GE2025 Abdulhabib Mwanyemba: Waliotaka kupora urais wa Samia tunawajua walipojificha

GE2025 Abdulhabib Mwanyemba: Waliotaka kupora urais wa Samia tunawajua walipojificha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Huu ni ukweli mchungu najua mnajua ila mlokuwa mnatikisa kiberiti.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, amelaani vikali kile alichokiita juhudi za watu wachache wenye nia ya kukwamisha misingi, tamaduni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kueneza na kuhamasisha usaliti ndani ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi Julai 26, 2025, ofisini kwake mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa chama kwa njia ya mtandao (Zoom Meeting), uliofanyika jijini Dodoma, Mwanyemba amesema kuwa UVCCM haitavumilia vitendo hivyo vinavyolenga kuhujumu uhai na mshikamano wa chama.

Ameongeza kuwa UVCCM haitakubali kuona watu hao wakiendelea kusambaza chuki na uchochezi, na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za chama.

Aidha, amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kufanikisha mkutano kwa njia ya kidijiti, akisema ni hatua kubwa ya kimaendeleo na kidemokrasia inayoendana na mabadiliko ya teknolojia duniani.
 
Tatizo ni kwamba, miguno na malalamiko yamekuwa mengi kwenye jamii. Hata hiyo system inatakiwa kuona msimamo wa watawaliwa. Pia mtia Nia pia anatakiwa kusoma na kunusa upepo. Kwa maoni yangu upepo naona unaovuma ni mbaya ( Kusi)
 
Mkiwamaliza chadema mtauwana wenyewe Kwa wenyewe utabiri unatimia. Chadema mnadhani mmewamudu Sasa mnaanza kutafutana wenyewe Kwa wenyewe.
 
Namuomba mama amuachie Baraba atupatie Pole pole tumshughulikie.

Kama mwanaume atoke hadharani aongee, anajificha kwa ninj?
 
Back
Top Bottom