Abdulkarim Karimjee

Abdulkarim Karimjee

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
0802b3c67710ceec309f1b47432d4546.jpg

Abdulkarim Karimjee (kushoto) akiwa na afisa raia wa uimgereza

UKUMBI wa bunge uliokuwa unatumika jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma unaitwa Karimjee Hall. Kwa kifupi, majina hayo yanatokana na familia ya Karimjee ya Madhehebu ya Bohra, iliyoongozwa na Jivanjee Budhabhoy mwaka 1825, iliyotoka huko Cutch Mandvi, India na kuja Afrika Mashariki na hatimaye kuishi Zanzibar.
Si hivyo tu, familia hiyo ndiyo iliyoutoa ukumbi huo utumike kuwa bunge la Tanganyika.

Ilikuwa ni familia ya wafanyabiashara iliyohamia baadaye Dar es Salaam, Tanganyika, ikapanua biashara zake nchini na nje ikiwa inajulikana kama Karimjee Jivanjee & Co Ltd ikijikita katika biashara za kilimo, viwanda na kadhalika.

be3eae99a0b93d52273ac77a3662d1ab.jpg

Abdulkarim akiwa Bungeni
Ukumbi huo ulipewa jina la mjukuu wa Jivanjee aliyeitwa Abdulkarim Yusufali Alibhai Karimjee aliyekuwa spika wa kwanza Mtanganyika tangu Januari 1, 1956 hadi Desemba 26, 1962 wakati Tanganyika ilipokuwa imepata uhuru. Abdulkarim aliyezaliwa 1906 na kufariki 1977, pia alikuwa Naibu Meya wa Dar es Salaam mwaka 1952 na 1956 akawa meya kamili wa jiji hilo.

Wakati wa uhuru yeye ndiye aliyeendesha shughuli zote za bunge na akawa mbunge kamili wa kuchaguliwa badala ya mbunge wa kuteuliwa. Mwaka 1960 hadi 1970 alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo nchini (NDC) na Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) na ndiye aliyeasisi Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Hiyo ndiyo familia ya Karimjee iliyokuwa maarufu si kwa biashara tu, bali kwa kutoa misaada mbalimbali ya kusaidia watu wengine, hususan maskini. Ilikuwa pia familia iliyopendwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa msimamo huo.
 
KJ Motors ilianzishwa na ukoo huohuo wa Karimjee Jeevanjee, na waliwasomesha Watanzania wa Kwanza nchini Japan mwanzoni mwa miaka ya sitini ili kujenga uwezo wa watanzania katika fani za urekebishaji magari yenye hitilafu (mechanical engineering) Ila ni historia iliyosahaulika. Wapo waasia waliokuwa na moyo wa kizalendo kuliko baada ya "wenzetu" waliotufikisha tulipo hii leo!!!
pongezi kwako mtoa mada.
 
Historia Nzuri hii. Vp wafanyabiashara wetu wa sasa watakumbukwa kwa lipi miaka ijayo?
Na hawa wafanyabiashara wenye asili ya India wanaiga nini cha kupendeza toka familia ya Karimjee?
 
Nasikia hiyo familia ndio yenye mkataba wa kudumu na serikali kuleta mashangingi toka Japan na kwingineko...
 
nilitarajia kitu kama hicho, hawa jamaa ukiona mahali wametoa msaada ujue kuna mahali wanaingiza
 
Na pale downtown Nairobi kuna eneo maarufu la bustani linaitwa JIVANJEE GARDEN.. je, ndo haohao ?
 
0802b3c67710ceec309f1b47432d4546.jpg

Abdulkarim Karimjee (kushoto) akiwa na afisa raia wa uimgereza

UKUMBI wa bunge uliokuwa unatumika jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma unaitwa Karimjee Hall. Kwa kifupi, majina hayo yanatokana na familia ya Karimjee ya Madhehebu ya Bohra, iliyoongozwa na Jivanjee Budhabhoy mwaka 1825, iliyotoka huko Cutch Mandvi, India na kuja Afrika Mashariki na hatimaye kuishi Zanzibar.
Si hivyo tu, familia hiyo ndiyo iliyoutoa ukumbi huo utumike kuwa bunge la Tanganyika.

Ilikuwa ni familia ya wafanyabiashara iliyohamia baadaye Dar es Salaam, Tanganyika, ikapanua biashara zake nchini na nje ikiwa inajulikana kama Karimjee Jivanjee & Co Ltd ikijikita katika biashara za kilimo, viwanda na kadhalika.

be3eae99a0b93d52273ac77a3662d1ab.jpg

Abdulkarim akiwa Bungeni
Ukumbi huo ulipewa jina la mjukuu wa Jivanjee aliyeitwa Abdulkarim Yusufali Alibhai Karimjee aliyekuwa spika wa kwanza Mtanganyika tangu Januari 1, 1956 hadi Desemba 26, 1962 wakati Tanganyika ilipokuwa imepata uhuru. Abdulkarim aliyezaliwa 1906 na kufariki 1977, pia alikuwa Naibu Meya wa Dar es Salaam mwaka 1952 na 1956 akawa meya kamili wa jiji hilo.

Wakati wa uhuru yeye ndiye aliyeendesha shughuli zote za bunge na akawa mbunge kamili wa kuchaguliwa badala ya mbunge wa kuteuliwa. Mwaka 1960 hadi 1970 alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo nchini (NDC) na Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) na ndiye aliyeasisi Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Hiyo ndiyo familia ya Karimjee iliyokuwa maarufu si kwa biashara tu, bali kwa kutoa misaada mbalimbali ya kusaidia watu wengine, hususan maskini. Ilikuwa pia familia iliyopendwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa msimamo huo.
Ndiyo wenye TOYOTA TANZANIA LIMITED
 
Na pale downtown Nairobi kuna eneo maarufu la bustani linaitwa JIVANJEE GARDEN.. je, ndo haohao ?
Na huko jijini Tanga kuna Karimjee Jivanjee secondary school (Usagara secondary school). Vile vile hulo jijini Tanga kuna jumba la Karimjee Jivanjee sisal estates....Tanga kunani......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom