DOUGLAS SALLU,
Wana JF, hebu tuwe na heshima!, hata kama watu wanatumia just pen names, kama mtu anatumia jina la kiume mfano Yohane Mbatizaji, hata kama in reality mtu huyo unamjua kuwa KE, humu jf aheshimiwe kwa jina analotumia ambalo linaonyesha gender yake ni HE!. Kitendo cha kumuita Mkuu John The Baptist kuwa ni dada ni kumdhalilisha!, na udhalilishaji huo haukuishia kwake, umemuingiza hadi Mwenezi wetu taifa, na kumuonyeshea ni mtu anayejivinjari na wadada hadi Dubai kama yule naniliu!.
Watu pekee ambao ni ruksa kuwahisi gender zao, ni wale, wanaotumia neutral names ambazo they don't depict gender kama kama jina la Wakudadavuwa, hadi mtu ajitambulishe mwenyewe gender yake, kama Mkuu Wakudadavuwa alivyojitambulisha kwangu kuwa yeye ni mkaka na mkubwa kwangu, hivyo mimi ni mdogo wake.
Kufuatia mimi siku hizi kuwa ni kada mpya wa Chama cha Mapinduzi, kila nikuona humu CCM inabagazwa, au viongozi wa CCM wana bagazwa, siwezi kukaa kimya, nitajitokeza kuwatetea na kukitetea chama changu humu Mitandaoni.
P