Abdulrahman Kinana: Kila chama kung'ang'ania Maslahi yake ndo sababu ya Kukwama kwa Katiba Mpya

Abdulrahman Kinana: Kila chama kung'ang'ania Maslahi yake ndo sababu ya Kukwama kwa Katiba Mpya

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Lakini moja ambalo lazima tukiri lilisaidia kukwamisha jambo hili (mchakato wa katiba), ni kwa kila chama kung'ang'ania maslahi yake. Nadhani huo ndiyo ukweli lazima tuseme - Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.

Watu wanakuja na mapendekezo, chama kimoja kinasema ndiyo, kimoja hapana. Wakati mwingine unaangalia zaidi mambo yanayohusiana na namna gani utakuwa madarakani kuliko namna gani wananchi wanafaiduka. Matokeo yake mnabaki kubishana- Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.
20220405_162858.jpg
 
Atajengewa mnara akikubali kutuletea katiba mpya. Comrade ebu amua moja tu tupate Katiba mpya basi!
 
Naona kama Kinana anapotosha, kwanza katiba mpya haikukwama bali Magufuli aligomea hatua ya kura. Ifahamike Ukawa walipojitoa ccm na wajumbe wengine wa bunge la katiba waliendelea hadi kupitisha katiba pendekezwa, na ikawa inasubiri kura za wananchi ili kuwa katiba rasmi.
 
Magufuli?
 
Kuwe na kura ya referendum wananchi wachague maslahi ya chama wanacho kiunga mkono.
sisi wnanchi hatuna mda na ujinga wenu- endeleeni tu kubishana sisi tunahangaika na maisha yetu
 
Back
Top Bottom