Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Hii amri ya abiria toka mikoani kushushwa Mbezi mbona hatupewi ukweli, siku zilizopita ilidaiwa mkuu wa mkoa alilalamikiwa na wafanyabiashara kuwa wanakosa wateja!
Hivi sasa tunaambiwa eti ni usalama kudhibiti wahamiaji! Kwani wahamiaji hawawezi kushuka au kupanda Kibaha au Bagamoyo! Mabasi ni tofauti na ndege Ulaya kwani yanaweza kushusha au kupandisha abiria mahali popote kabla ya kufika Mbezi, hapa hoja ya wafanyabiashara ya kukosa wateja inaipiku ya uhamiaji.
Hivi vituo vya mabasi kusudio lake ni kufanya biashara ya mikate na chipsi? Hakuna msafiri anayesafiri kwa ajili ya kununua chipsi, kama mkuu wa mkoa anawatetea wafanyabiashara akifurahi wasafiri wakiteseka, basi hilo ni tatizo.
Viongozi wanaowajali abiria hawatakuwa tayari kuona abiria wanateseka kwa utashi wa watu binafsi.