Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Kiswahili cha Wazanzibar hakieleweki na Wabara maarufu siku hizi kama Watanganyika. Kuugua kwao itakuwa inamaanisha hadi kulazwa. Sisi watanganyika hata ukipatwa na mafua kidogo tu ya kutoa kamasi, tunasema kuugua.Akitoa salaam za familia, mtoto wa mzee Ali Hassan Mwinyi, Abdul Mwinyi amesema baba yao hajawahi kuugua katika kipindi chote cha uhai wake. Kaanza kuugua kwa mara ya kwanza miaka 2 iliyopita.
Hakika mzee Mwinyi ni somo zuuri.
Mungu amrehemu.