Hatuhitaji upinzani wowote tu ilimradi bungeni, tunahitaji upinzani wa maana na wenye mantiki.Mwenyekiti wa Taifa wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Abdul Nondo, amesema kuwa watu wanaowahamasisha wananchi kutoshiriki kupiga kura wanakipa nguvu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu hatua hiyo huongeza nafasi ya chama tawala kuendelea kulitawala bunge bila ushindani.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana Julai 1, 2025 katika eneo la Kalinzi, Jimbo la Kigoma Kaskazini, Nondo alisema:
“Unapowahamasisha watu wasishiriki uchaguzi, kwa maana nyingine unaipa CCM nguvu ya kulitawala Bunge bila upinzani wowote. Wanaoeneza wazo la kususia wanatumikia mfumo tunaoupinga.”
Mwenyekiti huyo wa vijana alisisitiza kuwa ACT Wazalendo haitokimbia uchaguzi, hata kama mchakato wa uchaguzi huo umejaa dosari. Alisema chama hicho kimeamua kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili “kuwanyang’anya wahuni silaha zao kwa kuingia ulingoni na kuwashinda.”
“Tunasema tunakwenda kwenye uchaguzi wa kihuni kuzuia uhuni. Kususa hakuzuii udhalimu, bali kunautengenezea nafasi,” aliongeza Nondo.
View attachment 3391194
Chanzo:Nipashe
Kwani uchaguzi wa mwaka jana ulikuwaje?“Tunasema tunakwenda kwenye uchaguzi wa kihuni kuzuia uhuni. Kususa hakuzuii udhalimu, bali kunautengenezea nafasi,” aliongeza Nondo.
Nendeni mkashiriki, ila mkipigwa za USO mkatafute pa kupigia kelele. Tunaamini mtarudi hapa baada ya miezi mitatu, November mwanzoni kupiga kelele. Hamtasikilizwa. Ninaamini watz watawazodoa. Lakini kwa kuwa ni maamuzi yenu hakuna wa kuwazuia maana KATIBA ya nchi imewapa fursa ya kuamua mlitakaloMwenyekiti wa Taifa wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Abdul Nondo, amesema kuwa watu wanaowahamasisha wananchi kutoshiriki kupiga kura wanakipa nguvu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu hatua hiyo huongeza nafasi ya chama tawala kuendelea kulitawala bunge bila ushindani.