DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Abdul Nondo, amelaani vikali vifo vya wananchi waliouawa kwa risasi wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini, akisema kuwa hakuna sheria inayoidhinisha mtu kuuawa kwa kutokana na kile alichokitaja ‘kuandamana bila kibali’.
Akizungumza na wanahabari leo, Novemba 12, 2025, jijini Dar es Salaam, Nondo amejibu hoja zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida, waliodai kuwa maandamano hayo yalifanyika kinyume cha taratibu.
Ameeleza kuwa vitendo vya mauaji nje ya utaratibu wa kisheria vinapaswa kukemewa na jamii nzima, akibainisha kuwa sheria zipo wazi kuhusu namna ya kushughulikia makosa ya aina hiyo.
“Kanuni ya adhabu kifungu cha 77 kinataja mtu anayetuhumiwa kushiriki mkusanyiko usio halali au ghasia anatenda kosa na adhabu yake akikutwa ni hatia ya kifungo cha mwaka mmoja, kwanini kama walikuwa hawana kibali wasikamatwe kupelekwa mahakamani kushtakiwa ili sheria ipate mkondo wake?”, amehoji.