiana sana mzee Mohamed,kusudio lako huwa nini hasa!?
 
Katika maandiko yake msukumo wa kuyaandika huwa ni uislamu kwanza hivyo habari nzima itapindishwa kuelekea kwenye uislamu 😀 😀😀😀 anyway namwelewa mzee anamtetea allah na heri afanye kwa njia hii kuliko zile njia zao nyingine.......
Salari,
Nimeweza kuandika kwa kuwa Waislam wanayo historia ambayo wengine hawana.

Nani mwenye historia ya Hassan Omari Makunganya?

Nani mwenye historia ya Mtwa Abdallah Mkwawa?

Nani mwenye historia ya Abdulrauf Songea Mbano?

Nani mwenye historia ya Khadija Mkomanile?

Nani mwenye historia ya Kleist Abdallah Sykes, Schneider Abdillah Plantan?

Hii ni mifano michache katika historia ya Tanganyika.

Kwa nini katika historia ya TANU historia ya Abdulwahid Kleist Sykes haikuweko, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Suleiman Takadir, Rashid Ali Meli, Sheikh Mohamed Yusuf Badi kwa kuwataja wachache.

Vipi kuhusu wanawake katika TANU; Sharifa bint Mzee, Hawa bint Maftah, Zarula bint Abdulrahman, Halima Khamis, Halima Selengia, Nyange bint Chande kwa kuwataja wachache.

Unadhani mimi nimefanya makosa kutafiti na kuandika historia hii?

Hivi unajua kuwa nimepokea nishani tatu kutoka taasisi za Kiislam hadi sasa kwa ajili ya mchango wangu katika kuinusuru historia hii?

Unajua pia hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora miaka miwili mfululizo 2021 na 2022?
 
Mzee,
Kosa si kuandika historia ya watu wako. Shida inakujaga unavyowatweza wengine na kuwapandisha wazee wako wa kimnyema wa hapo Kkoo kana kwamba bila wao uhuru usingepatikana wakati unajua wazi vuguvugu la uhuru lilikuwa kila sehemu ndani ya Tanganyika na Africa kwa ujumla na si wamanyema wa Kkoo. Hapo ndiyo tunapataga shida.
Na afadhari siku hizi umepunguza kusema kuwa mlimfunza Nyerere kuvaa suruali na kumkopesha mafuta ya taa hapo magomeni.
 
James...
Sijui kwa nini unanizulia uongo.

Ningeandika kitabu kisichokuwa na adabu ningekiua kitabu changu.

Mabingwa wa African History John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan wasingetaka kujihusisha na kitabu cha kipuuzi.
 
Tulishajadiliana sana kuhusu wazee wako. Nafkiri unakumbuka. Kama ni kuhusu mafuta ya taa na kaptura za Nyerere nafkiri pia tulishawahi kuwa na mjadala huku ktk Uzi fulani. Kumbuka Mimi Sina shida na wazee wa kariakoo shida yangu ni jinsi wengine wanavyodunishwa ktk makala zako huku jamii unayoitaka ikipewa chapuo.
 
Hawa wakina Sykes wamekula sana neema ya nchi hiii
Kizazi chao kilichobaki inaelekea
Walishondwa kukiendeleza
Mzee said,alipenda sana aone wakina sykes ni watu fulani wakubwa serikalini

Ova
 
Katika maandiko yake msukumo wa kuyaandika huwa ni uislamu kwanza hivyo habari nzima itapindishwa kuelekea kwenye uislamu 😀 😀😀😀 anyway namwelewa mzee anamtetea allah na heri afanye kwa njia hii kuliko zile njia zao nyingine.......
Sykes hajatajwa!
Bufa,
Angalia post #28.

Katika historia ya Tanganyika kuanzia Deutsch Ostafrika baada ya Berlin Conference 1884 hadi kufikia harakati za kudai uhuru kuanzia kuundwa kwa African Association 1929 hadi TANU 1954 lazima utakutana na historia ya Sykes.

Hebu tuitazame historia ya Abushiri bin Salim Al Harith na makamanda wake Jumbe Shomari Jahazi na Makanda Mwinyimkuu.

Wakati wa vita hivi vya Abushiri kiongozi wa askari wa Kizulu chini ya Hermann von Wissmann alikuwa Chief Mohosh Shangaan.

Katika hawa askari wa Kizulu ambao mimi nawajua kwa majina ni Sykes Mbuwane, Chakulan na Machakaomo.

Hawa walipigana na Abushiri na makamanda wake Jahazi na Makanda.

Vitukuu vya hawa niliowataja hapa wako na baadhi mimi nawajua na wananijua.

Jirani ya kwangu yuko Yusuf huyu ni kitukuu cha Abushiri ana duka zuri la kuuza simu na accessories zake na mama yake yu hai.

Wajukuu wa Sykes Mbuwane ni Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes.

Wajukuu wa Chief Mohosh Shangaan (Afande Plantan) ni Bi. Maunda Plantan ambae mimi namwita mama.

Mjukuu wa Machakaomo ni Biti Hassan ambae kwangu pia ni mama na kaniona nikizaliwa Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) mwaka wa 1952 na kaniona hadi utu uzima.

Biti Hassan kafariki kiasi cha miaka 10 iliyopita na nyumba yake aliyorithi kutoka kwa baba yake Hassan Machakaomo ipo hadi leo hapo Mtaa wa Sykes.

Nyumba ya Machakaomo ipo hadi leo hapo mtaani.

Narudia kukuekeza kuwa hawa babu zao Wazulu ndiyo walisimama upande wa jeshi la Wajerumani likiongozwa na Hermann von Wissmann kupigana na Abushiri bin Salim na makamanda wake Makanda Mwinyimkuu na Jumbe Shomari Jahazi.

Kitukuu cha Chief Mohosh Shangaan, Mzee Khamis Salum mimi ananiita kaka na ni mtoto wa Bi. Maunda Plantan.

Mzee analijua lilipo kaburi la babu yake mkuu Chief Mohosh Shangaan na ameniahidi kunipeleka nilione pale Makaburi ya Ilala karibu na Karume Stadium.

Vitukuu vya Sykes Mbuwane wapo Dar es Salaam na wao wana watoto na wote wanaijua historia yao.

Maarufu katika hawa vitukuu ni Aisha "Daisy" Sykes (aliyeandika historia ya babu yake Kleist Sykes na ndiyo hii leo tunaisoma) na mdogo wake marehemu Kleist Sykes aliyekuwa Mayor wa Dar-es-Salaam.

Umefanya haraka kusema kuwa Sykes sikuwataja.

1717717960236.jpeg

Mwandishi ameshika Medali ya Mwenge wa Uhuru ya Abdul Sykes na vitukuu vya Sykes Mbuwane​
 
Ingekuwa mimi natangaza Uislam nisingeadhimishwa hapa JF mara mbili kama Mwandishi Bora.

Nisingealikwa kwenye vyuo maarufu Marekani na Ulaya.

Nisingealikwa kuzungumza VoA, BBC, DW, SABC, TBC, ITV, AZAM na vituo vingi vingine.
Subiri usifiwe we mzee, sio kila siku sijui wapi sijui wapi blaah blaah,Abdul Sykes, kipata,k,koo ,Mwl Nyerere alikaribishwa na wasilamu laalaa,leele.
Hadithi ni hizo tu?
 
Back
Top Bottom