Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #21
JK,..hizo sentensi mbili kwa kweli zimenifurahisha sana.
..zimenifurahisha kwasababu umeweza kueleza jambo kubwa kwa maneno machache, lakini kwa msisitizo mkubwa.
..nimerudia kusoma sentensi hizo tena na tena nikifurahia umahiri wako wa kucheza na maneno.
..THANK YOU!!
Mzaramo,Mzee wetu katika ubora wake ALLAH akuweke ewe uwe hazina ya vizazi vyetu kwa minakasha hii uiwekayo hapa jamvini Wallah.
ALLAH AKULIPE KHEYR.
Superbug,Huyu mzee mnamuonea sana kumuita mdini. Pia nadhani akiandika kitabu kitauzika sana kutokana na lugha yake na mambo mengi ayajuayo ni first hand informàtion.
Rodrick...Ulipozungumzia mafia nilikuwa nasubiri kusikia historia yao maana Zanzibar wanadai ile nisehemu yao
MashaallahNgongo,
Mimi si ustadhi wala sina uhusiano wowote na Mtaa wa Tandamti.
Nimeishi miaka mingi ya maisha yangu Masaki, Msasani Peninsular na anuani yangu ya Dar es Salaam ndivyo inavyoonyesha hadi sasa.
Hapo ndipo kwetu.
Ningeshukuru sana kama ningejaaliwa nikawa ustadh lakini kuwa ustadh kunahitaji ilm ambayo mie sina.
Mwanangu sasa mtu mzima ananambia,"Baba nikiona tabu sana kukuona wewe unasali nyuma yangu mie mwanao ndiyo imam naongoza sala."
Mie humjibu nikamwambia, "Ndiyo ujue faida ya ilm mimi baba yako nimekuwa chini wewe umekuwa juu sababu ni hiyo ilm ambayo mimi sina; ni hiyo Qur'an uliyohifadhi ndiyo imekunyanyua wewe. Hawawi sawa mwenye kujua na asiyejua."
Ningependa sana kuwa ustadh lakini kunahitaji ilm kuwa ustadh hakuji kirahisi upinde mgongo kwa walimu usomeshwe vitabu na vitabu.
Hakika ningependa kuwa ustadh.
Nilichoambulia ni passages and passages za William Shakespeare, Charles Dickens...
Ngongo unaponiita ustadh ilm niitakayo lakini sina unatonesha kidonda.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mnga'ato,
Allah ndiyo kauli yake katika Qur'an kuwa Muislam nduguye Muislam.
Aya inaendelea kueleza kupatanisha baina ya ndugu waliogombana.
Sikumbuki kichwa cha thread husika, ila nilipata kuandika kwenye hiyo thread ukweli huu uliothibitisha hapa: muislamu wa kweli HAWEZI na hapaswi kuwa rafiki au ndugu wa asie muislamu (especially Wakristo na Wayahudi).
Natamani ungetoa funzo hili siku kwa wale wote waliokuwa wananibishia. Asante sana mzee wetu kwa uthibitisho huu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni madai ya muda mrefu ya wanasiasa wa Zanzibar ila kwa sababu umebahatika kuwa na watu wa huko wanaweza kukupa historia vizuri kama kuna ukweliRodrick...
Hii ni habari mpya kwangu.
Tafadhali nipe taarifa zaidi.
Sent using Jamii Forums mobile app