Absalom Kibanda akamatwa!

Absalom Kibanda akamatwa!

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Jeshi la polisi linamshikilia mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, A. Kibanda kwa tuhuma za uchochezi. Kibanda anashikiliwa kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam.

===============

UPDATES

Habari zilizonaswa sasa hivi kutoka makao makuu ya polisi Dar zinasema Mhariri wa Tz Daima Absalom Kibanda ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa matatu kwa tuhuma za uchochezi. Amedhaminiwa na Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea kwa dhamana ya Sh 5,000,000/-. Kibanda anatakiwa kuripoti polisi hqtrs Jumatatu asubuhi.

PIA, SOMA:

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

 
wanamshikilia yeye wakati magazeti yanasambaa na ujumbe
 
uchochezi upi kafanya?au kurusu kuchapwa makala ya kukosoa polisi?
 
Hawawezi kupora haki ya watz kuhabarishwa. wachochezi ni wabunge wa ccm. A. kibanda ataibuka shujaa!!!! Tupo pamoja nawe kamanda.
 
Ukiona hivi ujue taarifa za kiintelejensia zinazo wasilishwa ikulu na hao usalama sijui wa taifa/ccm zinaonyesha magamba hali inazidi kuwa mbaya daily, kinachofanyika sasa ni kukabiliana na yeyote na kwa namna yoyote kwa anayezidi kuwa amusha watanzania toka usingizini, believe me mpaka 2015 kuna watu wengi sana watakuwa wako jela
 
Another flagrant example of abridgement of freedom of speech.
 
Hii nchi bana....kesho utasikia Yo YO korokoroni kwa kuwa member wa JF......
 
Mwenye details aweke basi, .....haitoshi kusema kuwa Kibanda kakamatwa!!
 
Mwenye details aweke basi, .....haitoshi kusema kuwa Kibanda kakamatwa!!

Ni kweli habari nepesi mno, hata hivyo huo uchochezi kama ni zile makala za kuamsha watawala basi na tufurahi naye kufikishwa kwake mahakamani..sina uhakika watapeleka wangapi mahakani kabla ya ku-apply njia sahihi za kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yao hasa ufisadi na umaskini uliokithiri..
 
Ni kweli habari nepesi mno, hata hivyo huo uchochezi kama ni zile makala za kuamsha watawala basi na tufurahi naye kufikishwa kwake mahakamani..sina uhakika watapeleka wangapi mahakani kabla ya ku-apply njia sahihi za kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yao hasa ufisadi na umaskini uliokithiri..


Ingekuwa vizuri mleta mada akatupatia details zaidi au walau aseme kuwa anafuatilia. Si tabia nzuri ya mtu kuleta breaking news kiduchu na kuwaachia wengine wajazie nyama
 
Kweli TZ inahitaji ukombozi umpya! Bora basi waanze ujenzi mpya wa magereza makubwa kwa ajiri ya wanaharakati kama Kibanda na wengineo maana haya yaliyopo yameshajaa yote.
 
Itakuwa ni mwendelezo wa kesi ya Mwigamba 'Kalamu ya Mwigamba' TD kila jumatano, Kibanda akiwa kama mhariri mtendaji anaunganishwa katika kesi ya uchochezi kufuatia kuruhusu makala inayodaiwa kuwachochea askari polisi wasiwatii maofisa wao, kwa kuwa tayari wanaye Kibanda, tusubiri kukamatwa mchapishaji, Mwananchi publications
 
Na wanavyoendelea kumshikilia na kumghasighasi ndivyo wanavyozidi kuvuta hisia za watu kujua hiyo habari ikoje na hivyo kuzidi kuusambaza huo waliouita uchochezi. Yani ndivyo wanavyozidi kujimaliza kwa kuongeza publicity ya ishu hiyo katika jamii.
 
Hebu tuelezeeni kwa kina kisa cha kukamatwa ni nini? habari hii bado ina-hang
 
Back
Top Bottom