Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo akiongea na wanahabari leo, amesema kuwa baada ya kutekwa na kuteswa na baadaye kutelekezwa Coco beach wilaya ya Kinondoni, alipewa masharti kadhaa ambayo aliambiwa kama hatayatimiza basi atauawa.
Walioniteka awalikuwa wakiniambia mimi nina mdomo, na waliponiacha Coco beach walinipa masharti ya kwamba
1. Tukikuacha usieleze chochote kuhusu kutekwa kwako, nikitoka pale niende nikae kimya.
2. Nisiongee na vyombo vya habari
3. Nisiendelee na mdomo wangu wa kuongea ongea na kuandika andika mtandaoni
4. Nikitoka pale wanaponiacha, basi moja kwa moja niende nyumbani kabisa nikapumzike ili nikiamka asubuhi taarifa zivume kuwa Nondo kapatikana akiwa kwake amelala ili vyombo vya mamlaka vipate kusema tukio hili limetengenezwa ni uongo kwamba mtu unawezaje kutekwa halafu ukaenda nyumbani kulala.
Masharti yote hayo waliyonipa nimeyavunja, sijatii hata sharti moja.