Abihudi Misholi vs Boni Mwaitege

Acha kufananisha Mwahangila na watu wa ajabu.
 
Wale wahenga wenzangu watakuwa wanakumbuka kuna mwimbaji enzi hizo alikuwa anaitwa Mwasumbi..kiukweli hajawahi kutokea kama yeye
 
Kwa Mungu hakuna mashindano!! ushindani wa ibilisi. kwa Mungu biashara ni moja tu! kuhubiri habari za Yesu.
 
Acha tu akisimulia Mungu alipomtoa na mapito aliyoyapitia ana kila sababu ya kuendelea kumtumikia Mungu..
Hiyo kazi aliipenda sana,abiud alikua anapiga shati lake limetoboka mgongoni,suruali ina celebration kali kalinyoosha na tai Huku hana viatu anaingia kwa mafimbo anahubiri na ataimba sana kumtukuza Mungu.
Si enzi hizo wala ganja tunaona huyu hayuko sawa kichwani.
Alikua na Target yake.
Kuna brother ake mkubwa ndo alikua muhubiri na familia yao kiukweli walikua watu wa mungu sana sema sijui vp walikua na mikasa sana
 
Binafsi namkubali Abiud.

"Mungu yuko hapa, Yesu Kristo yuko hapa....kwa nini mimi niteseke...!!" Mungu azidi kumtunza na kuachilia mafunuo zaidi ndani yake.
 
Usimfananishe Abiud na vitu vya kijinga😎

Kuna mmoja anaimba ili apate pesa ndio malengo yake makubwa, mmoja anaimba anamuimbia Mungu wake hajalala sana upande wa kupata pesa kupitia uimbaji
 
Ambwene Mwasongwe nadhani anaweza kuwa anaimba vitu vinavyofanana na Abiud....namkubali sama Ambwene.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…