Aboud Jumbe na Mke wa Idris Abdul Wakil hajaalikwa

Mbona hamumtaji mke wa Dr Omar Alli Juma

Dr Omar Ali Juma hakuwahi kuwa Rais wa Zanzibar wala Waziri mkuu wa Tanzania bali makamu wa rais na waziri kiongozi ndo maaa Nahodha hayumo pia waziri kiongozi wa Jumbe, Brigedia Ramadhani Haji naye katengwa kisiasa maana wote walifukuzwa 1984
 
Mnataka mzee wa watu apelekwe kwenye machela? Mnaijua hali ya afya yake? Ni tukio gani mmemwona hadharani mara ya mwisho? Mkipata majibu ya haya basi mtajua kwa nini hakualikwa
Wangealikwa na kuwepo kwenye list kisha tuambiwe fulani na fulani hawatahudhiria kwa sababu za kiafya na watanzania tuwaombee wapate nafuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
swali muhimu wakuu,
kwanini ccm inapinga serikali tatu?.
mwenye hekima ya ki-GT naomba ajibu kwa faida ya wanajf wote/kuweka record sawa.
natunguliza shukrani.

Hawataki demokrasi kubwa wanataka watumishi wa serikali wa ngazi za juu wazidi kuwa wakuteuliwa ndo sababu pia hawakutaka serikali za majimbo maana wakuu wa mikoa na wilaya watachaguliwa na wananchi na si kuteuliwa na Rais jambo ambalo litapunguza mamlaka na nguvu za Rais kitu ambacho CCM hawaki pia lengo kubwa la viongozi wa juu CCM wazidi kusujudiwa na watu ili wawateue sehemu mbalimbali wawe miungu watu ndo sababu Lowassa kazungukwa na watu sio kwamba wanampenda au ana dira ya kweli na Tanzania bali wanajua urais unanukia kwake basi wawe karibu ili akiutwaa basi wateuliwe sehemu mbalimbali,
 
Mkuu HNIC hebu funguka tukuelewe vizuri. Hawakualikwa kwenda wapi na je, kama ni wake wa marais waliowahi kuongoza TZ na ZNZ, Mzee Aboud Jumbe anaingiaje kwenye orodha hii?. Tulia unyooshe mambo Mkuu. Naomba kuwasilisha.

yaelekea hufahamu aboud jumbe ni nani.
 

asante,japo sijaridhika na ufafanuzi wako.
 
Wangealikwa na kuwepo kwenye list kisha tuambiwe fulani na fulani hawatahudhiria kwa sababu za kiafya na watanzania tuwaombee wapate nafuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wawaalike halafu what?!. Kumfurahisha nani? Uzee una nafuu? Uzee ni leo afadhari ya Jana.
 

Asante Mkuu. Nimepata kwa kuanzia angalau. Ngoja niendelee kuelimika hasa kuhusu sababu iliyofanywa waachwe.
 

Really?? Basi hii habari mpya sijawahi kuisikia kabisa japo wakati mzee Jumbe anajiuzulu nilikuwa darasa la 5, na enzi hizo tukisoma tukiwa wakubwa. Hebu kaka zetu na wanaoijua historia kama nguruvi, mag3 na wengine mtusaidie kuhusu usahihi wa hili aliloandika hapa, Rich Pol.
 
Kama kuna mtu wa kujivunia ktk mabadiliko ya katiba ni jumbe kwani aliyokuwa akidai na kuonekana msaliti ndio yaliyopendekezwa na tume ya katiba.wanaharakati mko wapi kumtetea mtu huyu
 
Mkuu nadhani ni habari ya kusadikika,kilichoelezwa wakati huo ni kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa,kuliko sababishwa na Jumbe kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili
 
Mnataka mzee wa watu apelekwe kwenye machela? Mnaijua hali ya afya yake? Ni tukio gani mmemwona hadharani mara ya mwisho? Mkipata majibu ya haya basi mtajua kwa nini hakualikwa

mkewe je? au mwakilishi wake?
 
Habari ni kuwa wake wa marais waliowahi kuongoza TZ na ZNZ wamealikwa kesho na wamegharamiwa

lakini cha ajabu kwenye mwaliko huo hatokuwepo mke wa Marehem Idrissa Abdul Wakil na wala hatokuwepo Mzee Aboud Jumbe

kulikoni?

Hapo ndo ufahamu kuwa CCM na JK ajenda yao moja Serikali 2. Hao viongozi walikuwa mwiba mkali sana kwa Nyerere walitaka Serikali 3 mpaka Jumbe akanyanywa nafasi zote za uongozi CCM na katika serikali ya Zanzibar na kuwekwa kizuizini -Jumbe na Wakil. So hawawezi kukanyaga Dodoma wasije kuwa kama Mtikila anavyowasumbua pale.
 
asante,japo sijaridhika na ufafanuzi wako.


Nyongeza nyingine wanaogopa Chadema kuunda serikali ya bara na CUF kuunda serikali ya Zanzibar wao wakakomea serikali ya Muungano na wakawa hawana madaraka mengi kwasababu wanajua Chadema ni mashuhuri bara na Zanzibar haina washabiki wengi na CUF ni mashuhuri Zanzibar na bara ina wachache kwa mtizamo huo CCM wanaamini huwezi kushinda kuwa Rais wa Jamhuri bila kuwa mashuhuri pote maana wapiga kura wa Rais huyo ni wa bara na visiwani kwa mtaji huo watazidi wao kuongoza labda Chadema na CUF waungane hiyo ndio calculation yao kuu ndo maana hawataki hoja ya serikali tatu na Chadema hawaoni tatizo swali la nyongeza mkuu iwapo hujaridhika uliza tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…