John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro zimesababisha madhara kwa kuharibu miundombinu ya reli ya kati na barabara ambapo daraja la Kidete Wilaya ya Kilosa limekatika na kusababisha treni kusimamisha safari zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majid Mwanga amefika eneo la tukio na kuwatoa hofu watumiaji wa njia hiyo, akieleza timu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeshafika hapo na inafanya kazi ya kurejesha miundombinu katika matumizi ya kawaida.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu na Tathimini TRC, Mhandisi Nelson Mtejo amesema daraja hilo lina urefu wa mita 36 na ina kingo za zege, Serikali imeanza kufanya matengenezo katika eneo hilo.