Abdul ana nondo, asema uchaguzi serikali za mtaa haupaswi kuendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Akizungumza na Clouds Media, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema wao kama chama hawakubaliani na sheria TAMISEMI kuendelea kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa.

Ameongeza kuwa tunapotaka Haki ya Uchaguzi, Uchaguzi wa uhuru na haki hatuwezi kuendelea endapo Ofisi ya TAMISEMI ambayo kimsingi ni Ofisi ya Rais na Waziri ndiye anayepewa mamlaka ya kusimami uchaguzi basi huo uhuru unaotakiwa hauwezi kuwepo. Tunaweza kubaki tunategemea UTASHI lakini hatujui huo utashi atakaokuja nao kesho utakuwa wa namna gani.

Hivyo ameshauri mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wapewe Tume ya Uchaguzi. Sheria ya TAMISEMI ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa isiwepo kabisa, kuwepo na sheria moja ya UCHAGUZI ambayo itakuwa sheria moja inayosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Udiwani, Ubunge na Urais

Your browser is not able to display this video.
 
Akizungumza na Clouds FM, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema wao kama chama hawakubaliani na sheria TAMISEMI kuendelea kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa.
Huyu atatimuliwa sasa hivi ACT Wazalendo, maana amekuwa anatoa matamko yanayoipinga serikali
 
Huyo kijana yuko sahihi na anayo hoja ya msingi.

Sijui kama 'consultant' ZZK anakubaliana na hilo 🤣
 
Ana hoja, sema ndio hivo hakuna atalae kubali, CCM waroho
 
Kwani zito anasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…