Abiria wa daladala tubadilike

Abiria wa daladala tubadilike

Salaam wakuu.

Heri ya pasaka kwa wale washerehekeao na ramadhan kareem kwa wale wafungao na heri ya sikukuu ya wajinga kwa tuisubiriyo.

Niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu.

Siku kadhaa zilizopita nilikuwa natoka tegeta naelekea kariakoo kwa daladala za T/NYUKI-GEREZANI.

siti niliyokuwa nimekaa nilikuwa na mdada fulani hivi kibonge aliyekuwa na bahasha ya chips.

Gari limetembea tembea akatoa chips yake kwenye bahasha na kuanza kuifakamia chips.
Nasema kuifakamia sababu alikuwa anakula kama vile anakimbizwa.

Wandugu kama unajijua haujui kula kistaarabu basi hakikisha umekula kwenye umma wa watu wachache tena walio busy na mambo yao kama kwenye vibanda vya chips.

Na sio kwenye umma wa watu wengi maana unaweza kujikuta unatia aibu na kuwatukanisha wazazi wako kwamba hawajakufundisha kula kistaarabu.

Kibonge wa watu kamaliza kula chips zake akafinyanga finyanga ile foil na bahasha na kuitupa dirishani huku gari likiwa linatembea.
Wakati huo daladala ina dustbin na tulikuwa tumekaa mbele kabisa jirani na makazi ya konda.

Akaona haitoshi akatoa dumu la maji kwenye mkoba na akanywa na akarudia kitendo kilekile cha kutupa nje ya gari huku likiwa lianatembea.

Shame upon her. Shame upon her. Shame upon her.
Na kama unaisoma hii jua kwamba nilikumaindi.

Huyo ni mfano mmoja nilioukumbuka saa kwa harakaharaka nilipokuwa nataka kuwasilisha kero yangu.
Ila watu wa aina hii wako wengi sana tena kwenye jiji letu la Dar es salaam.

Wadada mjiheshimu aisee, mnajipunguzia point kwa vijimambo vidogovidogo vya ajabu mnavyovifanya.
Mnatia aibu.

Huwa naitafakari sana akili ya mtu ambaye anatupa taka hovyo, hii haijalishi ni kwenye daladala au penginepo.

Jambo hili limekuwa ni kama tabia sasa, mtu anakunywa energy yake anamaliza anatupa kopo barabarani.Hata kama kuna watu wa usafi, mambo mengine ni ya kuyarekebisha wenyewe hata kabla hayajarekebishwa na watu baki.

Aisee watu mnaotupa makopo ya kwenye daladala muache.
Mnatukwaza.
Mnatukwaza sana.

Inawashushia heshima sana ni hamjui tu.
Watu hawawaambii papo kwa papo kuepusha mambo mengine ila mnawakera sana.

Natamani mamlaka ziweke sheria kali zitakazowawajibisha vikali watu wanaotupa taka kwenye usafiri wa umma.

TUBADILIKE.
TUBADILIKE.
TUBADILIKE.
Huyo kafanya makusudi akidhani anawakomesha waislam
 
Yaani mzungu aache kuwaza plan zake zinaendaje aje hukunjf kumlalamikia dada aliyekutanq nae kwenye daladala?

Yaani ajikwaze siku nzima mpaka awe traumatized kama wewe kisa mtu ambaye hana maslahi naye?

They always mind their own BIZNESes ndo mana mambo yao yananyooka.
Mzungu pori au ? Waswahili uwa mnanichekesha sana kuwafanya wazungu kama miungu yenu
 
Salaam wakuu.

Heri ya pasaka kwa wale washerehekeao na ramadhan kareem kwa wale wafungao na heri ya sikukuu ya wajinga kwa tuisubiriyo.

Niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu.

Siku kadhaa zilizopita nilikuwa natoka tegeta naelekea kariakoo kwa daladala za T/NYUKI-GEREZANI.

siti niliyokuwa nimekaa nilikuwa na mdada fulani hivi kibonge aliyekuwa na bahasha ya chips.

Gari limetembea tembea akatoa chips yake kwenye bahasha na kuanza kuifakamia chips.
Nasema kuifakamia sababu alikuwa anakula kama vile anakimbizwa.

Wandugu kama unajijua haujui kula kistaarabu basi hakikisha umekula kwenye umma wa watu wachache tena walio busy na mambo yao kama kwenye vibanda vya chips.

Na sio kwenye umma wa watu wengi maana unaweza kujikuta unatia aibu na kuwatukanisha wazazi wako kwamba hawajakufundisha kula kistaarabu.

Kibonge wa watu kamaliza kula chips zake akafinyanga finyanga ile foil na bahasha na kuitupa dirishani huku gari likiwa linatembea.
Wakati huo daladala ina dustbin na tulikuwa tumekaa mbele kabisa jirani na makazi ya konda.

Akaona haitoshi akatoa dumu la maji kwenye mkoba na akanywa na akarudia kitendo kilekile cha kutupa nje ya gari huku likiwa lianatembea.

Shame upon her. Shame upon her. Shame upon her.
Na kama unaisoma hii jua kwamba nilikumaindi.

Huyo ni mfano mmoja nilioukumbuka saa kwa harakaharaka nilipokuwa nataka kuwasilisha kero yangu.
Ila watu wa aina hii wako wengi sana tena kwenye jiji letu la Dar es salaam.

Wadada mjiheshimu aisee, mnajipunguzia point kwa vijimambo vidogovidogo vya ajabu mnavyovifanya.
Mnatia aibu.

Huwa naitafakari sana akili ya mtu ambaye anatupa taka hovyo, hii haijalishi ni kwenye daladala au penginepo.

Jambo hili limekuwa ni kama tabia sasa, mtu anakunywa energy yake anamaliza anatupa kopo barabarani.Hata kama kuna watu wa usafi, mambo mengine ni ya kuyarekebisha wenyewe hata kabla hayajarekebishwa na watu baki.

Aisee watu mnaotupa makopo ya kwenye daladala muache.
Mnatukwaza.
Mnatukwaza sana.

Inawashushia heshima sana ni hamjui tu.
Watu hawawaambii papo kwa papo kuepusha mambo mengine ila mnawakera sana.

Natamani mamlaka ziweke sheria kali zitakazowawajibisha vikali watu wanaotupa taka kwenye usafiri wa umma.

TUBADILIKE.
TUBADILIKE.
TUBADILIKE.
Mpuuzi mkubwa wewe.
Dala dala na muda wakumuangalia mtu ni wapi na wapi?
 
You sound like hiyo tabia ni ya wadada tu! Nimeona wanaume wakitafuna muhindi na kutupa gunzi nje, ingetosha kukemea hii tabia kwa ujumla bila kuininafsisha kwa 'wadada' kama maelezo yako yalivyo.
 
Humu ndani kuna watu wa hovyo namna hii,mwamba amekuja na kemeo kali juu ya mambo ya kijinga lakini bado Kuna mbongo amekaza mishipa ya Shingo anaandika ujinga,sasa mkuu hivi kwenye jamii yako wanafaidika na nini kupitia wewe ikiwa hapa tu ndani ya Dakika chache ushatema ujinga humu
Wewe ni mpumbavu na mpuuzi sana!....
 
Kuna mdada mmoja nilkua nasafiri kutoka Mwanza kwenda moshi .yule dada kaanza kula ovyo kuanzia shy hadi Singida.. kimbembe kutoka apo Singida ilikua ni tatizo ana rudisha chench kupitia dirishan while gari liko speed imagine safari yangu ilivyo kua mbaya ..
 
Ulimwambia? Kama ulikosa ujasiri wa kumchana pale pale halafu unakuja kuleta majungu huku, unataka sisi tukusaidiaje?

NB. Hii tabia ya kula hovyo ni mbaya, unakuta mdada anatoa chapati kwenye mkoba ndani ya daladala anaanza kula, akimaliza natoa tissue anajifuta halafu anatupa chini.. huu sio ustaalabu.
 
Ulimwambia? Kama ulikosa ujasiri wa kumchana pale pale halafu unakuja kuleta majungu huku, unataka sisi tukusaidiaje?.
Thubutu mfano ni mwanamke wa kizaramo halafu ujitie ujasiri kumchana atakachokujibu utaomba ushuke kituo kinachofuata hata kama hushuki hapo na suti xako za kistaarabu na kutoka hapo utaelewa ule msemo wa mind your own business maana yake nini?
 
Suala la ustaarabu, Wabongo tupo nyuma mno

Sasa Umbali huo tu, mtu anafakamia machipsi barabarani utasema hawezi kula akifika mwisho wa safari yake 🙌
 
Dar ni mji wa pilipilika mtu anafabya kazi kwa muhindi unataka akafike nacho ale kwa muhindi ?.mhindi atamwachisha kazi atamuona mwizi huwa anamuibia hela kuwa haiwezekani kwa mshahara anaompa amudu kununua chips kuku ndio maana anakula kabisa
 
Cha ajabu nini kula na kunywa kwenye basi.Mabasi ya safari ndefu mbona watu wanskula na kunywa ndani ya basi wakati linatembea
Kuna sehemu nimezungumzia kula na kunywa kwenye mabasi.

Au unapachika maneno yako uchwara yasiyo na mantiki.
 
Dar ni mji wa pilipilika mtu anafabya kazi kwa muhindi unataka akafike nacho ale kwa muhindi ?.mhindi atamwachisha kazi atamuona mwizi huwa anamuibia hela kuwa haiwezekani kwa mshahara anaompa amudu kununua chips kuku ndio maana anakula kabisa
Kwasababu hiyo naweza kuielewa
 
Humu ndani kuna watu wa hovyo namna hii,mwamba amekuja na kemeo kali juu ya mambo ya kijinga lakini bado Kuna mbongo amekaza mishipa ya Shingo anaandika ujinga,sasa mkuu hivi kwenye jamii yako wanafaidika na nini kupitia wewe ikiwa hapa tu ndani ya Dakika chache ushatema ujinga humu
Tanzania imejaaa wajinga wengi sana mkuu
 
Mpuuzi mkubwa wewe.
Dala dala na muda wakumuangalia mtu ni wapi na wapi?
Shukrani sana mkuu.

Nadhani lugha sahihi uliyopaswa kuitumia ni kupinga hoja yangu kwa hoja yako na wala si kunitukana.

Umedhihirisha kichwani kwako kukoje
 
You sound like hiyo tabia ni ya wadada tu! Nimeona wanaume wakitafuna muhindi na kutupa gunzi nje, ingetosha kukemea hii tabia kwa ujumla bila kuininafsisha kwa 'wadada' kama maelezo yako yalivyo.
Soma thread vizuri.

Kwenye title nimesema.

Abiria wa daladala tubadilike.

Kwenye body nikaongelea tabia hiyo kwa kutumia mfano wa huyo mdada uliotokea juzi kati hapo.

Na nikasema kabisa vitendo hivi vinafanywa na wengi.
 
Ulimwambia? Kama ulikosa ujasiri wa kumchana pale pale halafu unakuja kuleta majungu huku, unataka sisi tukusaidiaje?

NB. Hii tabia ya kula hovyo ni mbaya, unakuta mdada anatoa chapati kwenye mkoba ndani ya daladala anaanza kula, akimaliza natoa tissue anajifuta halafu anatupa chini.. huu sio ustaalabu.
Mkuu majungu yapi niliyoleta.
 
Dar ni mji wa pilipilika mtu anafabya kazi kwa muhindi unataka akafike nacho ale kwa muhindi ?.mhindi atamwachisha kazi atamuona mwizi huwa anamuibia hela kuwa haiwezekani kwa mshahara anaompa amudu kununua chips kuku ndio maana anakula kabisa
Shida sio kula kwenye gari shida ni kutupa mataka taka nje ya gari.
 
Back
Top Bottom