TAARIFA
Mimi kama mleta mada naomba nitoe ufafanuzi kwa wasomaji na wachangiaji mbalimbali juu ya mada niliyoiweka hapa majira ya jana usiku.
Nilichokileta hapa ilikuwa ni kero ambayo inatokana na vitendo vya abiria wa daladala za dar es salaam kutupa takataka za bidhaa wanazozitumia wakiwa ndani ya usafiri wa daladala.
Hichi ni kitendo kinachofanywa na abiria wa aina zote.
Me kwa Ke, watoto kwa wakubwa.
Jambo hili likikaliwa kimya na kuonekana ni la kawaida kuna watoto wanakua na wanaona.
Wataona ni kitendo sahihi na kinachokubalika katika jamii.
Mdada niliyemtumia hapo nimemuweka kama sampuli miongoni mwa watu wengi ambao ninawaona wakifanya vitendo hivyo ila yeye ni kama alikithirisha ukiangalia na namna alivyokuwa(hafananii kabisa).
Wito kwa wote wanaotaka kuchallenge hoja yangu.
Njooni mnichallenge kwa hoja zenye mashiko na si matusi.
Kila mmoja anajua kutukana na sidhani kama wote tukiamua tutukanane itakuwa ni jukwaa tena.
ASANTE.