Kuna siku (niliisikia hii story Power Breackfast) hivyohivyo mida ya usiku kama saa 3 hivi daladala la Ubungo Mbezi tena nasikia ilikuwa ile mi'bus mikubwa limesimama Ubungo konda anapigia debe Kimara,siku hiyo nasikia magari ya Mbezi yalikuwa adimu sana,abiria wa Mbezi kibao pale kituoni si wakaamua kupanda hivyoX2 konda kachukua nauli wamefika Kimara dereva kaligeuza kweli wakaanza kurudi Mjini,abiria walimvyomfata dereva akawatishia kuingiza bus mtaroni,hapo basi lipo kwenye mwendo mkali vibaya mno,dereva anakanyaga mafuta huku anachimba mkwara akiguswa amelibwaga,maskini abiria wale ikabidi wawe wapole,dereva anachochea tu,kufika Ubungo walitegemea ange'park ili kama vipi ndo wampige waapi wakiwa wanateremka kwenye mataa ya ubungo si kijani ya kunyoosha na kukunja ikawaka akalala nayo kulia,mpelampela unaambiwa Mandela road sasa hiyo. abiria wote roho mkononi,kufika external akalikunja tena kulia mpelampela kwenye rough road hivyohivyo mpaka Pori gani sijui huko akali'park akateremka mbio,hiyo sasa ilikuwa mida ya saa 5 unaambiwa,ikabidi abiria wam'tight konda,dakika chache likaibuka kundi la vijana na magongo/fimbo(kumbe mitaa ile ndo anayokaa dereva,kwahiyo alienda kuwaita wavuta bangi wenzake wakataka kuwachapa abiria,abiria na wenyewe wakakomaa wakiguswa wanalipiga moto basi ukichukulia miongoni mwao kulikuwa na wavuta fegi wasingekosa viberiti basi unaambiwa mzozo mkubwa ukatokea pale porini,bahati nzuri abiria mmoja alikuwa na namba za Bonge wa Clouds akampigia,bonge ndo akaenda pale na deffender ya polisi wakam'tight Konda akawapeleka kwa dereva wakamchukua wakamlazimisha apeleke abiria Mbezi under escort kisha akarudisha gari polisi na yeye kuhifadhiwa,sijui walimalizaje kesi ile ila abiria wa Mbezi siku ile walifika makwao saa 8 usiku.
My Take:
Kiukweli watumiaji wa usafiri wa daladala huwa wanateseka sana nyakati za asubuhi na jioni,hata kesi inapofikishwaga mbele ya sheria mathalani Polisi huwa inamalizwaga kiaina sana ksbb Jamaa huwa wanawatoa buku 2,2,5,5 dawa ni kuchukua hatua kama ile iliyochukuliwa na abiria wale walioelezewa na mtoa mada,big up kwao sana,matukio ya namna hii yakiwa yanatokea mara kwa mara watatia nidhamu.