Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ABDULWAHID SYKES NA HISTORIA YA TANU: "WE MZEE!" LUGHA YA DHARAU, KEJELI NA VITISHO''
Baada ya uhuru zilipoanza kauli ya kukashifu TAA na yeye mwenyewe Abdul kuwa hakuwa anaongoza chama cha siasa bali cha starehe mmoja wa marafiki zake aliyekuwa anaumizwa na maneno yale alikuwa Ahmed Rashad Ali.
(In Shaa Allah nitaweka historia ya Ahmed Rashad hapa kwa faida yetu sote).
Ahmed Rashad akawa anamuomba Abdul aeleze historia ya TANU kuanzia jinsi baba yake alivyoanza harakati kupitia African Association mwaka wa 1929.
Abdul Sykes alikataa akimwambia kuwa kama tatizo ni nani kaunda TANU yeye hilo halimshughulishi na hakika Abdul hakufungua kinywa chake hadi anaingia kaburini.
(In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa yale aliyoandika Daisy kuhusu vipi baba yake alikabiliana ni fitna hii katika kipindi hiki).
Nilipokuwa nasafiri kuwatafuta hawa wazalendo ilikuwa tukimaliza mazungumzo nataka kunyanyuka kuondoka wananambia nisubiri tupige fatha, yaani tufanye dua.
Wakisema kuwa hili jambo nililokuwa nalifanya ni kubwa sana linahitaji msaada wa Allah.
Baadhi ya wazee hawa wengi walifariki kabla kitabu hakijatoka na wengine nilibahatika kuwapa nakala ya kitabu kwa mkono wangu ingawa kilikuwa kwa Kiingereza na wasingeweza kukisoma.
Moyoni walikuwa wanasononeka kuwa mchango wao katika kupigania uhuru haukuzaa matunda waliyotegemea.
Leo nafarajika ninaposoma jina la Abdul Sykes lililofutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lilivyorejea na sasa limekuwa maarufu watu wakibishana kuhusu yeye.
Kleist Sykes mtoto wa Abdul Sykes alikuja ofisini kwangu Tanga kunishukuru baada ya baba yake na baba yake mdogo Ally Sykes, kutunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kleist alinipa mkono huku akibubujikwa na machozi.
Leo ninaposoma lugha za "We mzee," lugha za dharau na kejeli na wakati mwingine vitisho dhidi yangu sikasiriki.
Wale wazee waasisi wa TANU walinambia hii kazi niliyoamua kufanya ni nzito.
Daisy anaeleza chokochoko zilizivyoanza karibu ya kupata uhuru na zikaendelea baada ya uhuru:
‘’...uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na ulipopatikana ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.
Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.
Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa na kwenye ngazi nyingi wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.
Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake...’’
Katika kipindi hiki Abdul Sykes alikuwa anatembelea Mercedes Benz 220 SE.
Kijana mwingine Dar es Salaam aliyekuwa na gari kama hii alikuwa kijana wa Kiarabu Abbas Abdulwahab.
Huenda maisha kama haya ndiyo yaliyosababisha hasad na wivu dhidi yake na Abdul alikuwa hata hajafikisha miaka 35.
Kuna msemo wa Kiarabu unaosema kuwa, ''Sababu huondoa ajabu.''
Jibu tunalo kwa nini magazeti TANU ya chama alichoasisi na kukifadhili kwa miaka mingi hayakuweza kumpa Abdul Sykes ile heshima ndogo aliyostahili katika umauti wake.
Kuchapa taazia yake ndani ya magazeti ya Uhuru na The Nationaist na kueleza yale aliyoyafanya kwa Nyerere na TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni kumnyanyua juu katika sifa na heshima isiyo kifani.
Maadui wa Abdul Sykes walitaka jina lake lipotee kabisa katika ramani ya historia ya Tanzania.
Lakini Brendon Grimshaw alipochama taazia ya Abdu Sykes katika Sunday News (20 October, 1968) kichwa cha taazia ile ilikuwa katika wino mweusi uliokoza: ''ABDUL SYKES WAS A TANU PIONEER.''
Hiyo picha ni siku watoto wa Abdul Sykes waliponiita nikaione Medali aliyotunukiwa baba yao (posthumous) katika kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Aliyevaa nguo nyekundu ni Daisy na kushoto wa kwanza ni Kleist.