Abihudi Misholi vs Boni Mwaitege

Abihudi amechagua fungu jema
 
Wote wawili hawana kitu kwa huyu Dogo anaitwa Joel lwaga,ameimba sitabaki km nilivyo
Acha masihara bro...yani huyo dogo amfikie abiudi? Kaskilze album ya abiudi..huyu mzee shida
 
Acha tu akisimulia Mungu alipomtoa na mapito aliyoyapitia ana kila sababu ya kuendelea kumtumikia Mungu..
Ila hiyo kazi aliipenda tangia utotoni, kuna kaka yake alikua mtumishi miaka hiyo simkumbuki jina Martin sijui, sasa alikua kabla na baada ya mahubiri Abiud Anaimba halafu wananena kwa lugha,sasa si marafiki zake mtaani tukiskia vile tunashangaa maana ukimkuta siku za kawaida sio yeye kabisa
 
ABIUD MISHOLI noma. Nakumbuka chuo UE ikikaribia nyimbo ya SHUKA BWANA inatamba sana na wakati tukisikia wiki ijayo matokeo yatatoka basi TENDA MIUJIZA inatawala sana.
 
Uyo mnyakusya yupo vizuri ila hata huyo jamaa mwingine anatisha.
Sema mnyakusya anachanganya sana L na R

Ila either way... wako vzuri
My vote...misholi
 
Mim sina dini Ila napenda wimbo wa misholi unaitwa ameniita mungu,shetani hunipati tena ,naupenda
 
wote hakuna mkali... Ila Abiud nyimbo zake chache nilizosikiliza ziko safi sana yaani za utulivu fulani na mafeelings kwa mbali..., sio Bony mpiga kelele tu kota kitambo sielewagi anachoimba.
 
kupambanisha watumishi wa Mungu kiushabiki si jambo jema lakini hata huu mfananisho umekosa mizania. Abiud angeweza kufananishwa na mtu kama Ambwene
 
Mpambano sio fair Abiud mlinganishe na wenzie wa miziki ya kuabudu kama marehemu Sedekia na type hiyo , Mwaitege nyimbo za kuchangamka kama kina Ambwene Mwasongwe , Rose Muhando , Bahati Bukuku etc
 
Wote wawili hawana kitu kwa huyu Dogo anaitwa Joel lwaga,ameimba sitabaki km nilivyo

hao wapaka shedo tunawaona kama waimba gospel wale wa Kenya kina Willy Paul sijui Bahati , hakuna Mungu ndani yao bali wapo kibinadamu zaidi
 
Kuna wimbo hivi mzuri Sanaa unaitwa mkono wako mwimbaji zabroni kutoka kahama kama kuna member anao anisaidie mana najaribu kuudownload unagoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…