28 FEBRUARY 2026, Basi la Abood lilitoka Mbezi Bus Terminal, kufika chuo cha St Joseph likapata hitilafu, wahusika wakatoa taarifa kuwa Bus imekata Fen Belt, hivyo abiria tuwe wavumilivu fundi anakuja.
Tulikaa tangu Saa 1 Usiku hadi Saa 5 Usiku ndio Bus linaanza kutoka tena safari ya kutoka DAR-MBEYA, tulivyofika Msamvu Stendi wakatangaza Bus haiingii ndani ya kituo hicho, linaelekea Yard Kuu ya Abood kujaza mafuta, hapo ni Usiku wa Saa 9.
Your browser is not able to display this video.
Kufika Yard Bus ikapaki bila kujaza mafuta wala hakukuwa na taarifa yoyote Saa 10 ndipo abiria wakacharuka wakitaka wapewe bus lingine, kwa kweli ABOOD Customer Care si nzuri.
Ni zipi haki za abiria kupotezewa muda wao, safari ya DAR-MBEYA ilitumia Saa 24, ni sawa?
Abood ameluhuusu baadhi ya watu kuweka bus zao kwenye kampuni yake ndo shida ilipo anzia Abood ilikuwa zamani saiv hakuna kitu nilipanda gari lao mwezi wa kwanza gari siti cover mbovu kishenzi hakuna ace