Abdulrahman Kinana: Kila chama kung'ang'ania Maslahi yake ndo sababu ya Kukwama kwa Katiba Mpya

Abdulrahman Kinana: Kila chama kung'ang'ania Maslahi yake ndo sababu ya Kukwama kwa Katiba Mpya

Kwani katiba ni ya vyama vya siasa au Ya Wananchi?
Upinzani unataka tume huru itakayoshirikisha wajumbe wa vyama vyote hapa ni kutafuta tu vyeo ' posho na maruprupu ili viongozi wa vyama wapate vyeo na marupurupu tu kwa nini hawasemi tume huru viongozi wake wasiwe na vyama ?

Kwa nini wapiganie viongozi wa vyama vyote washirikishwe ikiwemo tume ya uchaguzi wakati asilimia kubwa ya wapiga kura hawana vyama? Kinana yuko sahihi
 
Kuwe na kura ya referendum wananchi wachague maslahi ya chama wanacho kiunga mkono.
CHADEMA haiwezi kushinda uchaguzi hata ukiwa huru kwa sasa.

Huo ndio UKWELI mchungu.

Nasema hili na Sina maslahi na chama chochote.

CCM bado in mtaji mkubwa wa wapiga kura hasa Wanawake, Wazee.

Na kitu cha hatari Hawa wapiga kura siyo watu wa kelele. Wataamka wataenda kupiga kura, mwisho wa siku utabaki kuwalaani, Mara wamehongwa T-shirt, Mara hawana akili, Mara Elimu ndogo na majina you're mabaya.

Wapiga kura was vyama vya upinzani wengi ni VIJANA OYA OYA ( Mashabiki ) ambao Mara nyingi inategemea wamehamasishwa vipi.
 
Kuchagua sera bora za chama hakuhusiani na kuwa mwanachama wa chama chochote.
Uko sahihi vyama vya upinzani sera hawana

Sera inatakiwa ku cover maeneo yote

Tuanzie na Chadema 2015 walipoweka Lowasa sera yao walisema kipau mbele cha kwanza Elimu, cha pili Elimu,cha Tatu Elimu pana sera hapo?

Haya 2020 Kaja Lisu na sentensi hazieleweki sera yetu Chadema ni maendeleo ya watu sio vitu tungo tata hata haieleweki!! Hata Chadema wengi ukiwauliza hawajui hata ilimaanisha nini kuna sera hapo?
 
Kuwe na kura ya referendum wananchi wachague maslahi ya chama wanacho kiunga mkono.
Nikikumbuka uchafuzi wa mwaka jana, Bora tu hiyo katiba iendelee mpk hapo tutakapokuwa huru kuchagua kuliko kupiga kura afu watu wafanye Yao alafu kuja kupata tena katiba nyingine ni miaka 40 ijayo coz lazma uhuni utafanyika tu
 
Lakini moja ambalo lazima tukiri lilisaidia kukwamisha jambo hili (mchakato wa katiba), ni kwa kila chama kung'ang'ania maslahi yake. Nadhani huo ndiyo ukweli lazima tuseme - Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.

Watu wanakuja na mapendekezo, chama kimoja kinasema ndiyo, kimoja hapana. Wakati mwingine unaangalia zaidi mambo yanayohusiana na namna gani utakuwa madarakani kuliko namna gani wananchi wanafaiduka. Matokeo yake mnabaki kubishana- Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.
View attachment 2176762
Mapendekezo ya tume ya Warioba, yalikuwa ni maoni ya wanamchi na yalikuwa na baraka za vyama na wadau wote except sisiem. Tuache kupindisha mambo, mchakato wa katiba mpya ulikwamishwa na sisiem, period.
 
Kwa nini vyama viwe na washiriki wengi wanaoweza kukwamisha mchakato wa Katiba mpya kwa maslahi ya chama flani? Katiba ni ya maslahi ya wananchi wote si kwa maslahi ya chana flani. Hapa tubatakiwa tujifunze kama nchi muundo wa Bunge uwe na uwakilishi wa aina gani?
 
Mapendekezo ya tume ya Warioba, yalikuwa ni maoni ya wanamchi na yalikuwa na baraka za vyama na wadau wote except sisiem. Tuache kupindisha mambo, mchakato wa katiba mpya ulikwamishwa na sisiem, period.
wananchi wapi- yaani Kigoma na Pemba kuna wanaNchi wengi kuliko jiji la Dar es Salaam? Au Kigoma na Pemba kuna watu wenye uelewa mkubwa kuliko watu walioko Dar? Mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba yalikuwa RUBBISH kama ripoti ya Tume ya madini, makenikia , mto mara na MV Bukoba-
 
Lakini moja ambalo lazima tukiri lilisaidia kukwamisha jambo hili (mchakato wa katiba), ni kwa kila chama kung'ang'ania maslahi yake. Nadhani huo ndiyo ukweli lazima tuseme - Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.

Watu wanakuja na mapendekezo, chama kimoja kinasema ndiyo, kimoja hapana. Wakati mwingine unaangalia zaidi mambo yanayohusiana na namna gani utakuwa madarakani kuliko namna gani wananchi wanafaiduka. Matokeo yake mnabaki kubishana- Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Abdulrahman Kinana.
View attachment 2176762
Good point kwa kweli
 
wananchi wapi- yaani Kigoma na Pemba kuna wanaNchi wengi kuliko jiji la Dar es Salaam? Au Kigoma na Pemba kuna watu wenye uelewa mkubwa kuliko watu walioko Dar? Mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba yalikuwa RUBBISH kama ripoti ya Tume ya madini, makenikia , mto mara na MV Bukoba-
Wewe utakuwa na minyoo mkuu
 
Anawapiga vijembe wenzie. Rasimu ya Waryoba imebeba maslahi na matakwa ya wananchi. CCM wakaibadili rasimu. Wapinzani wakakataa mabadiliko. Ikawa mwisho wa story. CCM wanategemea dhuluma kuendelea kutawala. Uwambie katiba yenye maslahi ya wananchi, wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom