Absalom Kibanda Aliteswa wakati ana Kesi ya Uchochezi (Inayohusu Polisi)

Absalom Kibanda Aliteswa wakati ana Kesi ya Uchochezi (Inayohusu Polisi)

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,786
Reaction score
1,715
Wakati upelelezi mwingine unaendelea juu ya Sakata la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda, ikiwemo kuhojiwa kwa Maggid Mjengwa, tujikumbushe kuwa Kibanda ana kesi. Tena kesi ya uchochezi inayolihusu jeshi la polisi moja kwa moja.

Makala hii inaelezea vizuri kesi hiyo

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, uliupatia upande wa utetezi nakala ya mlalamikaji katika kesi hiyo kama ulivyokuwa umeamriwa na mahakama hiyo kufanya hivyo.


Sambamba na hilo Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi , Wakili Mwandamizi wa Serikali Prosper Mwangamila aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi na kwamba wamekuja na mashahidi wa wawili ambao ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza(ACP), George Mwampashi na Rafael Hokororo na wapo tayari kwaajili ya kuanza kutoa ushahidi.

Lakini hata hivyo Hakimu Moshi alisema hakimu anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema amepata hudhuru hivyo yeye amepewa kesi hiyo jana kwaajili ya kuiarisha na hivyo anaiarisha hadi Oktoba 22 mwaka huu, nakuwataka mashahidi wote wafike bila kukosa.

Kwa mujibu wa nakala ya maelezo ya mlalamikaji wa kesi hiyo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), David Hizza ambaye anafanya kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi nchini, alidai kuwa moja ya majukumu yake ni kufuatilia matishio ya uhalifu pamoja na matukio ya uhalifu a kwamba anakumbuka Novemba 30 mwaka 2011 alipata nakala ya gazeti la Tanzania Daima toleo la Namba 2553.

Hizza alidai katika kulisoma nilikuta makala iliyokua katika ukurusa wa 14 ambayo ilisomeka ‘Kalamu ya Mwigamba' na ikaonyesha kuwa imeandikwa na mtu aitwaye Samson Mwigamba ambaye ni mdaiwa wa kwanza na makala hiyo ilisomeka ‘Waraka maalumu kwa askari wote' na katika kuisoma makala hiyo alibaini kuwa mwandishi alionyesha kuwaandikia askari wanaofanya kazi katika majeshi ya Jeshi la Polisi,Jeshi la Kujenga Taifa,Kikosi maalum cha Kuzuia Magendo,Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

"Katika kuusoma waraka huo yapo maeneo ambayo niliyaona kuwa ni uchochezi kwa askari hao kuwafanya wasiwatii viongozi wao jambo ambalo linaweza kuleta uasi jeshini.Maneno niliyoyaona kuwa ni uchochezi ni haya; "Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kila ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya'

"Na pia kulikuwa na maneno yanayochochea chuki kwa askari dhidi ya serikali yao ambayo ameitaja kuwa inawategemea wao lakini huku ikiminya haki zao na wazazi wao ‘Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung'oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wanafanya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung'oka madarakani jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia.Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea ninyi.Wanaminya haki zenu ninyi wenyewe,haki za wazazi wenu,marafiki zenu,jamaa zenu na majirani zenu"alidai SSP-Hizza.

Hizza alidai maneno kwamba askari wako tayari kung'oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia kung'oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia wa kawaida na askari kuonyesha jinsi askari wasivyojari utu wa raia jambo ambalo linachochea chuki dhidi ya majeshi yetu kwa raia na kwamba kitendo cha kuwaambia askari wasiwatii viongozi wao wanaowaamuru katika shughuli zao ni kuwashawishi wasitii kiapo cha utii walichofanya wakati wanaajiriwa kama askari ‘kinachomtaka kila askari kuwa mwaminifu na mtii kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa uaminifu kuitumikia na kuilinda jamhuri wakati wote wa utumishi wao na kutii amri zote za rais na viongozi walio juu yao'.

"Ushawishi huo alioufanya mwandishi wa makala hiyo ni uvunjaji wa sheria za nchi na baada ya kuusoma waraka huo niliwasiliana na viongozi wangu katika idara na wote baada ya kuupitia walikuwa na maoni kuwa una taarifa za kiuchochezi hivyo ni vema waliohusika wahojiwe na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta naye mahojiano na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta mwandishi wa makala hiyo(Mwigamba) na kufanya naye mahojiano na akakiri kuwa ndiye aliyeandika waraka huo lakini akadai alifanya hivyo kwa lengo la kuelimisha"alidai Hizza.

Aliendelea kueleza kuwa maelezo ya Mwigamba yaliandikwa kisha akapelekwa mahakamani hapo pia alimwita Mhariri Mtendaji wa gazeti hili Absalom Kibanda ambaye naye alimhoji juu ya uhalali wa gazeti lake kutoa waraka huo ambao ni wa kichochezi lakini naye akadai waraka huo ni wa kawaida na siyo wa uchochezi kwa askari hivyo naye alipelekwa mahakamani na kwamba alimwita na kumhoji Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication ambaye ni mshitakiwa wa tatu, Theophil Makunga ambaye kampuni yake ndiyo ilichapa gazeti hilo na kumhoji.

Aidha alidai kuwa kwa upande wa Makunga alidai anao mkatana na kampuni ya Freemedia ambyo nio watoaji wa gazeti hilo unaonyesha kuwa jukumu la kisheria la yaliyomo katika katika gazeti hilo anayewajibika ni Free Media na sio wao.Ili kulithibitisha hilo kisheria nilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Raphael Hokororo ambaye alidai jukumu la uchapaji haliondolewi na mkataba huo bali linabaki kwa kampuni hiyo ya uchapaji na alikusanya ushahidi na kisha kulipelekea jalada kwa maoni ya kisheria.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Septemba 11 mwaka 2012.

My take:

Kamata kamata ya akina Maggid, video ya Rwakatare na kesi ya ugaidi, vinaweza kutufanya tusahau bifu kama hizi ambazo zilikuwepo kati ya Polisi na Kibanda.

Sijui kama DPP atakuwa na interest ya kujaribu kuona connection kati ya bifu hii na tukio la Kuteswa Kibanda.

PIA, SOMA:

- Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

 
Kwahili
IKULU na
hasa JK, na timu yake (TISS) wanahusika from A - Z. Ndo
maana kwa sisi wenye akili tunajua tu Uchunguzi wa issue hii ya KIBANDA,
utaishia juu juu kama ilivyokuwa kwenye issue ya "kujivua gamba", na
udhaifu huu wa kuanza jambo na kushindwa kulikamilisha obvious ni wa
JK!!
huo ni ukweli usiopingika ndg.yangu JK anahusika na unyama wote
unaoendelea,kumbuka mtikila aliwahi kumuita gaidi wengi
hawakuelewa,lakini kwa sasa rangi zote za JK tumeziona.nchi haitakuwa salama hadi huyu gaidi aondoke zake madarakani.
 
"Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kila ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya" - Samson Mwigamba.

Maneno hayo Mwigamba alikuwa anawaambia maaskari wa majeshi ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Kikosi maalum cha Kuzuia Magendo, Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Maneno hayo yaliwakera sana watawala wetu na TISS.

Kwa kuwa Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti lililochapisha makala hiyo, naye pia alishtakiwa kwa kosa la UCHOCHEZI.
 
Mwandishi akamatwa tuhuma za kushambuliwa kwa KibandaHabari zilizolifikia gazeti hili jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa KibandaSource; Mwananchi jpili
 
Mwandishi akamatwa tuhuma za kushambuliwa kwa KibandaHabari zilizolifikia gazeti hili jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa KibandaSource; Mwananchi jpili
Wanajaribu kuipotezea.

Suala zima ni kuwa huyu Kibanda alionekana kuwakera watawala kwa makala zake.

Huyu si wa kwanza: Tunajua jinsi Said Kubenea na Jerry Muro walivyoshughulikiwa.

Sasa watafukiaje uchafu wao wenyewe? Maggid Mjengwa na Ludovick mbuzi wa kafara?
 
Wanajaribu kuipotezea.

Suala zima ni kuwa huyu Kibanda alionekana kuwakera watawala kwa makala zake.

Huyu si wa kwanza: Tunajua jinsi Said Kubenea na Jerry Muro walivyoshughulikiwa.

Sasa watafukiaje uchafu wao wenyewe? Maggid Mjengwa na Ludovick mbuzi wa kafara?

Well said mkuu..
Hiyo habari nimeisoma mwananchi nikaona niwashirikishe! Hope nimesomeka
 
Naikumbuka hii kesi.

Naanza ku connect dots....


Unganisha na taarifa aliyopeleka kibanda kwamba kuna watu wanamfuata na isichukuliwe hadi anadhurika.

Ongezea na maneno aliyosikia kibanda wakati anateswa "afande mshoot, mshoot afande....",

Changanya na kigugumizi cha polisi katika kumtafuta aliyemgaidi kibanda.

n.k.n.k!

TWENDE KIONGOZI, TUKO PAMOJA!
 
Unganisha na taarifa aliyopeleka kibanda kwamba kuna watu wanamfuata na isichukuliwe hadi anadhurika.

Ongezea na maneno aliyosikia kibanda wakati anateswa "afande mshoot, mshoot afande....",

Changanya na kigugumizi cha polisi katika kumtafuta aliyemgaidi kibanda.

n.k.n.k!

TWENDE KIONGOZI, TUKO PAMOJA!
Unganisha na akina Nape na Ridhiwani kutoa matamko ya haraka haraka..

Unganisha na safari za watawala wetu kwenda kumwona hospitalini...

Unganisha na Mwigulu kuongea kwa jazba sana bungeni juzi huku akipiga meza kwa nguvu na akivumiliwa na spika...
 
Ingefaa kama mashirika ya kijasusi kutoka nje ya nchi kupeleleza hili tukio.Kwani kwa sasa wanaopeleleza ndo watuhumiwa wa haya matukio.Wananchi tulio wengi hatuna imani na vyombo vyetu vya dola.
 
Kibanda aliwahi kuiita serikali ya j.k ni dhaifu kabla hata ya mhe. Mnyika

Kibanda amewahi kukataa uteuzi wa mhe. Nchimbi wa ujumbe wa vazi la taifa
 
Unganisha na akina Nape na Ridhiwani kutoa matamko ya haraka haraka..

Unganisha na safari za watawala wetu kwenda kumwona hospitalini...

Unganisha na Mwigulu kuongea kwa jazba sana bungeni juzi huku akipiga meza kwa nguvu na akivumiliwa na spika...

unganisha na jinsi nape alivyojipendekeza kupiga picha na kibanda kwenye chumba alichokuwa amelazwa huko s.Africa lakini akaishia kutimuliwa kama mbwa koko.......
 
Wanajaribu kuipotezea.

Suala zima ni kuwa huyu Kibanda alionekana kuwakera watawala kwa makala zake.

Huyu si wa kwanza: Tunajua jinsi Said Kubenea na Jerry Muro walivyoshughulikiwa.

Sasa watafukiaje uchafu wao wenyewe? Maggid Mjengwa na Ludovick mbuzi wa kafara?

Mkuu hapo kwenye RED hao sio Mbuzi wa Kafara wanaingizwa hapo huku wakijua ni nini wanakifanya kumbuka taarifa za hao watu siku ya tukio la kutekwa na kuteswa kwa kibanda pia kumbuka kauli za NAPE na Riz 1 baada ya kuteswa Kibanda. Mjengwa na Ludovick wanaingizwa katika sakata ili kwa Lengo la Kumwingiza Lwakatare na tukio ili.
 
Back
Top Bottom