Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi kupitia Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania limewaonya Madereva na Makondakta wa vyombo vya moto mikoa yote nchini kuacha kuzidisha abiria wanapokuwa safarini na kuzingatia kanuni za Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini (LATRA) kwani jeshi halitosita kuchukua hatua kali za sheria ikiwa ni pamoja kutozwa faini na kufungiwa leseni
Onyo hilo limetolewa na Kamishna msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Oparesheni kikosi cha Usalama barabarani Tanzania ACP Joseph Mwakabonga wakati wa Oparesheni ya Ukaguzi wa Magari katika Stendi Kuu ya Segera, iliyopo wilaya ya Handeni mkoani Tanga
Aidha amewataka madereva kuendelea kuchukua Tahadhari kwa kuendesha magari kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kuepuka matumizi ya Mwendokasi barabarani ambayo imekuwa ni chanzo cha ajali nyingi barabarani
ACP Mwakabonga amesema Jeshi la Polisi limejipanga imara katika vituo mbalimbali vya barabarani nchini ikiwa ni katika kuhakikisha wanadhibiti makosa yanayotokea Barabarani ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali madereva wanaokwenda kinyume na Sheria ya usalama barabarani.