Abdul Nondo: Masharti yote niliyopewa na watekaji nimeyavunja, vyombo vya mamlaka vilitaka viseme ni tukio la kutengeneza

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo akiongea na wanahabari leo, amesema kuwa baada ya kutekwa na kuteswa na baadaye kutelekezwa Coco beach wilaya ya Kinondoni, alipewa masharti kadhaa ambayo aliambiwa kama hatayatimiza basi atauawa.

Walioniteka awalikuwa wakiniambia mimi nina mdomo, na waliponiacha Coco beach walinipa masharti ya kwamba

1. Tukikuacha usieleze chochote kuhusu kutekwa kwako, nikitoka pale niende nikae kimya.
2. Nisiongee na vyombo vya habari
3. Nisiendelee na mdomo wangu wa kuongea ongea na kuandika andika mtandaoni
4. Nikitoka pale wanaponiacha, basi moja kwa moja niende nyumbani kabisa nikapumzike ili nikiamka asubuhi taarifa zivume kuwa Nondo kapatikana akiwa kwake amelala ili vyombo vya mamlaka vipate kusema tukio hili limetengenezwa ni uongo kwamba mtu unawezaje kutekwa halafu ukaenda nyumbani kulala.

Masharti yote hayo waliyonipa nimeyavunja, sijatii hata sharti moja.
 
Walioniteka awalikuwa wakiniambia mimi nina mdomo, na waliponiacha Coco beach walinipa masharti ya kwamba tukikuacha usieleze chochote kuhusu kutekwa kwako, nikitoka pale niende nikae kimya. Nisiongee na vyombo vya habari, nisiendelee na mdomo wangu wa kuongea ongea na kuandika andika mtandaoni, na nikitoka pale wanaponiacha, basi moja kwa moja niende nyumbani kabisa nikapumzike ili nikiamka asubuhi taarifa zivume kuwa Nondo kapatikana akiwa kwake amelala ili vyombo vya mamlaka vipate kusema tukio hili limetengenezwa ni uongo kwamba mtu unawezaje kutekwa halafu ukaenda nyumbani kulala.

Masharti yote hayo waliyonipa nimeyavunja, sijatii hata sharti moja.
Wamvunje mguu then aende nyumbani kwamba hakuna kilichotokea
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo akiongea na wanahabari leo, amesema kuwa baada ya kutekwa na kuteswa na baadaye kutelekezwa Coco beach wilaya ya Kinondoni, alipewa masharti kadhaa ambayo aliambiwa kama hatayatimiza basi atauawa.

Walioniteka awalikuwa wakiniambia mimi nina mdomo, na waliponiacha Coco beach walinipa masharti ya kwamba

1. Tukikuacha usieleze chochote kuhusu kutekwa kwako, nikitoka pale niende nikae kimya.
2. Nisiongee na vyombo vya habari
3. Nisiendelee na mdomo wangu wa kuongea ongea na kuandika andika mtandaoni
4. Nikitoka pale wanaponiacha, basi moja kwa moja niende nyumbani kabisa nikapumzike ili nikiamka asubuhi taarifa zivume kuwa Nondo kapatikana akiwa kwake amelala ili vyombo vya mamlaka vipate kusema tukio hili limetengenezwa ni uongo kwamba mtu unawezaje kutekwa halafu ukaenda nyumbani kulala.

Masharti yote hayo waliyonipa nimeyavunja, sijatii hata sharti moja.
Huyu naye watamuua kama yule kijana aliyechana picha
 
Vipi wakianza kurusha zile clip za .....? Nondo atavumilia??
 
Hawa wajinga kama imeshindikana kuungana ili watuachie nchi yetu, basi kila mtu awe anamalizana nao kivyake.
 
Huu utawala wa mama umekuwa wa kijinga na kishamba sana.Yaani mtu akiongea ukweli wanawatuma askari wao wawaue watanzania wanaoyasema maovu Yao.Halafu Kuna wajinga na wapumbavu wanasema eti 2025 agombee Tena!Hatutakubali huu ujinga
 
Ndio maana wengine tumeamua kupenda mpira
Hao kina Soka na kibao walipewa masharti gani!?maana hadi Leo hawapo
 
Hii ni clue muhimu sana kwa wenzetu wanaotekwa na kisha kupatikana kwa sangoma, michepuko, hotelini na hata wanaokaa kimya kana kwamba hakuna lililotokea (kwa mfano Mo) kumbe wanatii maagizo bila shuruti.

Big up kwa ujasiri wako Mr. Nondo, hakuna kuogopa.
 
Ndio maana wengine tumeamua kupenda mpira
Hao kina Soka na kibao walipewa masharti gani!?maana hadi Leo hawapo
MImi nilijua Abdul Nondo kakosea kitu kikubwa sana. Kumbe ni kuongea ongea tu tena hawajataja hata aliongea nini
 
Afadhali yeye Nondo karudi kuja kuhadithia, akina Deusdith Soka na wenzake na yule dogo aliyechoma picha ya Malikia wale imeonekana wauawe.☹️

Ninachokiona hapa ni kwamba hukumu ya kifo nje ya mahakama inawalenga zaidi wana CHADEMA kuliko vyama vingine halafu Mbowe anataka siasa za kistaarabu.
 
Back
Top Bottom