Abdul Nondo: Kauli ya Nchimbi kuhusu Katiba Mpya ni hadaa za Serikali kwa Umma

Abdul Nondo: Kauli ya Nchimbi kuhusu Katiba Mpya ni hadaa za Serikali kwa Umma

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
753
Reaction score
1,699
Abdul nondo anasema.....

1785067397635.jpeg
1785067489605.jpeg

Ngome ya vijana ACT wazalendo tumesikia kauli ya Makamu wa Rais Dkt.Emmanuel John Nchimbi aliyoitoa tarehe 24/Julai/2026 kuhusu hoja ya KATIBA MPYA. Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel John Nchimbi anasema serikali inataka KATIBA MPYA, Rais Samia anataka KATIBA MPYA na CCM pia inataka KATIBA MPYA na ndio maana wameiweka kwenye ilani ya CCM ya 2025 alafu mwisho anamalizia akituambia “PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA,KOMAENI HAPO”.

Kauli hii ya Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni kauli yenye utata,inayohitaji kuhojiwa na sio kupigiwa makofi. Kifalsafa hii ni kauli inayokinzana na kanuni ya kimantiki “Rules of Logic au Law of non-contradiction inayoasema “X haiwezi kuwa X na isiwe X kwa wakati mmoja” (X cannot be X and be X simultaneously or at the same time). Ni lazima X hiyo iwe na sifa moja aidha iwe sio X, au iwe ni X haiwezi kuwa na sifa mbili kwa wakati mmoja.

Huwezi kusema CCM wanataka katiba mpya ,Rais anataka katiba Mpya na Serikali inataka katiba mpya alafu wakati huo huo unasema “PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA”, tafakuri ya kimantiki inakataa. Dkt. Emmanuel John Nchimbi anasema tupambane tupambane na nani ikiwa anasema Rais anataka katiba Mpya, tupambane na nani ikiwa anasema CCM inataka katiba Mpya, tupambane na nani ikiwa anasema serikali inataka katiba mpya, tupambane na nani ikiwa wananchi wote na makundi yote tunataka katiba Mpya nani anazuia hadi wananchi tupambane? Kauli ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi ni kauli tata, ni kauli isiyo na muunganiko wa kifikra, ni kauli isiyo na mtiririko wa kimantiki.

Pia soma
Ni kauli inayoashiria muendelezo wa hadaa za serikali na chama cha mapinduzi (CCM) kufanya suala la katiba mpya kama ajenda ya kisiasa ya kuhada umma. Dkt. Emmanuel Nchimbi hapaswi kujitenga na serikali ya CCM, yeye alikuwa mgombea mwenza wa Urais kupitia CCM kwenye uchaguzi wa 2025 alizunguka nchi nzima yeye na Mgombea wa CCM Rais Samia wakiahidi na kunadi pamoja kuhuisha mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa kwanini leo kauli ibadilike na kutuambia TUPAMBANE kwahiyo waliahidi wasichoweza kukitekeleza? Kwamba ahadi ya Katiba Mpya kwenye kampeni ilikuwa hadaa? Kwanini tuambiwe tupambane kwa jambo ambalo CCM, Serikali na Rais wanalitaka?

Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977 ibara ya 47 (1) inasema “Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu Mambo yote ya Jamhuri ya Muungano.
  1. Atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa mambo ya Muungano.
  2. Atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais.
  3. Atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Makamu wa Rais pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM, Makamu wa Rais pia ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri huyu ni kiongozi wa pili wa kiserikali baada ya Rais, vyovyote vile kauli ya Makamu wa Rais ni kauli ya serikali.
Kwa mantiki hii katika dhana ya uwajibikaji wa pamoja (Government /Collective Responsibility), hatuwezi kumtenganisha Dkt. Emmanuel Nchimbi na Serikali, hatuwezi mtenganisha Dkt. Emmanuel Nchimbi na CCM na hatuwezi mtenganisha Dkt.Emmanuel Nchimbi na Rais Samia sababu ni Ofisi moja. Hivyo, kauli hii ya Makamu wa Rais Dkt.Emmanuel John Nchimbi (Ofisi ya Rais) kutuambia tupambane ina tafsiri ya kwamba CCM, Serikali, Rais na wasaidizi wake wote na yeye mwenyewe Dkt.Emmanuel Nchimbi kama makamu wa Rais hawana dhamira ya dhati ya kuhuisha mchakato wa katiba mpya ndio maana tunaambiwa “PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA”.

Na hii inaashiria hata waliyoahidi katika Ilani ya CCM 2025 ukurasa wa 32 aya ya 47(ii) kuhuisha na kuendeleza mchakato wa katiba mpya ni hadaa na hata matamko ya kiserikali na tume mbalimbali kuhusu hitaji la mchakato wa katiba mpya ni hadaa. Na ndio maana hadi sasa hakuna bajeti ya serikali iliyotengwa kwa ajili ya mchakato wa katiba mpya wala hakuna hata ratiba ya utekelezaji wa mchakato wa katiba hadi sasa na kauli za viongozi wa serikali na CCM za siku zote zinaonesha wazi kutokuwa na dhamira ya dhati, mfano Kauli za Makamu Mwenyekiti ndug.Stephen Wasira.

Serikali yenye dhamira ya dhati ingeonesha kwa vitendo na sio matamshi ya kisiasa na hadaa katika majukwaa. Serikali yenye dhamira ya dhati kupitia Makamu wa Rais tungepata kusikia majibu kutoka kwake kwaniaba ya Rais au Serikali kwamba utekelezaji wa ahadi yao kwenye ilani ya kuhuisha mchakato wa katiba mpya kama hitaji la msingi la sasa la wananchi yeye akiwa kama mgombea mwenza wa Urais wa CCM 2025 na sasa Makamu wa Rais wamefikia wapi katika utekelezaji. Kauli za kutuambia TUPAMBANE ni hadaa na kuashiria ukosefu wa dhamira ya dhati kwa serikali yote na CCM kwa ujumla.

Kama ni kupambana watanzania wamepambana tangu 1991, Mwaka 1991 Tume ya Jaji Nyalali chini ya utawala wa Ali Hassan Mwinyi ilipendekeza katiba mpya ila CCM na serikali yake ilikataa, Tume ya Jaji Robert Kisanga 1998 wakati wa utawala wa Benjamini W. Mkapa ilipendekeza kupatikana kwa katiba Mpya ila CCM na serikali yake ilikataa, Kamati ya Jaji Mark Bomani mwaka 2003 ilipendekeza pia kupatikana kwa katiba Mpya ila CCM na serikali yake walikataa.

Tume ya Jaji Sinde Warioba ikafanya kazi kubwa hadi kutengeneza Rasimu baada ya kukusanya maoni nchi nzima wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete 2013 ila hatimaye mchakato huo ukaenda kuuliwa na kuzikwa katika Bunge la katiba baada ya CCM kuingiza maslahi yao binafsi na kutumia wingi wao kuharibu mchakato (Tyranny of the majority ), Kikosi kazi cha Prof. Mukandala 2022 kilipendekeza katiba Mpya ila CCM na Serikali yake bado hawaoneshi dhamira, Tume ya haki Jinai ya Jaji Chande 2023 ilipendekeza katiba Mpya na pia Tume ya kuchunguza matukio baada ya uchaguzi 2025 chini ya Jaji Chande pia ilipendekeza suala la katiba mpya baada ya damu kumwagika na watanzania kupoteza maisha ila CCM na serikali yake bado haioneshi dhamira ya dhati katika hili.

Kupambana kwa namna gani serikali kupitia Makamu wa Rais Dkt. Emmanael Nchimbi anataka tupambane, watu wamepambana na wanapambana ila huishia maumivu na madhila makubwa.

Kwa mantiki hii, Ngome ya vijana ACT wazalendo tunatoa raia kwa vijana wenzetu nchini, vyama vya siasa, viongozi wa dini, Asasi za kiraia, wanaharakati na wananchi wote kwamba hatupaswi kuyumbishwa na hadaa za CCM na serikali yake, kwani wanaonesha kutokuwa na dhamira ya dhati ya kuhuisha mchakato wa katiba mpya. Ni wajibu wetu kuunganisha nguvu kwa umoja wetu bila kuchoka kulazimisha na kuhimiza serikali kuanza mchakato wa katiba mpya sasa.

Katiba mpya haitapatikana kwa kauli tamu tuu za majukwaani sababu kauli tamu za majukwaani zimekuwepo kwa muda mrefu, bali katiba mpya itapatikana kwa dhamira ya kweli na ya vitendo ya viongozi waliopo madarakani, ushiriki wa vyama vyote kwa umoja wetu bila kujali tofauti ya itikadi zetu, Asasi za kiraia, vijana, viongozi wa dini ,wanaharakati na wananchi wote kwa umoja wetu madhubuti katika kuungana pamoja kuhakikisha mchakato wa katiba mpya unaanza, unafanyika kwa uwazi, ushirikishwaji na kwa nia ya kujenga Taifa lenye Demokrasia imara.

Sisi Ngome ya vijana tunaamini bado hatujachelewa, tunapendekeza hatua hizi kuafuatwa kuelekea kuliponya Taifa.

1) Mwenyekiti wa CHADEMA Wakili Tundu Antiphas Mughwai Lissu achiwe sababu kesi yake ni kisiasa.

2) Uwajibikaji kwa yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

3) Kufuta kesi za kigaidi dhidi ya vijana mbalimbali, viongozi wa vyama na wananchi pamoja na wahadhiri.

4) Kutumia wapatanishi kutoka umoja wa Afrika au Jumuiya ya SADC katika kufanya mazungumzo ya namna ya kwenda mbele kutokana na mkwamo uliopo ikiwa ni pamoja na kuhuisha mchakato wa katiba mpya. Hii itajenga kuaminiana na kusonga mbele.

5) Ratiba ya utekelezaji wa mchakato wa katiba mpya itolewe, iwe wazi. Mchakato utawaliwe na dhamira ya kweli, nia thabiti kwa maslahi na mustakabali wa Taifa letu ili kupata katiba bora itakayoimarisha uwajibikaji, Demokrasia kwa ujumla, chaguzi huru na haki, utawala wa sheria, kulinda haki za watu na kujenga taasisi imara na Madhubuti.

Hatua hizi zitarejesha matumaini na mwanzo mzuri wa kuaminiana kwa makundi yote kama njia pekee ya kwenda mbele na kuliponya Taifa letu.

===========

My take

Ila ACT Wazalendo mnapata wapi hiyo nguvu ya kukosoa CCM wakati wote ni wale wale? Mnawapiga vita lakini mmekubali kuwa miongoni mwao? Hata mtu mjinga hapotezi muda na nyie hata kama mmeongea point sababu mmeshapoteza legitimacy the moment mlikubali kushiriki uchaguzi huo hata baada ya kuona dalili zote kuwa ni upuuzi, na mkatumaliza zaidi mlipokubali viti mlivyopatiwa.

Yaani mtasema nini ili Watanganyika tuwaelewe? Labda muachie siti zenu zote na kuvunja hayo maridhiano ya kipuuzi. Watu wameua ndugu zenu halafu leo mnasema tusonge mbele bila yoyote kuwajibika. Msitupandishe visukari bana, mkae na mabwana zenu kimya na njia mliyoichagua, siku ya hukumu wote mtalipia.
 
Sasa wewe Nondo kwanini tusikuone au tusikuite kuwa ni msaliti wa huyo Nchimbi maana ndiyo chama chenu hicho
 
Sasa bwana nondo hayo unayozungumza mlitakiwa mzungumze kwenye vikao vyenu vya familia nyie si ndugu wa damu kabisa?
 
Back
Top Bottom